Kikwete agoma kusaini waraka kuhusu wabunge kujipandishia posho

Anasubiri kwanza asikie kuna wabunge fulani wanataka kuonana naye Ikulu kutoa maoni kuhusu posho, halafu baadaye NEC ya CCM itoe ruhusa kwa makundi mengine kumuona pia, halafu litokee kundi lingine kumtembelea Ikulu kupeleka maoni yake, halafu ndio atie saini na kusema mjadala wa posho unaruhusiwa kuendelea hata baada ya saini yake!

Mkuu huu u-great thinker hapa umetulia! Na inawezekana kufanya hivyo.
 
Af hawa watu mbona wanataka kutufanya Watanganyika hatuna akili?! Mbona Spika amesema zimeshaanza kulipwa toka tar 8/11?!

Inamaana zilianza kulipwa kabla rais hajasaini? Au walimzarau kwamba hana ujanja wakutosaini? Mtazamo wangu jamaa ashasaini anatupiga changa la macho ili tumwone mwema japo sivyo
 
Labda Kikwete kakosa muda wa kusaini. Anavyosainigi haraka haraka, tena kwa mbwembwe bila hata kufahamu kilichomo! Kama ni kweli alidhamiria kutosaini kwaajili ya hali ya Nchi, na kwamba hawastahili kuongezewa kiasi hicho, aseme wazi. Watanzania tuna haki ya kufahamu msimamo wake katika suala hilo. Bi kiroboto hajui azungumzalo, tumsamehe bure, kwani hata uspika kazawadiwa.

Yaani wanafunzi wa Vyuo Vikuu wananyimwa kuongezewa 2500, walau ili ifike 10,000/- yeye anasema maisha Dodoma ni magumu, UDOM ipo Arusha? St. Johns?, Mipango, Madini? Na vyuo vingine vilivyoomba kuongezewa walau kiasi hicho ili waweze kula kwa siku?
Yaani basi tu Nchi ikishaingia ulajiulaji unaohalalishwa na wapumbavu fulani basi tu.

Nasema tena JK labda hajausaini kwa kukosa nafasi, kama sivyo aseme, kinyume chake hakuna haja ya kuanza kumpongeza. Maana tunafahamu kuwa yeye ni kinara wa kusaini mambo haraka haraka kishabiki bila hata kuchunguza.

mkuu nimeipenda hapo kuwa maisha ya dodoma ni magumu inamaana udom wanasavaivo je kwa 7500 per day huku mbunge kwa 70000 na maalawans mengine kibao ashindwe?
 
propaganda za CCM Kikwete asisaini Kashililah amepata wapi pesa alizowaongezea wabunge kwenye akaunti zao asizozielezea ,jamani wananchi tunaweza tukatambua uongo wao Raisi si saini ,Mkulo niko gizani Spika wameshalipwa,kashililah wamelipwa lakini sio posho what a hell
 
It doesn't matter.....In Tanzania.. everything is possible.. hata kama posho ingepandishwa to 70,000 hadi 1,000,000 kwa siku.. Watu watapiga kelele, wataandika kwenye magazeti, wataandika kwenye blog & JF, lakini at the end, watarudi kwenye umasikini, kulala kwenye giza, kukosa maji, kukosa madawa, kukosa chakula na mwisho watu watatoa tabasamu pevu kwa wale wanao-wadhulumu.. ..Ni moja ya maajabu 7 ya dunia! Where is our line in a Guinness World Records book?

Hapo ndipo watz wananiacha hoi, wanayasahau mambo mapema mno bila kuchukua hatua
 
Mhe Rais Kikwete,

Japo natamani sana nikupe hongera KATIKA HILI la kuamka japo kwa kuchelewa na kuanza kulinda maslahi ya umma (sisi walipakodi badala ya ulinzi wa maslahi ya CCM) kwa kudaiwa kugomea kuidhinisha posho hizi kwa wabunge wasiotuletea tija yoyote hadi leo hii lakini mwenzio nasita sana.

