Kikwete afichua anamiliki ng’ombe bora 400 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete afichua anamiliki ng’ombe bora 400

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Sep 27, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Na Mgaya Kingoba,[/FONT]
  [FONT=&quot]Ngorongoro[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Mgombea urais wa tiketi ya CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameonesha mfano katika kuhimiza ufugaji wa kisasa na usio wa kuhamahama kufuata malisho, akimiliki ng’ombe 400 ambao malisho yake yanalimwa katika shamba lake.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Amewaambia wafugaji nchini kwamba kama hawajui ng’ombe wao watakula nini, ni bora wasifuge.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Alitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti mjini Rujewa wilayani Mbarali mkoani Mbeya wiki hii na juzi alikuwa Loliondo wilayani hapa, kote akiomba kura kwa wananchi.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Rais Kikwete alieleza hayo wakati akifafanua kuhusu ilani ya Uchaguzi ya CCM, inavyoelekeza juu ya ufugaji wa kisasa na hasa kuhakikiksha wafugaji hawaendelei kuhamahama kwa nia ya kusaka malisho.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]”Mimi pia nafuga, nina ng’ombe si haba. Sasa nimelima majani, nina ng’ombe 400 na ekari 600, na nimechimba kisima napata maji pale,” alieleza Rais Kikwete bila kufafanua lilipo shamba lake.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]“Katika kiangazi kikali cha mwaka, hakuna ng’ombe wangu hata mmoja aliyekufa. Sina ugomvi na jirani yangu. Ni kitu kinachowezekana tunaposema ufike wakati wafugaji wasihemeane na wawe na malisho ya mifugo yao.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Alisema kama mfugaji hajui ng’ombe wake watakula nini, ni bora asifuge kwa sababu kwa mwenendo wa sasa, ufugaji wa kuhamahama hauna muda mrefu……[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Chanzo: HABARILEO Jumapili.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mtaji wa CCM ni ujinga wa watanzania - Baregu

  [​IMG]
   
 3. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mchungaji,

  Hii ndiyo inyowapa kiburi CCM. Maana wanajua hata tufanye nini tunaowaongoza hawana cha kufanya. Ona sasa hii hali! Hao ni watoto na si ajabu hayo maji ni ya kunywa na kupikia!!!

  Kweli unaweza kusimama na kuipigia vigelegele CCM kwa shangwe ya mazuri!! Kweli...

  Wakati wao umefika...
   
 4. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hapa mbona panafanana sana na sehemu moja huko Bumbuli - Lushoto. Wanafulia humohumo na kuchota maji kwa ajili ya kupikia na kunywa. Hayo ndo maendeleo CCM imewaletea wananchi.
   
 5. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Duu kumbe Jk ni bonge la fisadi, yaani hekari 600, zote peke yake? hivi kila mtanzania akitaka pata hekali japo 100 kwa nchi yetu Tanzania yenye wakazi takribani milioni 40 tutatosha??

  JK acha dharau zako, we unategemea kila mfugaji akitaka kulima majani ya mifugo yake kwa hekari 600 hiyo ardhi itatoka wapi? ama kweli mwenye shibe hamjui mwenye njaa!
   
 6. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mkuu upo sahihi kabisa..........Pia on the way to Handeni, you can see this just besides the road. Inasikitisha sana.
   
 7. J

  JohnShao Member

  #7
  Sep 27, 2010
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kisa ufagaji wetu siyo wa kisasa na kilimo chetu siyo cha kisasa kiko kwenye mfumo wa kumiliki ardhi na siyo ujinga au kukosa elimu kwa wafugaji na wakulima. Kufanya ardhi mali ya serikali kunawaneemesha tu watendaji wa serikali na kuwadhulumu wazalishaji hasa wakulima na wafugaji. Kikwete anasema ana ngombe 400 lakini pia ana shamba la eka 600. Hivi viwili ni muhimu vinaenda pamoja. Huwezi kuwa na ngombe 400 na shamba la eka 2.

