Kikwete aguswa kifo cha Rais wa kwanza Algeria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete aguswa kifo cha Rais wa kwanza Algeria

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tume ya Katiba, Apr 14, 2012.

 1. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  RAIS Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria, Abdelaziz Bouteflika kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Kwanza wa nchi hiyo, Ahmed Ben Bella.

  Katika salamu zake kwa Rais wa Algeria alilozitoa jana kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Rais Kikwete alieleza kushtushwa kwake na taarifa za kusikitisha za msiba huo wa Baba wa Taifa wa nchi hiyo kilichotokea Aprili 11 mwaka huu katika mji wa Algiers.

  “Nimeshtushwa sana na kifo cha Baba wa Taifa lenu, kwa niaba ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa niaba yangu, ninawapa pole kwa msiba huu na kupitia wewe unifikishie pole yangu kwa familia, ndugu na wananchi wa Algeria,” alisema Kikwete.

  Alisema Tanzania daima itamkumbuka hayati Ahmed Ben Bella kwa juhudi kubwa alizozifanya kujenga uhusiano mzuri baina ya nchi hizo mbili (Tanzania na Algeria) hadi leo.

  Rais Kikwete pia alisema atakumbukwa kama Mwana wa Afrika hasa kutokana na kusimamia umoja na maslahi ya Waafrika.

  “Hakika Waafrika tumempoteza mmoja kiongozi mwanamapinduzi aliyetoa maisha yake si tu kwa uhuru wa Algeria bali wa mataifa mengine ya Afrika yaliyokuwa bado chini ya wakoloni.”

  Akieleza zaidi namna Bella alivyokuwa, Rais Kikwete alisema pia alikuwa mhimili chanya wa
  kupigania amani na utulivu kwa Afrika kwa umakini mkubwa kama Mwenyekiti wa Jukwaa la Busara (Pannel of the Wise) la nchi za Umoja wa Afrika (AU).

  “Katika kipindi hiki kigumu, tunaungana nanyi kumuomba Mwenyezi Mungu awajalie familia
  ya marehemu na wananchi wote wa Algeria faraja na moyo wa subira kwa msiba huu na aipumzishe roho yake mahala pema peponi,” alisema Kikwete katika salamu zake hizo.

  Kwa mujibu wa familia ya marehemu, Bella aliyekuwa na umri wa miaka 95 alifariki Aprili 11 mwaka huu nyumbani kwake Algiers.

  Alikuwa Rais wa kwanza wa Algeria mwaka 1962 hadi 1965 baada ya nchi hiyo kupata uhuru kutoka kwa Wafaransa.

  Utawala wale mwaka 1965 uliangushwa na aliyekuwa Waziri wake wa Ulinzi, Houri Boumediene ambaye anaelezwa kuwa ni mshirika wa karibu wa Rais wa sasa

  HabariLeo | Kikwete aguswa kifo cha Rais wa kwanza Algeria
   
 2. Goheki

  Goheki JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 270
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kwani hatahudhiria mazishi?
   
Loading...