Ndio, Rais wangu nasema moyo unnisita kukupongeza juu ya hili tena naogopa sana kufanya hivo maana sielewi ni dakika ya ngapi mara baada ya kukupongeza juu ya hilo hata utakaponigeuka na kurudi kinyumenyume kwenda kutilia sahihi yako ya kubariki zoezi hili chukizo bila kujali tulivyo sakafuni kabisa hivi sasa kwa ugumu wa maisha ile mbaya!!!

Hivi utakua umewahi kurudi nyuma kidogo hata ukajiuliza kwamba pindi unaopoonekana kujikita zaidi juu ya ULINZI WA MASLAHI BINAFSI YA CCM KWA GHARAMA YA KODI ZETU HATA TUSIO WANACHAMA HUKU UKITELEKEZA MASLAHI YA UMMA NZIMA wa nchi hii mwenzetu umewahi hata kuhisi uhalali wa aina ya ukichaa ambao huwa unatupanda vichwani kwa maonevu ya aina hiyo Baba?

Huku unapoendelea kutaafakari juu ya hilo, hebu mie niacheni kwanza nikajivutie pumsi kwanza kuangalia upepo wa ustaarabu mzima hapa.

unataka ukuu wa mkoa au wa wila? Maana naona unapongeza upupu jamaa kafanya lipi lakupongeza?Acha wehu
 
Kaka umeongea neno hii mijiongozi inajijali yenyewe,na kumsahau kijana aliye mtaan kwa kukosa ajila hvo kuishia kuwa mpiga nondo,inamsahau mama mjamzito anayejifungua katika mahospital yasiyo na hadhi,yanasahau walimu ambao wamewezesha yafike hapo,pia yanasahau yalikotoka,hii yawezekana ni laana na ndo maana mijitumbo inasogea mbele kwa kutumia visivo halal.
 
>> Katibu Wa Bunge (Hakuna Ongezeko La Posho)

>> Spika Wa Bunge (ongezeko La Posho Liko Tokea 8/11)

>> Rais (Agoma Kusaini Waraka.)

Nimuamini nani kati ya hawa? Nitegemee nini kutoka kwa hawa? Na Je ni kipi kinafuat?

Wanatudhihirishia niwaropokaji na watu wasiokuwa na ushirikiano katika utendaji wao japo ni chama kimoja
 
Yule anaitwa ****** bana hivi ndo kabila linaloongoza kwa usanii TZ nini maana jama anawazidi mpaka akina kanumba kwa usanii
 
Hee! imekuwa kuwaje tena mpaka anamsaliti Mhishimiwa Supika??
 
>> Katibu Wa Bunge (Hakuna Ongezeko La Posho)

>> Spika Wa Bunge (ongezeko La Posho Liko Tokea 8/11)

>> Rais (Agoma Kusaini Waraka.)

Nimuamini nani kati ya hawa? Nitegemee nini kutoka kwa hawa? Na Je ni kipi kinafuat?
ni kwamba JK ameshasaini ila anaona upepo unakuwa mmbaya ndio maana anazugisha
 
Si atie sahihi tu yaishe!?

Mkapa kesha mwambia asiwe kama Rais Robot !

He have to reason and think deeply before signing of anything submitted to him.
Kwa kweli hivi sasa Watanzania tunapitia kipindi kigumu sana tangu nchi yetu ipate UHURU. Hatuna Rais mwenye busara pale Ikulu,Kiwete amekaa pale kama zezeta tu hana moja wala mbili.

Kusema la ukweli Kiwete HAKUPASWA AWE RAIS HATA KWA AWAMU YA MASAA. He is a bogus President ever!
 
Taarifa kuwa bado kuna watumishi wa umma ambao hawajalipwa mishahara zinatia mashaka uwezo wa Serikali kifedha. TRA wanajitapa kila kukicha kuvuka malengo katika kukusanya kodi, lakini swali linakuja, hayo malengo ni sahihi kiasi gani?

