Kikwete Acheni Masihara......

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,947
709
Ni jambo linalotia kichefuchefu kuona muswada uliopelekwa kwenye semina ya Bunge lililopita unataka kupelekwa kwenye Bunge lijalo. Cha kushangaza zaidi ni pale muswada huo unakuwa na saini ya FISADI aliyeachia ngazi. Kitu nachojiuliza ni kuwa baada ya huo muswada kukataliwa na wabunge, wahusika akiwa Waziri, Naibu waziri na wengineo waliahidi kufanya marekebisho. Anyway, huyu Mh. Ngeleja alipopata promotion toka naibu hadi full waziri aliahidi kuwa atafanya mabadiliko mapema iwezekanavyo kuhusu hilo pamoja na mapendekezo ya Kamati ya Mwakyembe. Sasa ndiyo nini kupeleka muswada ule ule ambao haukuwa na cha ziada kipya huku ukiwa umehitimishwa na sahihi ya Fisadi KARA-MAVI. Jamani hivi ni lini hii serikali ya Kikwete itakuwa serious???????????? Yaani hata Waziri hakuupitia tena hata danganyia angeweza kubadili signature. Walishazoea Majority ya wabunge ambao ni SISIEMU wenyewe kutegesha tu mkono na kulamba bahasha zao za posho bila kuangalia au kusoma kwa makini vitu kama hivyo.
Mie nafikiri waziri Ngelega ulitakiwa uachie ngazi maana siamini kama unajua unachokifanya hapo wizarani. Itakuwaje upeleke muswada kwa wabunge ukijua kuwa hauna idhini yako?????? Kama hukutia saini ina maana hukuidhinisha document ya serikali kwenda nje. Hakuna hata aliyesaini on behalf, kwa msingi huo inamaanisha hukuusoma kabisa na kama uliusoma basi hukufanyia marakebisho kulingana na mapungufu yaliyokuwemo. Sasa kama hukupitia muswada itakuwaje sembuse Mkataba???????? Yaani tayari ulishaonyesha mapungufu na hufai kabisa. Au JK atueleze kama NAZIR-A KURAMAVI alijiuzuru kigeresha na bado anafanya kazi za serikali, inawezekana labda tunafichwa.

Sasa huku tunaambiwa kuwa kunaweza kukawepo mgao wa umeme. Na tuna waziri ambaye aliahidi kuwa atafanya mabadiliko mapema kuhusu suala la umeme. Sasa hayo mabadiliko ni yapi au ndo ya kuacha signature ya Fisadi kwenye muswada. Itakuwa ni AIBU na KICHESHO cha KARNE Tanzania kuanza ku-experience tena mgao wakati kuna makampuni hapa yanalamba pesa zetu kwa wingi tu kwa ajili ya uzalishaji. JK tafadhali acheni masihara kabisa, haiwezekani watu wakaanza ku-face mgao watu wengine bado wamekalia pesa za wananchi mojawapo akiwa rafikiyo. Jamani hizi ni mali ya watanzania halafu leo unadiriki kusema kutakuwepo na mgao. Ben Mkapa hujamuuliza kuhusu Songas halafu mnasema TANESCO kununua hisa Songas. Jamani jamani, rudisha kwanza Songas kwa wananchi kwanza halafu mambo mengine ndo yataanza kujadiliwa. Ben na Yona walituibia hii Songas halafu JK umepata madaraka hutaki kuhoji jinsi walivyo acquire hiyo Songas...
Nasema tena ACHENI MASIHARA, kuweni serious na kazi za watu jamani, ndo wamewaweka hapa. Hainingii hata kwa sekunde watu wa-face mgao huku DOWANS ikiendelea kulamba pesa zetu, Ben na Yona wao wakizidi kuneemeka na Songas yetu. Pls JK do something about that........
 
Kila siku napata jambo jipya hapa JF, nilikuwa sijui kama Songas nayo ni ya BEN&YONA.

Mr.President when are you coming back?.....We real miss you!
 
ndo wamewaweka hapa. Hainingii hata kwa sekunde watu wa-face mgao huku DOWANS ikiendelea kulamba pesa zetu, Ben na Yona wao wakizidi kuneemeka na Songas yetu. Pls JK do something about that........

Kamanda font uliyotumia sio mwake kabisa!
 
Serikali ya mseto au pure inahitajika hata hapa Tanganyika na sio Zanzibar pekee,Mh.Kikwete lazima aunde serikali ya Mseto kuikoa Tanganyika la si hivyo uzito unazidi kuielemea Nchi hii yenye utajiri nambari mbili duniani na ambayo ni masikini nambari 23.
 

Mr.President when are you coming back?.....We real miss you!

Yuko Busy na mambo ya AU, sasa hivi ana shughulikia mambo ya Comoro baadaye Zimbabwe, vuteni subira watanzania JK ni raisi pia wa Africa yote..
 
JK naye ni mwana system jamani
Tunaelekea ya Zimbabwe sasa, watu wanahoji kwanini raia wa Zimbabwe hawaonyeshi dalili zozote za kumkataa
Mugabe!!!
Nauliza tena je sisi tumekubaliana na hali halisi ya viongozi wetu, tukianza na kikwete, kwanini kama sisi ndo tulimweka madarakani, je hatuna nguvu ya kumwajibisha jamani?? Maana kubali kataa mambo yanakuwa mabaya kila kukicha na jamaa kakaa kimya tu, anakula raha.

BabaH hata Wazimbabwe sasa wanaanza kuamka, angalia figures kutoka The Economist la wiki hii, sisi sijui tutaamka lini

The latest opinion poll by the Mass Public Opinion Institute, run by a professor at the University of Zimbabwe, gives Mr Tsvangirai 28% of the vote, Mr Mugabe 20% and Mr Makoni 9%. Another 24% refuse to reveal a preference, suggesting still wider support for the opposition, and 8% are undecided. Such figures should be treated cautiously, but it seems more than possible that Mr Mugabe will fail to win the 50%-plus needed to clinch victory in the first round, even if he rigs as ruthlessly as he has done before. A run-off would have to be held within three weeks.
 
Yuko Busy na mambo ya AU, sasa hivi ana shughulikia mambo ya Comoro baadaye Zimbabwe, vuteni subira watanzania JK ni raisi pia wa Africa yote..

Kweli Mkuu huyu jamaa inaonekana hakujiandaa kabisa kuwa kiongozi wa watanzania. Ila ule uwaziri wa mambo ya nchi za nje alikuwa anauweza sana na ndio maana unaona pamoja na matatizo yaliyoko nchini, yeye anaweza sana mambo ya AU, Kenya, Zimbabwe, Commoro na kualika akina Bush basi.

Ukimwambia Sijui EPA, Richmonduli, Dowans anaona siyo kazi yake. Washauri wake wamwambie haya ndiyo mabomu aliyokalia siyo Comoro, nk.
 
Kikwete ajue kuwa voice of people is the vice of God!
It seems as if he never get any irritation from all the rubbishes done to the country.
 
BabaH hata Wazimbabwe sasa wanaanza kuamka, angalia figures kutoka The Economist la wiki hii, sisi sijui tutaamka lini


Mkuu pundit polls za zimbabwe ni ngumu kuziamini maana watu kule ni waoga kuliko hata enzi zile za chama kushika hatamu hapa TZ, lakini reality still inapotray watu wamechoka kabisa na mugabe na pia ZANU PF lakini are they ready for change??????????

Nadhani utakubaliana nami ktk hali kama ile change itakuja tu damu ikimwagika...........
 
Ama kweli wadanganyika .Yaani nyie ndiyo mnajua kwamba JK hakujiandaa kuwa Rais ? Mie nilijua tangia siku ya kwanza anatangaza nia ya kuwa rais .Hakuwahi kusema kwa nini anataka kuwa Rais ila alisema anataka kuendeleza yale yale ya Mkapa na Ilani ya CCM.Na ya Mkapa wote mnayajua sasa mnasemaje ?
 
Kila siku napata jambo jipya hapa JF, nilikuwa sijui kama Songas nayo ni ya BEN&YONA.

Mr.President when are you coming back?.....We real miss you!

Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu sasa CCM wanacheza watakavyo si wana kika kitu kuanzia jeshi na kila chombo cha usalama?
 
Back
Top Bottom