Kikwete acha kuvunja sheria za Nchi . | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete acha kuvunja sheria za Nchi .

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mpaka Kieleweke, Mar 5, 2009.

 1. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,135
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Jana wakati Rais Kikwete akiwa anazindua komandi ya kikosi cha ardhini cha jeshi letu JWTZ aliutangazia umma kuwa ameamua kuongeza muda wa kustaafu kwa wanajeshi eti kutoka miaka 57 hadi miaka 60.

  Sasa hawa ni watumishi wa Serikali na wapo chini ya sheria ya utumishi wa umma , sasa haya mamlaka ya kuongeza muda wa kustaafu ameyatoa wapi?

  Ametumia kigezo gani cha sheria ama ni sheria gani inampa mamlaka ya kuongeza muda wa kikundi fulani cha wafanyakazi kustaafu?

  Tunaelekea wapi na utamaduni huu wa kuvunja sheria za Nchi , na je?tukienda hivi tutaweza kufika?

  Namshauri Rais sasa awe anafuata sheria na kamwe asiwe wa kwanza kuvunja sheria , na yeye ajue kuwa kama alimwadhibu Mnnali kwa sababu ya kuwacharaza waalimu bakora na kusema huko ni kukiuka sheria anapaswa naye awajibishwe .

  Tujenge utamaduni wa kuheshimu sheria zetu, kwani Nchi bila sheria ni fujo.
   
 2. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,135
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Serikali imeongeza muda wa kustaafu kwa askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Rais Jakaya Kikwete alitoa taarifa hiyo jana katika uzinduzi wa Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu (LFC) Kibaha, mkoani Pwani.

  Kwa mujibu wa Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, utaratibu huo utaanza Julai mwaka huu. Alisema maofisa wa ngazi ya juu kuanzia Julai mwaka huu wataongezwa muda, kutokana na kuwa uzoefu unaonyesha kwamba maofisa hao walikuwa wakistaafu wakiwa bado vijana.

  "Uzoefu umeonyesha kwamba askari walikuwa wakistaafu wakiwa vijana na bado wana nguvu … kwa sasa tunaongeza umri wa kustaafu utakuwa ni miaka 60 na si 57 kama ilivyokuwa awali," alisema Kikwete na kuongeza kuwa mabadiliko hayo yatafanyika kwa ngazi zote.

  Kwa mujibu wa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi, awali maofisa kuanzia cheo cha Brigedia Jenerali hadi Jenerali, walistaafu wakiwa na umri wa miaka 57. Maofia wa vyeo vingine, walistaafu kulingana na vyeo vyao jeshini.

  Rais Kikwete alisema serikali itahakikisha bajeti ya Jeshi hilo inaongezwa ili kulifanya liwe la kisasa zaidi na kwamba litaendelea kujengeka na kuendelea kutimiza wajibu wake kitaifa na kimataifa. Alisema kuzinduliwa kwa Kamandi hiyo ya nchi kavu, kunalifanya JWTZ kuwa na kamandi tatu. Nyingine ni ya Ulinzi wa Anga (AFC) na Kamandi ya Wanamaji (Navy).

  Kulingana na taarifa ya Rais Kikwete, LFC itashughulika na suala zima la kutoa mafunzo kwa askari na kuhakikisha linaandaa wanajeshi kwa shughuli za kivita na ulinzi wa mipaka ya nchi. Alisema kuwa Jeshi linaendelea kutimiza wajibu wa kitaifa na kimataifa katika ulinzi. Alisema Serikali ya Chad imeiomba Tanzania kupeleka majeshi kwa ajili ya kulinda amani katika nchi hiyo yenye machafuko ya kisiasa. Hata hivyo, Dk Mwinyi aliliambia gazeti hili kwa simu kuwa uamuzi wa kupeleka majeshi, utafanyika baada ya majadiliano na pia kwa kuzingatia uwezo wa nchi.
   
