Kikwete ahofia kung'olewa CCM kwa madai ya kushindwa kukiendesha chama

mtundu

Member
Oct 6, 2011
22
7
RAIS Jakaya Kikwete sasa anakabiliwa na wimbi zito la kujinasua kutoka kwenye mpango unaosukwa na makada wa chama hicho kumng'oa kwenye nafasi ya mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Makundi yanayotaka kumng'oa yanadai ameshindwa kukiendesha chama, na hali hiyo imeifanya serikali kuwa goigoi.

Habari* zinadai kuwa baadhi ya wanachama wakiongozwa na wajumbe kadhaa wa Halmashauri Kuu (NEC), watokao Kanda ya Ziwa ndio wamekuwa wanaandaa mkakati wa mabadiliko ya kile wanachoita ‘kukinusuru chama.'

Zinaongeza kuwa Rais Kikwete ameshindwa kukiendesha chama hicho na matokeo yake ni kuwa makundi yanayohasimiana yameshamiri na kuharibu taswira ya CCM.

"Kwa hali ilivyo sasa lolote linaweza kutokea, maana watu wamechoshwa na mwenyekiti wetu ambaye amekuwa kinara wa kuchochea siasa za makundi," alisema kada mmoja.

Chanzo kimoja* kilisema* kuwa Rais Mkapa hivi sasa anaonekana kuwa kiongozi imara zaidi ndiyo maana alikabidhiwa jukumu la kuzindua na kufunga kampeni za chama hicho katika Jimbo la Igunga.

HABARI YOTE IPO HAPA << KIKWETE AHOFIA KUNG'OLEWA>>

NAOMBA MNISAIDIE WANA JF:

1.JE INAWEZEKANAJE RAISI ASTAAFU HALAFU ARUDI MADARAKANI TENA?

2.KWA MIAKA NENDA RUDI,NIMEKUWA NIKIONA KUWA RAISI NDIYE MWENYEKETI WA CHAMA,,VIPI MIPANGO HII YA KUMPENDEKEZA MKAPA NA SALM AHMED SALIM? INAWEZEKANA?
 
Mkapa hafai ndiye aliyeuza kwa fujo mali zetu!kurudi madarakani kwa rais hakuna shida mbona putin wa russia anarudi madarakani ili mradi uwe mtendaji mzuri.fikiria rwanda wangempa kagame miaka 10 huenda wasingekua na maendeleo kama waliyoyafikia sasa
 
mkapa hafai ndiye aliyeuza kwa fujo mali zetu!kurudi madarakani kwa rais hakuna shida mbona putin wa russia anarudi madarakani ili mradi uwe mtendaji mzuri.fikiria rwanda wangempa kagame miaka 10 huenda wasingekua na maendeleo kama waliyoyafikia sasa

kama ni kweli aliuza mali zetu kwa fujo,iwaje ccm wanataka kumpa ngazi ya juu kiasi hicho?
 
Kuna watu wachache sana ndani ya CCM leo ambao wanaweza kusimama na kunyooshea wenzao vidole kwa dhamira ya dhati ya kutaka kukinusuru chama hicho. Hayo makiundi yanayohasimiana ni wale wale tu ambao wanapigania vita matumbo yao
 

1.JE INAWEZEKANAJE RAISI ASTAAFU HALAFU ARUDI MADARAKANI TENA?

2.KWA MIAKA NENDA RUDI,NIMEKUWA NIKIONA KUWA RAISI NDIYE MWENYEKETI WA CHAMA,,VIPI MIPANGO HII YA KUMPENDEKEZA MKAPA NA SALM AHMED SALIM? INAWEZEKANA?

ni mazoea tu kuwa rais ndo awe mwenyekiti wa chama, lakini haiko kwenye katiba yao. wanaweza kumpa mwingine na ndipo raisi atasaidiwa kazi kwani atalazimika kutekeleza matakwa/ilani ya chama chake. kwa sasa yeye ni kila kitu.

kama ana hofu, ni ishira ya uchu wa madaraka.
 
ni mazoea tu kuwa rais ndo awe mwenyekiti wa chama, lakini haiko kwenye katiba yao. Wanaweza kumpa mwingine na ndipo raisi atasaidiwa kazi kwani atalazimika kutekeleza matakwa/ilani ya chama chake. Kwa sasa yeye ni kila kitu.

