Kikwete aendelea kumshambulia Magufuli

Wakti wa uzinduzi ujenzi wa Barabara ya New Bagamoyo JK aliendelea kuishutumu Wizara ya Ujenzi kwa kusema hadharani kwamba:- Wananchi kujenga kwenye Hifadhi ya Barabara ni Uzembe wa Wizara na Tanroads.

Jamani kuna Mantiki hapo kuishutumu Wizara na Tanroads?

Vipi habari ya kuchakachua noti mpya mbona hatujaskia kauli kali kama hiyo kwa wizara husika?

Jamani tubadilishane mawazo!!!

Mkulo ni Muislam mwenzake ndio maana anamlinda

Mbona alipokuwepo Waziri Kawambwa hajawahi kukemea Tanroad na Wizara na madudu yalikuwepo

Kwasababu ni Muislam mwenzake na wanatoka ukanda mmoja.
 
We dubo unahuakika huyu ni Dr Slaa mwenyewe kaandika hapo au ni jina la kutumia humu la mtu?
 
I salute you Nguruvi3 for understanding what I intended to SAY/deliver!!
A good Leader stand for what he says. The way Kikwete reacted on that inaugaration contradicted with previous comment by himself!!! thats where my problem is!!!

Kinachogomba hapa si yeye kusema au kutoa kauli. Tatizo ni kuwa kauli anazotoa zinafanya mtu mwenye akili timamu ashindwe kuelewa anasimamia nini na kwanini.
Alipomdhalilisha Magufuli ambaye ndiye waziri husika kuwa anavunja nyumba za wanyonge na aache alikuwa anatafuta 'popularity' kwa kuonyesha 'sympathy' kwa wanyonge. Sasa anapoambiwa gharama za ujenzi zinachangiwa na malipo yatokananyo na kubomoa nyumba za wavamiaji anasema wizara na idara zake hazifanyi kazi. Huyu ndiye JK.

Fikiria, yeye kama mwenyekiti wa kamti kuu (CC) aliwahi kusema kamati kuu inaafiki kulipa Dowans. Alipokuwa na wabunge ubungo plaza akasema wameamua wasilipe na hata yeye haimpendezi. Ni JK.
 
Akikaa kimya mnadai kuna vacuum ya uongozi, akikemea eti anawaumbua mawaziri wake!
Acheni uchokozi!

Rais hawezi kuongoza kwa kulalamika jukwaani. Rais si mtu ambaye hana mamlaka ya kiutendaji. Sasa analalamika kwenye hotuba katuambia kachukua hatua gani kumaliza hii kero? Kamuwajibisha mtu? Mimi sanasana naona anaharibu morale kwa kutofata kanuni za "collective responsibility". Ukikubali kufanya kazi na mtu, huwezi kumkosoa hadharani, ukiona hafai muwajibishe. Haya mambo ya kukosoana kwenye hotuba ni umbeya tu, hayana tija.

Ni kawaida sasa kwa Kikwete kulalamika kama vile na yeye ni raia asiye na mamlaka, wakati ana mamlaka yote mpaka nyota ya begani ya kuwakilisha dola kashachukua, sasa analia lia nini? Na hayo anayokemea majukwaani kashawaambia hao watendaji wake kwenye vikao vya ndani?

Kikwete ni ndumilakuwili anayetaka kuonekana mzuri kwa kila mtu, na ni mwoga anayeogopa kuwajibisha watu. Na kashawajua watanzania wengi hawana muda wa kuangalia mambo kwa undani hivyo akiwapa mchezo wa kuigiza majukwaani tu bila mkakati madhubuti, basi watasema "rais mkali kweli kweli" na kumpa pointi, halafu kesho keshokutwa mambo yakienda mrama tunampa udhuru, eti rais anafanya kazi vizuri lakini anaangushwa na watendaji wake.

Kama anaangushwa na watendaji wake, na yeye hajui au hajali basi tatizo ni yeye.
 
Back
Top Bottom