Kikwete ahutubia Taifa Julai 31 - hutuba ya mwisho

Hofstede.. unajua hilo wala hawakuwaambia wananchi mapema.. mimi nilidhani ni mfumo mpya wa kudumu kumbe ni wamuda tu.
 
Anateleza kidogo hapa na kusema kuwa Nyerere alizungumzia watu wanaobagua wenzao kwa misingi ya dini/ukabila/rangi etc ni wa kuwaogopa kama ukoma.............ukweli ni kuwa Nyerere alizungumzia watu wanaotumia pesa kukimbilia Ikulu ndio wa kuogopa kama ukoma..!

Sijui ni tatizo la speechwriter au mkuu aliongeza mwenyewe?

Chadema can make a very good political campaign clip out of haya maneno.
 
Maoni.
Hotuba za kila mwezi: Amesifia utaratibu huu na kusema utaendelea. Kumbukumbu zinaonyesha kuwa suala la Richmond lilipotinga bungeni hakutoa hotuba za mwezi kwa miezi 3 eti alikuwa safarini.!
Zanzibar: Amesema maamuzi na mijadala ilikuwa migumu kupitia kamati. Kikao cha butiama hakikutoa maamuzi yoyote ila kushabikia kura za maoni. Muafaka wa Znz ni jitihada za Seif na karume peke yao, isitumike ku score political point.
Kuhusu mfumo wa GNU amesema tutaungalia baada ya miaka 5 kutathmini. Ina maana hili jambo limefanyika bila maono''vision'' ya miaka ya mbeleni. Je hii si kazi ya zima moto!
Uchaguzi: Amesema tume imewezehwa kufanya kazi kwa ufanisi,na uchaguzi utakuwa wa ufanisi. Hakuna mahali aliposema ''uchaguzi huru na wa haki'' kuna mahali ametumia neno uhuru wa wanachi ..., kwahiyo anafamu tume si huru ndio maana anasisitiza ifanye kazi kwa ufanisi tu.
Kanuni: wananchi wasirande rande. Hivi ni kwanini wananchi wanaranda randa? ni kwasababu ya wizi wa kura hasa ukizingatia kuwa tume,polisi ni sehemu ya chama,haki ipo wapi. Wananchi waelewe jinsi ya kulinda haki zao. Mawakala,sasa kama CCM wanahonga kuteuliwa watakosa vipi milioni ya kumpa wakala.!! kama tume si huru haki ya mpizani ipo mashakani.wakala si jibu kamili ni sehemu ya jibu
Vyama: Amesema viache magenge. Mbona lile genge la CCM lililofanya uharibifu KCMC hospitali halikuchukuliwa hatua. Magenge ni yapi, au alimaanisha wapinzani
Barabara: Kama zipo sababu za msingi zilizohakikiwa kitaalamu na wataalam wetu,kuna sababu gani kufikiria jirani anasema nini katika maendeleo yetu ikiwa ni pamoja na utunzaji rasimali zetu wenyewe.
 
Anateleza kidogo hapa na kusema kuwa Nyerere alizungumzia watu wanaobagua wenzao kwa misingi ya dini/ukabila/rangi etc ni wa kuwaogopa kama ukoma.............ukweli ni kuwa Nyerere alizungumzia watu wanaotumia pesa kukimbilia Ikulu ndio wa kuogopa kama ukoma..!

Sijui ni tatizo la speechwriter au mkuu aliongeza mwenyewe?

Did he really said this, did his speech writer really write this? Wakuu kama kweli basi siasa ni mchezo wa kufanya watu wajinga.
 
Sielewi ni kwanini Kikwete ameona kuwa anawiwa maelezo na wa Kenya kuhusu barabara inayopita Serengeti iliyoko Tanzania?

Ni kama TZ ilivyogomewa kuuza bembe za ndovu na Kenya ,madhara ya mbuga hiyo yatakuwa mpaka Kenya ila ktk hili nadhani hawana nguvu ya kuzuia.
 
Mimi nilichoshangaa ni kuwa watanzania kweli tunaonekana sallow.Haya ndio maneno ya mwisho na ya msingi kwa rais kuzungumzia?
Kwa nini asiongele kuwa ajira kiasi gani zimeongezeka au kupungua ktk utawala wake.
Uchumi umekuwa kivipi maana wananchi kila siku wana hoji how inasemwa uchumi umekuwa wakati mambo ovyo ,bei za vitu juu kila kukicha.
Kwa nini asiongelee mambo yaliokusa taifa kuhusiana na maisha bora ,umeme, maji, afya.
Usalama wa raia kutokana na mauwaji yanayoendelea bongo ukizingatia kuna mtu potential ametoka kuuwawa.
Kwa kuongelea uchaguzi nampongeza safi,barabara ya serengeti zero maana ni kama ahadi kuwarainisha wananchi wa huko na imechukua sehemu kubwa I wonder.
Nampongeza pia kwa kupunguza kuchekacheka ,mengine zero-nada
 
kama kuna mtu mwenye full hotuba atuwekee tuweze kuipitia na kuichambua
 
Sielewi ni kwanini Kikwete ameona kuwa anawiwa maelezo na wa Kenya kuhusu barabara inayopita Serengeti iliyoko Tanzania?
Barabara hiyo italeta usumbufu mkubwa kwa wanyama ambao huwa wanaenda na kurudi Kenya.

Angalia kiambatanisho hapa chini
 
Attachments

  • serengeti.jpg
    serengeti.jpg
    50.2 KB · Views: 73
Mwanakijiji nakusikia unaguna "hah!" baada ya rais kusema "mfumo wa serikali ya umoja Zanzibar siyo wa milele" unajua hata mimi nimeshangaa yaani unapoitisha referendum si maana ya kubadili katiba? na anaposema kila baada ya miaka mitano watakuwa wanauangalia huu si uhuni?, yaani kila miaka mitano wazanzibar wawe wanapiga kura za maoni?. Maana kama jambo limeingizwa kwa kura ya maoni basi halilatoka pasi na kura hiyo hiyo kupigwa tena. Kwa mtazamo wangu hakukuwa na haja ya hii kura kama mtazamo ni huu wa kureview every five years.

Ufisadi mwingine huu wa kutumia hela za wananchi au kuna % itapita CCM kwenye hizo hela za kura za maoni
 
Mwanakijiji nakusikia unaguna "hah!" baada ya rais kusema "mfumo wa serikali ya umoja Zanzibar siyo wa milele" unajua hata mimi nimeshangaa yaani unapoitisha referendum si maana ya kubadili katiba? na anaposema kila baada ya miaka mitano watakuwa wanauangalia huu si uhuni?, yaani kila miaka mitano wazanzibar wawe wanapiga kura za maoni?. Maana kama jambo limeingizwa kwa kura ya maoni basi halilatoka pasi na kura hiyo hiyo kupigwa tena. Kwa mtazamo wangu hakukuwa na haja ya hii kura kama mtazamo ni huu wa kureview every five years.

huyu jamaa hana akili kabisa, so kura ya maoni mantiki yake nini, maana watu wakipiga kura ya maoni na kusema ndiyo maana kifungu hicho kinaingizwa kwenye katiba, huyu jamaa amewahi kuwa ji--loo, make haiingiii akilini mwa watu wenye upeo useme kitu kilichoamliwa na kura ya maoni kitakuwa reviewed after every 5yrs, sijawahi ona hili
 
Back
Top Bottom