  Utaratibu wa huko nyuma wa kuwanyang'anya wakulima Waafrika wenye mashamba ya eka 50, 100 hata 200, kuwanyanganya mashamba yao na kuwaachia eka 6 tu umechangia sana kulemaza siyo maendeleo ya kilimo na ufugaji wa kisasa tu bali pia fikra za viongozi na wasomi wengi kuhusu ni nini cha kufanya ili kilimo chetu kiwe cha kisasa na ufugaji wetu uwe wa kisasa.  Ukitaka ufugaji wa kisasa au kilimo cha kisasa sharti mfumo wa kumiliki ardhi uwe wa kisasa na yule mkulima au mfugaji aliye mstari wa mbele aungwe mkono na ashangiliwe. Hili la kutenganisha ufugaji wa kisasa au kilimo cha kisasa na mfumo wa kumiliki ardhi ni kosa kubwa na in fact wizara ya ardhi inatakiwa iwe idara chini ya wizara ya kilimo kwani kilimo na ufugaji ndio watumiaji wakubwa wa ardhi na ndiyo wanaoathirika vibaya kama sera ya kumiliki ardhi ni mbovu.

  Nchi imebinafsisha kila kitu, hata serikali yenyewe, lakini hawataki kuibinafsisha ardhi kwa mkulima mwenyewe na mfugaji mwenyewe. Hii licha ya kujulikana wazi kuwa katika nchi zote zenye mafanikio makubwa katika kilimo na ufugaji, ardhi au ni mali ya mzalishaji kabisa, yaani freehold, au mzalishaji ana lease ya muda mrefu, miaka 99 hadi 999. Uhakika wa kwamba ardhi ni mali yako na siyo serikali wala mtu mwingine anaweza kukunyanganya ni nguzo muhimu inayomfanya mkulima awekeze kwenye kilimo cha kisasa au mfugaji kwenye ufugaji wa kisasa.

  Sera hii mpya ya kumiliki ardhi ilipendekezwa miaka michache kabla ya uhuru kwa Kenya na Tanzania lakini kwa bahati mbaya Tanzania iliikataa na Kenya ikaikubali. Tofauti hii, licha ya zigizaga zake tangu miaka hiyo, ni moja ya misingi mikuu ya tofauti ya mafanikio kati ya Kenya na Tanzania hadi leo.

  Hongera JK kwa kuwa na ngombe wa kisasa 400 na shamba la eka 600. Tunahitaji vikwazo vinavyowakwamisha wakulima na wafugaji wengi kuweza nao wakawa na ngombe wa kisasa 400 na zaidi na shamba la eka 600 na zaidi - siyo Marais wastaafu tu na upendeleo kwa wawekezaji au wa nje au wa ndani lakini wenye asili ya uarabu, uhindi au uzungu tu. Vikwazo vinavyowakwamisha wakulima na wafugaji Waafrika wa tangu asilia kuwa wakulima na wafugaji wa kisasa ndivyo vinavyotakiwa viondolewe na kikwazo cha msingi kabisa ni kile cha kumpora mkulima au mfugaji ardhi yake kisha kumwambia aboreshe kilimo au ufugaji.
   
 8. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,394
  Trophy Points: 280
  DUU NDANI YA MIAKA 5 KAJENGA HEKALU MIGOMBANI PALE MOROKO REGENT,MSOGA HEKALU NA NGOMBE 400 HEKA 600.je ndani ya miaka 10 Atakuwa tajiri wa namna gani?siasa inalipa jamani kwa afrika.
   
 9. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Ng'ombe wa Kikwete wana maisha bora lakini hawalipi kodi, watanzania wanaolipa kodi hawajui hata watakula nini mwisho wa siku. Kodi zetu watanzania zinawanenepesha ng'ombe wa Kikwete huku watoto wetu wakikaa chini sakafuni kwa kukosa madawati ! Raisi na kiongozi mkuu wa CCM eti hana hata aibu anapotamba kwa hilo, aibu iliyoje Watanzania !
   
 10. Madago

  Madago Senior Member

  #10
  Sep 27, 2010
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa mtaji huu, hii sera ya kuwapa ardhi wawekezaji wa nje kwa ajili ya "biofuels" si itakinzana sana na hoja ya watanzania kufanikishwa na kuwa wafugaji bora? hizi ardhi watakzopewa watu wa nje kwa ajili ya majatropha kwanini wafugaji wanaohangaika wasipewe na kuwezeshwa kama mkuu wa nchi anavyojiwezesha ngombe zake?
   
 11. E

  Estmeed Reader Senior Member

  #11
  Sep 27, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 12. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2010
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kikwete mtu mmoja hekari 600 za kuchungia ng'ombe wake wakati Wamasai wanahangaika na ngombe wao hawana sehemu za kulishia, wamenyang'anywa na Kikwete, na serikali yake.
   
 13. T

  Thin Line New Member

  #13
  Sep 27, 2010
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhshmw unaongea na 'farmers','pastoralists','peasants' au 'civil workers' kama wewe? Hebu share nao mbinu ulizotumia kupata mtaji wa shughuli hiyo na imekuchukua muda kiasi gani kufikia hapo! Hiyo italeta picha kamili kwa WAPGA KURA WAKO!
   
 14. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #14
  Sep 27, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Mwenye nacho kumsanifu/kumkebehi asiye nacho!
   
 15. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #15
  Sep 27, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Sickened! for good!!
   
 16. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #16
  Sep 27, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280
  JK anashindana na Museveni kwa ufugaji ...alishawahi kuelezea namna alivyofurahishwa na NGOMBE aina ya ANKOLE kule kwenye ranchi ya Museveni ya RAKITURA.............infact JK na Lowasa wamekuwa wakifanya biashara ya kuuza ngombe COMORO kwa muda mrefu sasa..tangu wakiwa mawaziri...

  SIPINGI RAIS KUWA mfugaji bora.....kwani si vibaya akiwa na shamba la namna hiyo la mfano kwa wengine....ila asijilinganishe yeye na wafugaji wengine hata wale wakubwa.....YEYE MASHAMBA YAKE YANAHUDUMIWA NA SERIKALI...HIVYO AKIBWETEKA NI VIGUMU KUJUWA FAIDA AU HASARA HALISI.....

  TUSEME KAMA FAMILIA YAKE INAVYOHUDUMIWA NA KUFUJA MALI..BASI HATA NGOMBE NA MBUZI WAKE BASI NI MIFUGO YA KWANZA NCHINI ...INABAHATIKA KUHUDUMIWA NA SERIKALI ....SI KAMA NGOMBE WANGU MIMI....
   
 17. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #17
  Sep 27, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Badala ya wafugaji kupewa somo ni jinsi gani wafuge mifigo kwa maendeleo yao,, jk anawatishia sasa inasaidia nini???
  Tukumbuke kuwa hawa wafugaji hawajaenda shule, hawana muda wa kusikiliza vipindi vya redio vyenye mafundisho wala hawana muda wa kutulia pamoja embu tujiulize yeye ng'ombe 400 ekari 600 je mwenye 3500 atatumia ekari ngapi na hizo ekari ziko wapi????

  Hatumchagui ili aende akaendelee kuuza sura huko marekani, serengeti na bagamoyo kwake..
   
 18. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #18
  Sep 28, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,611
  Likes Received: 4,710
  Trophy Points: 280
  Hivi na misukule anayo mingapi? Maana kawafanya CCM wote misule yake, hata akiharibu wao wanamshangilia tu, kweli JK kiboko. OLE WAKO JK na MNAJIMU WAKO, saa ya kuwaadhibu imefika
   
 19. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,319
  Likes Received: 22,162
  Trophy Points: 280
  Kudadadadeki.
  Mifugo yote kwangu, ardhi kwangu, ma beema ya ikulu yote kwangu, mabenzi pia yote mimi.
  Mashangingi kwangu, majumba yote mimi.
  Thats y milafi ya ccm haitaki kuachia nchi
   
 20. S

  SuperNgekewa Member

  #20
  Sep 29, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baregu asisahau kwamba wa kwanza wa kulaumiwa kwa ujinga wa Watanzania ni maprofesa wenyewe kwani maprofesa ndio wanaofundisha walimu wanaokwenda kuwafundisha wanafunzi ambao ndio Watanzania wenyewe. Kama Watanzania wana fikra potofu ina maana kuwa waliowafundisha wana fikra potofu; na kama walimu wao wana fikra potofu basi chanzo hasa ni kwamba maprofesa wanawapa wakufunzi fikra potofu.

  Ni vizuri kwamba Profesa Baregu anatambua kuwa taifa limegubikwa na ujinga uliokubuhu, lakini ni vizuri pia kama akienda hatua ya pili na kutambua kuwa wasababishi wakuu wa ujinga huu ni maprofesa wenzake. Kwa hiyo ili kuondoa ujinga huu wa taifa inabidi maprofesa waanze kukosoana wenyewe kwa wenyewe, siyo kuendelea kuoneana aibu na kulindana kama wanavyofanya viongozi wa serikali. Wakosoane wenyewe kwa wenyewe kwani sisi huku uraiani tunaogopa watakapojibu mashambulizi kwa kusema: ibid., op. cit.; et al., na kadhalika.
   
Loading...