Nadhani malengo hayo yaliwekwa ili kuwapa ujiko watu kwani nijuavyo mimi ni asilimia ndogo sana ya watanzania wanalipa kodi na wale wanaolipa wanalipa kidogo sana ukilinganisha na kile walichostahili kulipa.

TRA inanuka rushwa, ukitaka kujua hilo wewe jaribu kutaka kulipa kodi kisheria bila kuongea na afisa wa TRA, watakubamiza kuliko kawaida na kama una mzigo utautoa baada ya muda mrefu sana. Hii ndio Tanzania ambayo Serikali yake inashindwa leo kulipa mishahara ya watumishi wake kwa wakati.

Kuna haja ya viongozi wetu kuchukua hatua za dhati kuongeza makusanyo. Kikwete nakuaminia, fanya mageuzi katika hilo ili nchi isonge mbele. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
Pamoja na yote hayo sidhani ka TRA ni tatizo kubwa, Matatizo yapo kwa hao watumiaji wa hz KODI (serikali)
 
Hivi ndivyo alivyobandika ukurasa wake wa fesibuku.

https://www.jamiiforums.com/ 276361_100002217546016_1623176887_q.jpg

[h=6]Jakaya Kikwete
[/h][h=6]Baadhi ya ujumbe/maoni toka kwenu:

1."Hello Rais wangu. Serikali kwa sasa sio sikivu tu bali imekuwa na upole uliopitiliza kiasi kwamba wanasiasa uchwara na wanaharakati uchwara wanaitumia nafasi hiyo vibaya.Serikali ikiendelea kuwa kimya katika hili ni hatari kwa mustakabali wa Taifa letu. Freedom of speech ni kubwa mno. Mungu ibariki Tanzania. Kazi njema." (Max)

2."Sometime people talk without... thinking critically but I belive you are the best may God help you and our nation." (Mathew)

3."Posho za Wabunge toka 70,000 TZS hadi 200,000TZS ni mzigo kwa wananchi, tafadhali simamia jambo hili mapema. Tuangalie na sisi waalimu pia. Hali yetu ni mbaya sana." (Salim)

4."Ajira baba, ajira. Elimu zetu hazitufundishi ujasiriamali. Tunamaliza masomo na kukosa ajira. Tumejazana mitaani. Tumia miaka iliyobaki kututatulia tatizo hili." (Gratian)

5."Hivi suala la umeme limefikia wapi? Ki ukweli naona wizara imeshindwa kupata ufumbuzi wa kudumu. Mbona tuko nyuma sana? Hakuna vyanzo vingine?" (Mabula)

6. "Mr. President, I am an engineer, have some ideas that can help in solving the electricity problem. How do I reach you?" (Sameer)

7."Mheshimiwa Rais pole na kazi. Hivi suala la Katiba limefikia wapi? Kwa nini tunahitaji Katiba mpya? Naomba usimamie utoaji wa elimu kuhusu Katiba. Nina wasiwasi wananchi tutaburuzwa na ninyi wachache, wanasiasa na wasomi katika suala la katiba, wengi hatujui nini kinaendelea. Asante." (Ibrahim)

8. "Tafadhali dhibiti uhuru wa kutoa maoni. Imekuwa too much sasa. Watu wanautumia vibaya. Ni hilo tu kwa leo." (Halima)

9."Mpango wa shule za kata unakosa waalimu makini na vifaa bora Mheshimiwa Rais, shule zipo sawa lakini je hizi changamoto za waalimu na vifaa zinakabiliwa kwa wakati?" (Sandra)

10. "Hallow Mr President, I should first congratulate you for using Facebook media, for this enables people to interact with you freely. The Legal and Human Rights centre have posted a video, depicting actions of police brutality in Iringa. I think the police involved should be brought to justice." (Abdallah)
[/h]
 
Back
Top Bottom