Zee la shamba
Member
- Oct 17, 2007
- 55
- 3
::>Amporomosha mkurugenzi mzito
::>Amrejesha jeshini, hofu yatawala
na mwandishi wetu
FAGIO la Rais Jakaya Kikwete, limefanya kazi tena katika muda usiozidi saa 24.
Zamu hii ameamua kumngoa Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Technolojia (COSTECH), Profesa Yadon Kohi.
Profesa Kohi ambaye ni Brigedia Jenerali wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), jana alitaarifiwa rasmi kuwa, uteuzi wake umetenguliwa, na anapaswa kurejea jeshini.
Hatua hii ya Rais iliilazimu Bodi ya Wakurugenzi kukaa kwa dharura Dar es Salaam jana, na kumteua Dk. Rose Kingamkono, kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH. Dk. Rose alikuwa Mkurugenzi wa Utafiti kabla ya uteuzi huo.
Habari za nafasi ya Profesa Kohi kutenguliwa, zilianza kusambaa juzi jioni, lakini hakukuwapo chombo chochote huru cha kuzithibitisha, hadi jana, ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya COSTECH, Profesa Burton Mwamila, alipotoa taarifa kwa vyombo vya habari.
Taarifa hiyo fupi iliyokuwa na misitari mitano, ikiwa imeandikwa kwa Kiingereza, ilisomeka: Tunapenda kuifahamisha jamii kuwa Dk. Rose Rita Kingamkono, ameteuliwa na Bodi ya COSTECH kama Kaimu Mkurugenzi kuanzia Desemba 7, 2007.
Hii inatokana na uamuzi wa Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kwamba Profesa Brigedia Jenerali Yodan Mtalima Kohi, arudi katika Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Juzi Rais Kikwete alipangua safu ya wakurugenzi katika Wizara ya Maliasili na Utalii, na kuteua wapya kushika nyadhifa hizo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, alisema, mabadiliko hayo yalilenga kuleta ufanisi.
Lengo la mabadiliko haya ni kuleta ufanisi katika utendaji wa idara zilizo chini ya wizara. Tulichelewa kufanya mabadiliko, kwa sababu umakini wa hali ya juu ulihitajika, alisema Profesa Maghembe.
Katika mabadiliko hayo, Erasmus Tarimo, ambaye awali alikuwa Ofisa Wanyamapori Mkuu, aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, kuchukua nafasi ya Emmanuel Severre, ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Severre, aliyekuwa akituhumiwa kwa kashfa nyingi, na akidaiwa kutamba kuwa yeye ni kisiki cha mpingo kwa hali yoyote asingeondolewa katika wizara hiyo.Mwaka jana, Waziri wa Mifugo, Anthony Diallo, alipoteuliwa kushika Wizara ya Maliasili na Utalii, Severre alikaririwa akitamba kuwa juhudi za kumngoa alizokuwa ameanzisha Diallo zisingefua dafu. Na kweli Diallo alingolewa na kumuacha Severre.
Kwa pande wa Profesa Kohi, kwa muda wa miaka 14 aliyoingoza COSTECH tangu mwaka 1993, ameelezwa kuwa ameshindwa kuifanya tume hiyo kutimiza malengo yake.
Inadaiwa kuwa alikuwa na safari nyingi za nje, huku uongozi wa tume hiyo uliokuwa chini yake, ukiwa unaingia mikataba na kampuni za simu kuvuna fedha kwa bei nafuu, hali iliyosababisha majengo ya COSTECH kupigwa rangi za kampuni moja ya simu. Baadaye rangi hizo zilifutwa.
Pia zipo tuhuma kuwa, magari ya COSTECH yalikuwa yakitumiwa na uongozi wa juu chini ya uongozi wa Profesa Kohi kwenda kuwindia wanyama pori, hali iliyomkera Rais Kikwete.
Sayansi imedumaa nchini. Chini ya uongozi wake imekuwa ni semina, mikutano, safari, basi hakuna utafiti unaofanywa, hatafuti fedha kwa ajili ya tume, kila kitu kinakwenda tu, kilisema chanzo chetu.Mabadiliko yanayotokea sasa, yanadhihirisha kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa hivi karibuni katika Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM, mjini Dodoma, aliposema atahakikisha anasafisha uoza serikalini.Kwa kuonyesha kuwa amedhamiria kutenda anenayo, hivi karibuni ameunda kamati mbili za kuchunguza masuala mazito, likiwamo la kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond, na ile ya kuchunguza na kupitia sera na mikataba ya madini.
Matukio hayo mawili, yametengeneza hofu kubwa na kusababisha kihoro kutawala miongoni mwa watendaji wa Serikali. Hii ilithibitika wakati mkurugeni mmoja alipopigiwa simu kutoa maoni yake jana: Sina la kuzungumza. We niache tu, huwezi kujua labda kesho ni mimi. Ngoja tuone kwanza mzunguko unakwendaje.
Source: Mtanzania newspaper