Kama ana hofu, ni ishira ya uchu wa madaraka.

asante mkuu kwa kunifungua.nilikuwa sijui
 
Unajua JK anachokosea ni kitu kidogo, maamuzi dhaifu na huruma. Alitangaza kuwa CCM itajivua gamba ameshindwa kutekeleza nadharia hiyo kwa vitendo lakini amesahau magamba tayari yameshadhalilika kwa kauli yake hiyo. Hivyo akuanzae mmalize, JK ameyachokoza magamba na ameshindwa kuyang'oa ngoja yammalize sasa.
 
haya ni mambo ya kichama siyo serikali.kama katiba ya chama chao inaruhusu mwenyekiti mstaafu kurua kugombea uwenyekiti upya hamna tatizo
 
jk aendeleza udhaifu wake na makundi ktk chama na hatimaye wasambaratike, wapinzani waendelee kujiimarisha kwa ajili ya kuchua dola.
 
jk aendeleza udhaifu wake na makundi ktk chama na hatimaye wasambaratike, wapinzani waendelee kujiimarisha kwa ajili ya kuchua dola.
JK sio chama, yeye ataondoka lakini chama kitabaki. Atakuja mwingine na atapita kiulaini tu. Mimi nashauri na CDM wafate hivyo maana naona CDM ni watu sio chama. Leo Mbowe au Slaa akitoka basi CDM miguu juu.
 
Hapo kweli inatakiwa mipango ya kukiimarisha chama na sioni tatizo kwa Mkapa kurudi kama wanaona ndie mtu anayeweza kukiunganisha chama.
 
Mimi natamani waendelee kuraruana tu ili hatimae tutoke kwenye wilderness,hili jambo ni zuri sana kwa mustakabali wa taifa letu.
 
Sasa hapo dhana nzima ya kujivua gamba ndio inafanya kazi-yaani mabadiliko ya kimfumo na uendeshaji wa chama-.Tatizo la magamba ni conservative wanadhani zama hizi bado ni za enzi za mwalimu! ndio maana hata nchi inaelekea shimoni kwa kukumbatia idea za kizamani bila kuruhusu mabadiliko kulingana na wakati tuliopo sasa.Magwanda nao wajifunze wasivimbe kichwa kwa kujiona wako safe kwani wind of change hupita kote kote,ni swala la muda tu! magamba wa ngazi ya juu wakubaliane na wanachama wanachotaka kwani waliwasha wenyewe moto wa kuvua gamba sasa wasilalamike ukiwaunguza! nawapongèza hao wenye lengo hilo kwani sasa wanaifanyia kazi dhana ya kuvua gamba yaani change of system!
 
JK hawezi kukubali chama Kimvunjikie.Atakuwa amejiingiza ktk record ya mwenyekiti aliyefanikiwa kukivunja chama cha Mapinduzi.No one would like to go down in history with that kind of Record
 
CCM KWA SASA WAPO TAYALI KUKODI VIONGOZI KUTOKA NJE YA NCHI ILI KUKINUSURU CHAMA! watalalama sana kwakuwa wanaolalama ni wale waliowekeza kidogo (wenye hisa chache) lakini mtu kam EL huwezi kuona analalamika kwakuwa anahisa za kutosha kufanya maamuzi.
 
Jk ma' president u had a very gud vision na chama... Bt da pbm is on approach ur usin... I knw u ve a true willin ya kueliminate viwavi wote wanaotafuna chama na nchi bt ur main weaknes is ur weak wen it comes 2 mek a decision... Don wory ma' presidnt chinjia baharini viwavi wote... And am assured u wil b remembrd as a only president who transform DIRTY CCM 2 CLEAN CCM... Go JK...
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom