HARAKATI za kuwania urais zinahusishwa kuandaliwa kwa mtandao mpya wa Rais Jakaya Kikwete ambao unadaiwa unawarejesha baadhi ya wajumbe wake wa zamani, unampigia debe Spika Samuel Sitta na umetanuliwa hadi kuwashirikisha baadhi ya viongozi wa vyama vya Upinzani, Raia Mwema imeelezwa.
Kwa mujibu wa habari zilizotufikia, juhudi hizo zinalenga kumfanya Rais Kikwete kupigiwa kura ya ‘ndiyo au hapana' kama ilivyokuwa wakati wa mfumo wa chama kimoja. Ili kufanikisha mpango huo, baadhi ya vyama vya Upinzani havitarajii kusimamisha wagombea urais na badala yake watajielekeza kwenye kuwania nafasi za ubunge.
Mbali na mtandao huo mpya kutema wanamtandao wa zamani waliochafuka kwa kashfa za ufisadi, unatajwa pia kuhusisha baadhi ya wanaharakati na kundi teule la vijana katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), baadhi wakiwa karibu na familia ya Kikwete.
Hata hivyo, wakati hayo yakitokea ndani ya CCM zimekuwapo taarifa kwamba baadhi ya vigogo wa chama hicho wanawashawishi wenzao kuchukua fomu za kuwania urais ili kumpinga Rais Kikwete, huku kukiwa na juhudi na mikakati ya kuwazima watu hao.
Pamoja na juhudi hizo kupata vizingiti ndani na nje ya CCM, baadhi ya jumuiya za CCM ambazo viongozi wake wakuu wametangaza kumuunga mkono Kikwete.
Inaelezwa kuwa wanaoshawishiwa bado hawajaonyesha nia dhahiri kukubali ama hata kukataa waziwazi ushawishi huo wakihofia kile kinachotajwa kuwa ni utamaduni wa CCM kumwacha Rais aliye madarakani kuongoza kwa mihula miwili.
Rais Kikwete
Sababu nyingine inaelezwa kuwa ni wanaoshawishiwa kumpinga Kikwete ndani ya CCM kujawa na hofu endapo wakishindwa hali itakayowagharimu katika nafasi nyingine za uongozi.
Moja ya sababu zinazotumika kushawishi baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM kumpinga Kikwete ni kile kinachotajwa kuwa ugumu wake katika kuamua masuala muhimu kwa Taifa, ikiwamo kusimamia misingi ya chama hicho katika kupambana na mitandao ya kifisadi ambayo si tu imejiimarisha CCM bali hata katika Serikali yake, kuanzia ngazi ya Baraza la Mawaziri.
Wakati hali ikiwa hivyo ndani ya CCM, katika vyama vya Upinzani wenyeviti wa baadhi ya vyama hivyo ambao wamekuwa wakigombea urais sasa wametangaza kuachana na azma hiyo. Miongoni mwao ni Freeman Mbowe, ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo.
Mbowe anajiandaa kuwania ubunge katika Jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro ambalo alipata kuliwakilisha bungeni. Jimbo hilo sasa linashikiliwa na Mbunge wa CCM, Fuya Kimbita.
Awali duru za kisiasa zilibainisha kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa ndiye atakayeteuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho lakini sasa mpango huo haupo na Dk. Slaa anatarajiwa kuwania tena ubunge katika Jimbo la Karatu, ambako anatajwa kuwa na nguvu kubwa kisiasa. Yeye mwenyewe amepata kukana waziwazi kuwa ana mpango wa kuwania urais.
Sintofahamu pia imejitokeza katika Chama Cha Wananchi (CUF) ambacho kimekuwa na kawaida ya kumsimamisha Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye amewania nafasi hiyo mara tatu bila mafanikio makubwa.
Sasa chama hicho kimekaa kimya kuhusu uamuzi wake wa kuweka au kutoweka mgombea ikidaiwa kuwa ki mbioni kuimarisha uswahiba na CCM.
Uswahiba wa CUF na CCM umeanzia Zanzibar ambako ndiko iliko ngome kuu ya chama hicho kwa kiongozi mwenye nguvu na mzoefu, Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad kukutana na Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, kabla ya kutaka Rais huyo aongezewe muda wa urais, msimamo ambao bado unaichanganya CUF na CCM sawia.
Mbali ya uamuzi huo wa Seif, hatua ya Rais Kikwete kumteua msaidizi muhimu wa Seif, Ismael Jussa Ladhu, kuwa Mbunge, umeelezwa kuwa moja ya mikakati ya CCM kuimarisha mahusiano yake na CUF kwa kigezo cha kile kinachoitwa "maridhiano ya Kitaifa."
Chama cha NCCR-Mageuzi ambacho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 kilimteua Dk. Sengodo Mvungi, kuwania urais bado kimebaki kimya huku Mwenyekiti wake, James Mbatia, akitangaza nia yake ya kuwania ubunge katika Jimbo la Kawe, jijini Dar es Salaam, ambalo kwa sasa linaongozwa na Rita Mlaki wa CCM.
NCCR-Mageuzi pia imekuwa ikitoa matamko kadhaa yanayoashiria kuonyesha kuwa chama hicho sasa hakina ‘ugomvi' sana na CCM baada ya Kikwete kuingia madarakani.
Augustine Mrema, Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) amekwisha kuweka wazi kwamba kiu yake ya urais imetoweka na kwa ajili hiyo hatowania urais, badala yake atakwenda kuwania ubunge katika Jimbo la kwao la Vunjo, Kilimanjaro linaloshikiliwa na Aloyce Kimaro. Mrema ni kati ya viongozi wa Upinzani waliokwisha kutangaza waziwazi kumuunga mkono Rais Kikwete.
Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo ambaye aliwania urais mwaka 1995 na mwaka 2000, aliona busara ya kwenda jimboni mwaka 2005, akafanikiwa kuwa mbunge, sasa anajiandaa kutetea nafasi yake hatua hiyo ikiacha chama chake bila mgombea wa urais.
Katika harakati za kuzuia upinzani dhidi ya Rais Kikwete, mtabiri maarufu nchini Sheikh Yahya Hussein wa Dar es Salaam naye alijitumbukiza ulingoni kwa kutabiri vifo kwa ambao wangejitokeza.
Ni ajabu kwamba kuna pilikapilika za kutaka Rais Kikwete awe mgombea pekee ikizingatiwa kwamba ana historia ya kuingia ulingoni tangu mwaka 1995 alipojitosa kuwania nafasi ya kupitishwa ndani ya CCM kabla ya kupitishwa Benjamin Mkapa.
Katika hatua nyingine juhudi binafsi za Kikwete kwa kugharamiwa na baadhi ya rafiki zake zimekuwa zikielekezwa kuhakikisha makundi yanayotishia uhai wa CCM yanamalizwa huku akitumia nafasi hiyo kuwatumia vijana na watu wake wa ndani kufanya kampeni nchi nzima.