 3. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2009
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,299
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Nina swali kidogo ndugu zangu tuseme Bwana shamba wa serikali ana miaka 55, na mwanajeshi ana 55, je mwanajeshi atakuwa bado kijana kuliko bwana shamba? nafikiri hii ni janja ya uchaguzi wa mwaka 2010
   
 4. H

  Huduma Member

  #4
  Mar 5, 2009
  Joined: Jan 26, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwakyembe. ITV. Excellent. 110%. Maana kama ni kleptocracy ya government halafu na wabunge tunaowategemea nao wakawa kwenye kundi la mijizi. Si tutakuwa tumekwisha. Angalau ipo harufu ya watu wenye kijiuchungu na walalahoi wa nchi hi.

  Hivi nyie serikali na hasa ikulu na hao waliokuwa zamani wafanyakazi wa Richmond waliopo hapo Ikulu mnadhani watu wote ni vipofu. Nyie ndio vipofu ndio maana mnashindwa kuona ishara za nyakati. Kama mlituibia huko nyuma waziwazi tena mchana kweupe sasa mkitaka kuiba ili mrudi kiulaini madarakani kwa kuhonga kanzu, kanga na hinabu na pilao lisilo na nyama sio miaka hii eti.

  Nilikwishasema mimi kuwa nchi hii bila kuongolewa kwa kupewa persona non-grata wazungu koko kadhaa, wahindi kadhaa na burushi mmoja toka tabora hakuna tutakachoweza kufanikisha -maana wanaojidai wanatusaidia ndio wamalizaji, wezi wakubwa.....wizi mtupu!

  Haya yote pengine yanatokea kwa sababu viongozi tunaowaheshimu kuwa wanatuongoza na wanaongoza nchi kumbe haki ya mama wao pia wanaongozwa na kuendesha na maburushi. wamasai na wasukuma wenye fedha, wandengereko wachache, wahindi, mabaniani na wazungu wanaogopeka kwa sababu ngozi zao nyeupe huku Zeruzeru wakidhalilishwa kwa sababu ya weupe huo huo! Maajabu ndani ya hijabu la siasa zisizo za wazi wala zisizo na tumbo la uchungu la mzazi wa taifa la kesho na kesho kutwa!

  Tuna maamuzi ya kufanya hapa. Ama tuamue kuendelea kuwaibia na kuwadanganya watu wetu kwa janja za kisiasa na manufaa ya wachache au tuache kuiba kwanza ili watu wapate angalau mahitaji ya msingi na nchi kuanza kuendelea. Maana nchi ikiwa katika mwendo hakuna atakayoona hivi vijisenti tuwili tutatu vikitgoka kwenda kujenga chama au kupigia kampeni za kuwasafishia au kuwafagilia wakubwa njia 2010.

  Viongozi wetu lazima wajiulize nao pia watakuwa wageni wa kudumu kwenye 3 x 6 au makaburi yao yatakuwa kama mapyramidi ya Mafirauni waliowatangulia wao?


  huduma
   
 5. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ninavyojua mimi ni kuwa watumishi wote wa umma wanatakiwa kustaafu wakiwa na miaka 60. Sasa kama Rais ameongeza umri wa kustaafu kwa wanajeshi, inaonyesha kuwa wao walikuwa wanatumia kanuni tofauti na inawezekana ni wao tu ndio waliokuwa wakistaafu wakiwa na umri mdogo kuliko wengine.

  Naamini Rais kwa mamlaka aliyonayo, ana uwezo wa kufanya uamuzi alioufanya.
   
 6. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Kwa bahati mbaya sijui kuhusu wanajeshi, lakini kwa upande wa watumishi wa umma, Rais kama rais hawezi kubadilisha mishahara na kutangaza kiholela.
  Lakini labda utaratibu ulifuatwa lakini ulifanyika kinyemela. :)
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,597
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Rais ametangaza tu... Taratibu zingine zilikuwa zimekwisha fanyika kwa mjibu wa waziri wa ulinzi. