Kikwete ahubiri Uzalendo kwa wanafunzi wa Tanzania, Beijing - China.

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi {CCM} na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo tarehe 20th April 2016 amekutana na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wa Tawi la Beijing ambao ni Wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu, katika Ukumbi wa Grand uliopo katika Makazi ya Viongozi ya Diaoyutai State Guesthouse jijini Beijin, nchini China.

Wakisoma risala yao, Wanafunzi hao kutoka vyuo mbalimbali vilivyopo Beijin na miji ya karibu kama vile Tianjin walimuhakikishia Mheshimiwa Dkt. Kikwete kuwa wao ni waaminifu na wazalendo kwa Taifa lao na kwamba wako tayari kurudi nyumbani na kutumia elimu zao katika kuhakikisha kuwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanafikiwa.

Katika mazungumzo na Wanachama hao, Mhe Kikwete amewakumbusha jukumu kubwa lililo mbele yao la kujenga Chama na kulijenga Taifa la Tanzania, katika hotuba yake ameeleza kuwa China imefanya Mapinduzi makubwa katika maendeleo na kuboresha ustawi wa watu wa nchi hiyo, hivyo kuwataka kujifunza na kuchukua maarifa ya China na kuyatumia wakirudi nchini ili kufanikisha Mapinduzi makubwa ya Kiuchumi na maendeleo kwa ujumla.

Mheshimiwa Kikwete na Ujumbe wake wanatarajia kutembelea Jimbo la Fu Zhou hapo kesho na kushuhudia maendeleo makubwa yaliyosimamiwa na Katibu Mkuu wa CCP na Rais wa Serikali ya watu wa China Mhe Xi Jinping, pamoja na kufanya mazungumzo muhimu na Viongozi wa Chama Cha Kikomunisti cha China {CCP} katika jimbo hilo.
leo.jpg
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa wanafunzi wa kitanzania wanaosoma China; Kutoka Kushoto ni Hilda, Seleman Serera, Mhe Jakaya Kikwete, Mwneyekiti wa wanafunzi Ndg Juma Mashenene na Katibu Ndg Hanifa Yusuph Mohamed.

sere.jpg

Miongoni mwa wanafunzi waliokitokeza kwenye kikao hicho Ndg Irene Msaki (kushoto) na Annastazia Gabriel.

sule.jpg

Mhe Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi watanzania wanaosoma nchini China.
 
Daaah aisee, huko sijui alipanda ndege gani maana sijui kama emirates zinaenda huko, au itakuwa alipanda British airways
 
Kwend china na korea from tz unatoka na Emirate hadi dubai then pale ndo unafaulisha ndege
 
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi {CCM} na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo tarehe 20th April 2016 amekutana na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wa Tawi la Beijing ambao ni Wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu, katika Ukumbi wa Grand uliopo katika Makazi ya Viongozi ya Diaoyutai State Guesthouse jijini Beijin, nchini China.

Wakisoma risala yao, Wanafunzi hao kutoka vyuo mbalimbali vilivyopo Beijin na miji ya karibu kama vile Tianjin walimuhakikishia Mheshimiwa Dkt. Kikwete kuwa wao ni waaminifu na wazalendo kwa Taifa lao na kwamba wako tayari kurudi nyumbani na kutumia elimu zao katika kuhakikisha kuwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanafikiwa.

Katika mazungumzo na Wanachama hao, Mhe Kikwete amewakumbusha jukumu kubwa lililo mbele yao la kujenga Chama na kulijenga Taifa la Tanzania, katika hotuba yake ameeleza kuwa China imefanya Mapinduzi makubwa katika maendeleo na kuboresha ustawi wa watu wa nchi hiyo, hivyo kuwataka kujifunza na kuchukua maarifa ya China na kuyatumia wakirudi nchini ili kufanikisha Mapinduzi makubwa ya Kiuchumi na maendeleo kwa ujumla.

Mheshimiwa Kikwete na Ujumbe wake wanatarajia kutembelea Jimbo la Fu Zhou hapo kesho na kushuhudia maendeleo makubwa yaliyosimamiwa na Katibu Mkuu wa CCP na Rais wa Serikali ya watu wa China Mhe Xi Jinping, pamoja na kufanya mazungumzo muhimu na Viongozi wa Chama Cha Kikomunisti cha China {CCP} katika jimbo hilo.View attachment 341529Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa wanafunzi wa kitanzania wanaosoma China; Kutoka Kushoto ni Hilda, Seleman Serera, Mhe Jakaya Kikwete, Mwneyekiti wa wanafunzi Ndg Juma Mashenene na Katibu Ndg Hanifa Yusuph Mohamed.

View attachment 341531
Miongoni mwa wanafunzi waliokitokeza kwenye kikao hicho Ndg Irene Msaki (kushoto) na Annastazia Gabriel.

View attachment 341532
Mhe Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi watanzania wanaosoma nchini China.

Tupe route, baada ya hapa wapi tena?
 
Kwamba baada ya hapo atarudi msoga sidhani, atatengeneza safari nyingine tu hata iweje ili mradi apande ndege

Najua, ndio maana nikauliza route, baada ya China anaenda wapi Chile, Jamaica au wapi? Maana najua hata akija Msonga, anapitia tu kusalimia.
 
Haya bana tumejua kuwa upo china baba!

Kikwete amestaafu, Sasa anaweza kuzunguka Dunia yote atakavyo kama kiu ya matembezi haijamwisha. Kama ana fedha za kuzunguka Duniani acha afanye hivyo. Hata Nyerere alitembea sana baada ya kustaafu Uraisi, alipokuwa Mwenyekiti wa South- South Commission alitembea sehemu nyingi sana za Dunia
 
pia anaendelea kuitafutia nchi fursa mbalimbali, pia anaboresha diplomasia ya nchi, ndo maana magufuli hasafiri sana jk anamsaidia, tuangalie lengo la hiyo ziara, sio kulaumu tu kuwa anapenda kusafiri. endelea kuvutia wawekezaji na magufuli simamia serikali vema.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom