Kikwete agoma kusaini waraka kuhusu wabunge kujipandishia posho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete agoma kusaini waraka kuhusu wabunge kujipandishia posho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mluga, Dec 8, 2011.

 1. mluga

  mluga JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 678
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  [h=1]Kikwete agoma kusaini waraka[/h] Posho za Wabunge

  Mwandishi Wetu

  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete

  Wabunge wageukana, sasa 'kidole na jicho'

  RAIS wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, anatajwa kugoma kutia saini waraka wa mapendekezo ya viwango vipya vya ongezeko la posho za “kukaa kitako” bungeni zinazolipwa kwa wabunge kutoka Sh. 70,000 za sasa hadi Sh. 200,000, Raia Mwema limeelezwa.

  Habari zinasema, wakati Kikwete akigoma kusaini waraka huo wa posho, zipo taarifa kuwa malipo ya posho mpya yamekwishafanyika kinyemela kwa matarajio kuwa angesaini.

  Hata hivyo, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila, amekana kufanya malipo hayo akisema kiasi cha ziada kilicholipwa kwa wabunge ni stahili isiyohusiana na nyongeza ya posho.

  Kwa upande wake, Kikwete amegoma kutia saini waraka husika kwa mujibu wa mamlaka yake. Taratibu zilizopo ni kwamba, Rais hufikishiwa mapendekezo hayo na yeye anaweza kuidhinisha kwa kutia saini ikiwa ni kibali kinachowezesha Bunge kwenda Wizara ya Fedha kuchukua fedha hizo tayari kwa shughuli iliyokusudiwa.

  Mbali na kibali hicho cha Rais kuwezesha Bunge kupewa fungu la fedha husika kutoka Hazina (Wizara ya Fedha) lakini pia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) hufanya ukaguzi wa hesabu husika kwa kutumia masharti yaliyopo kwenye waraka unaotiwa saini na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya uhakika vya habari, Rais Kikwete alipelekewa waraka huo mapema na ilitarajiwa angeweza kutia saini haraka; lakini imekuwa kinyume, kielezwa kuwa ‘kelele’ za makundi mbalimbali ya jamii zimechangia kumfanya asite kutia saini kama ilivyotarajiwa.

  “Huo waraka wa mapendekezo ni kweli umefikishwa kwa Rais kwa muda sasa lakini hajatia saini, ingawa anakubali posho za sasa haziwatoshi wabunge lakini pia anatambua kuwa hali ya uchumi kwa mwananchi mmoja mmoja si nzuri, na kwa hiyo, ni vema hili suala kulishughulikia kwa umakini mkubwa”, kilieleza chanzo chetu cha habari kutoka Ikulu.

  Wakati hali ikiwa hivyo kwa upande wa Rais, taarifa za Bunge zinaeleza kuwa mchakato wa nyongeza za posho ulipitia hatua karibu zote katika Bunge.

  Hatua hizo ni pamoja na kujadiliwa na kupitishwa na Tume ya Bunge inayoundwa na makamishna ambao ni wabunge pia, Kamati ya Uongozi ya Bunge inayoundwa na wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge na mwisho, wabunge wote kupewa muhtasari husika na kujadili na kisha, kukubali au kutokubali taarifa husika.

  Kwa hiyo, Raia Mwema, kupitia vyanzo vyake vya habari, limejiridhisha kuwa Bunge lilifikia uamuzi wa kuongeza posho hizo na wabunge wa kambi ya upinzani na chama tawala kwa ujumla wao, walikubali uamuzi huo.

  Inaelezwa kuwa mbunge pekee mwenye msimamo mkali dhidi ya kuchukua posho ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, ambaye hata hizi posho za zamani amegoma kuzichukua kwa muda mrefu sasa.

  Hata hivyo, wabunge wenzake katika chama chake wamekuwa wakichukua posho hizo na hata zile za semina mbalimbali kwa wabunge, ikiwamo semina iliyofadhiliwa na fedha kutoka Wizara ya Nishati na Madini, na kugharimu kibarua cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, David Jairo.

  Mbali na uamuzi huo wa Rais kutosaini ili kuidhinisha posho mpya, kumekuwa na madai kwamba katika Bunge lililopita wabunge walilipwa posho hizo kwa viwango vipya kabla ya kuidhinishwa na kwamba kwa sasa, wanaweza kutakiwa kuzirejesha kwa njia ya makato yenye utaratibu maalumu.

  Kutokana na madai hayo, Raia Mwema iliwasiliana na Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila ambaye alikiri wabunge kulipwa kiwango fulani cha ziada cha fedha lakini akikanusha kuwa si nyongeza ya posho kama ilivyoelezwa.

  “Si kweli wabunge wamelipwa hizo posho mpya. Hakuna aliyelipwa. Mimi nitapata wapi fedha za kuwalipa....kutoka kwenye fungu gani? Kwa sababu hadi sasa hakuna kibali chochote kilichotolewa kutoka mamlaka husika kwamba posho zimeongezwa, haya mambo yanazo taratibu zake za kisheria....si utashi wangu kusema posho imepanda na kwa hiyo niwalipe wabunge.”

  “Kwa hiyo, uongozi wa Bunge hauwezi kufanya uamuzi wowote nje ya taratibu za kisheria zilizopo. Hata kama hiyo posho ingekuwa imepanda, kuna maswali mengi ya kujiuliza na kupata majibu. Je, viwango vipya vinapaswa kuanza kulipwa wakati gani, je, ni kuanzia mikutano iliyopita ya Bunge? Je, ni kuanzia mwanzo wa Bunge hili au kuanzia mikutano ijayo ya Bunge?” alisema Kashilila.

  Katika hatua nyingine, Raia Mwema imebaini kuwapo kwa mawasiliano yasiyo rasmi kati ya Rais na baadhi ya wabunge, wakimshauri kutoongeza posho hizo kwa sababu kufanya hivyo ni kuzidisha pengo kati ya wenye nacho na wasio nacho katika jamii ya Watanzania, wengi wao wakiwa masikini.

  “Wapo ambao wameamua kumpa ushauri Rais kwamba si wakati muafaka kutia saini waraka wa nyongeza ya posho mpya. Wanadhani kwamba kuna sababu nyingi za msingi ambazo zinahusisha hali za Watanzania wa kawaida, wakiwamo watumishi wa Serikali na kubwa zaidi, hali ya uchumi haijatulia kiasi hicho,” alieleza mmoja wa wasaidizi wa Rais Kikwete.

  Kutokana na ushauri huo kwake, Rais Kikwete ananukuliwa akiwajibu kwa kusema; “Mimi ndiyo mwamuzi wa mwisho.”

  Lakini wakati hali ikiwa hivyo, yapo mapendekezo mengine mbadala miongoni mwa wabunge na baadhi ya viongozi waandamizi serikalini ambao hata hivyo, wamekataa majina yao yasiandikwe gazetini kwa sasa.

  Wabunge na maofisa hao wanapendekeza kuwa posho ya ‘kukaa kitako’ bungeni si lazima kuongezwa, lakini malipo kwa wabunge yanayostahili nyongeza ni malipo ya posho ya kujikimu wakiwa nje ya kituo cha kazi (per diem).

  Kwa sasa wabunge hulipwa posho ya kujikimu Sh. 80,000 kwa siku. Posho nyingine ni mafuta Sh. 50,000 kila mwezi na posho ya ‘kukaa kitako’ (sitting allowance) bungeni Sh.70,000.

  Wabunge na maofisa hao wanashauri nyongeza ya per diem kwa kuzingatia kuwa gharama za maisha zimepanda, ikiwamo hoteli ambazo wengi huishi wakiwa katika shughuli za Bunge Dodoma, ingawa wengine wanazo nyumba zao binafsi.

  “Nadhani kama ni ongezeko la per diem sawa kwa sababu gharama za hoteli na masuala mengine zimepanda mno. Hata kama wakilipa Sh.300,000 si tatizo kwa hadhi ya mbunge ambaye huwa na nyaraka mbalimbali na kwa hiyo, ni lazima aishi sehemu ya uhakika.

  “Lakini kulipana posho ya kukaa kitako tu kufikia 200,000 ni ngumu sana kueleweka kwa wananchi wetu. Ni kuzidi kujichonganisha na wananchi,” alisema mbunge mmoja katika mazunguzo yake na gazeti hili.

  Uchunguzi wa Raia Mwema umebaini kuwa Rais Jakaya Kikwete kwa mara ya mwisho aliwahi kusaini waraka wa nyongeza ya posho kwa wabunge Oktoba, mwaka jana, kupitia waraka namba CAB111/338/01/83.

  Waraka huo unatambulika kama waraka wa Rais kuhusu masharti ya mbunge. Hata wakati mjadala wa kususia au kutosusia posho za wabunge ulipoibuka bungeni, hususan Bunge la bajeti mwaka huu, utetezi ambao hata hivyo ni dhaifu, ulieleza kwamba, kuchukua posho ni sehemu ya masharti ya mbunge.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,375
  Likes Received: 19,635
  Trophy Points: 280
  anapima upepo huyu ..anavyopenda kusaini saini huyu ...
   
 3. YEYE

  YEYE JF-Expert Member

  #3
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Af hawa watu mbona wanataka kutufanya Watanganyika hatuna akili?! Mbona Spika amesema zimeshaanza kulipwa toka tar 8/11?!
   
 4. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  I do not trust my president any more.
   
 5. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #5
  Dec 8, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,155
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Hii sio kweli tena nakataa kabisa, kwa hii miongozi yetu ya kiafrika mibingwa ya kuanguka na kalamu(kusaini) na ndio maana sometimes yanabeba mafaili kwenda kusaini nje ya nchi. AMAUTI
   
 6. D

  Dopas JF-Expert Member

  #6
  Dec 8, 2011
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Labda Kikwete kakosa muda wa kusaini. Anavyosainigi haraka haraka, tena kwa mbwembwe bila hata kufahamu kilichomo! Kama ni kweli alidhamiria kutosaini kwaajili ya hali ya Nchi, na kwamba hawastahili kuongezewa kiasi hicho, aseme wazi. Watanzania tuna haki ya kufahamu msimamo wake katika suala hilo. Bi kiroboto hajui azungumzalo, tumsamehe bure, kwani hata uspika kazawadiwa.

  Yaani wanafunzi wa Vyuo Vikuu wananyimwa kuongezewa 2500, walau ili ifike 10,000/- yeye anasema maisha Dodoma ni magumu, UDOM ipo Arusha? St. Johns?, Mipango, Madini? Na vyuo vingine vilivyoomba kuongezewa walau kiasi hicho ili waweze kula kwa siku?
  Yaani basi tu Nchi ikishaingia ulajiulaji unaohalalishwa na wapumbavu fulani basi tu.

  Nasema tena JK labda hajausaini kwa kukosa nafasi, kama sivyo aseme, kinyume chake hakuna haja ya kuanza kumpongeza. Maana tunafahamu kuwa yeye ni kinara wa kusaini mambo haraka haraka kishabiki bila hata kuchunguza.
   
 7. Mtu Mzima

  Mtu Mzima JF-Expert Member

  #7
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Blah Blah za kuuza gazeti...
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Dec 8, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Si atie sahihi tu yaishe!?
   
 9. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #9
  Dec 8, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  The problem with this country is that every leader believes, under the conviction based on previous experience, that you can cheat all the people all the time. When rumours surfaced about sitting allowance increase, the parliament secretary came out and categorically invalidated them. In no time Madam speaker held news conference to clarify on the issue where she acknowledged the changes only controverting the claimed 300,000 sum as it has been published by the media.

  The series just rolls on and it is now JK turn to exhibit his theatric talents knowing that Tanzanians have already learnt to live with this kind of drama.
   
 10. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #10
  Dec 8, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,875
  Trophy Points: 280
  Anasubiri kwanza asikie kuna wabunge fulani wanataka kuonana naye Ikulu kutoa maoni kuhusu posho, halafu baadaye NEC ya CCM itoe ruhusa kwa makundi mengine kumuona pia, halafu litokee kundi lingine kumtembelea Ikulu kupeleka maoni yake, halafu ndio atie saini na kusema mjadala wa posho unaruhusiwa kuendelea hata baada ya saini yake!
   
 11. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #11
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  have you ever trusted him before????
   
 12. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #12
  Dec 8, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  It doesn't matter.....In Tanzania.. everything is possible.. hata kama posho ingepandishwa to 70,000 hadi 1,000,000 kwa siku.. Watu watapiga kelele, wataandika kwenye magazeti, wataandika kwenye blog & JF, lakini at the end, watarudi kwenye umasikini, kulala kwenye giza, kukosa maji, kukosa madawa, kukosa chakula na mwisho watu watatoa tabasamu pevu kwa wale wanao-wadhulumu.. ..Ni moja ya maajabu 7 ya dunia! Where is our line in a Guinness World Records book?
   
 13. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #13
  Dec 8, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Time for commercial break

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mhe Rais Kikwete,

  Japo natamani sana nikupe hongera KATIKA HILI la kuamka japo kwa kuchelewa na kuanza kulinda maslahi ya umma (sisi walipakodi badala ya ulinzi wa maslahi ya CCM) kwa kudaiwa kugomea kuidhinisha posho hizi kwa wabunge wasiotuletea tija yoyote hadi leo hii lakini mwenzio nasita sana.

  Ndio, Rais wangu nasema moyo unnisita kukupongeza juu ya hili tena naogopa sana kufanya hivo maana sielewi ni dakika ya ngapi mara baada ya kukupongeza juu ya hilo hata utakaponigeuka na kurudi kinyumenyume kwenda kutilia sahihi yako ya kubariki zoezi hili chukizo bila kujali tulivyo sakafuni kabisa hivi sasa kwa ugumu wa maisha ile mbaya!!!

  Hivi utakua umewahi kurudi nyuma kidogo hata ukajiuliza kwamba pindi unaopoonekana kujikita zaidi juu ya ULINZI WA MASLAHI BINAFSI YA CCM KWA GHARAMA YA KODI ZETU HATA TUSIO WANACHAMA HUKU UKITELEKEZA MASLAHI YA UMMA NZIMA wa nchi hii mwenzetu umewahi hata kuhisi uhalali wa aina ya ukichaa ambao huwa unatupanda vichwani kwa maonevu ya aina hiyo Baba?

  Huku unapoendelea kutaafakari juu ya hilo, hebu mie niacheni kwanza nikajivutie pumsi kwanza kuangalia upepo wa ustaarabu mzima hapa.
   
 15. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #15
  Dec 8, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ni kweli jamaa lazima atasaini tu, tatizo hata washauli wake ni vilaza.
   
 16. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #16
  Dec 8, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ukitazama kauli Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashililah,Spika Anne Makinda na JK unaweza kupata picha kamili jinsi serikali ya CCM inavyo fanya kazi.
   
 17. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #17
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,934
  Trophy Points: 280
  Anataka kuwapiga bao jingine la kisigino, JK kweli msanii sijawahi ona!

  Inaonekana amejipanga kuchukuwa credits everywhere, mhn!

  Mtu ambaye bado sijui atamchezea mchezo gani kwenye huu mtiririko wake wa kujiweka upande wa wananchi na dalili za kutaka kujisafisha, ni EL,huyo naona anamvutia pumzi dakika za mwisho.

  Tatizo kubwa alilonalo kati yake na EL ni conflict of interests ambazo mmojawapo kuzifanikisha za kwake ni lazima za mwenzake ziwe unrealised.
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Dec 8, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,610
  Likes Received: 82,192
  Trophy Points: 280
  Rais kasusa Mkuu!!!! Hatukuwahi kumsikia Mwalimu hata siku moja anafanya usanii kama huu eti wa kususa!!!! Sasa Rais unasusa unamsusia nani!!!? Nchi yetu kweli imepata kiongozi!!!!
   
 19. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #19
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,934
  Trophy Points: 280
  Anataka kuchukua credit kutoka kwa wananchi kuwa anajali matumizi.
   
 20. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #20
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  >> Katibu Wa Bunge (Hakuna Ongezeko La Posho)

  >> Spika Wa Bunge (ongezeko La Posho Liko Tokea 8/11)

  >> Rais (Agoma Kusaini Waraka.)

  Nimuamini nani kati ya hawa? Nitegemee nini kutoka kwa hawa? Na Je ni kipi kinafuat?
   
Loading...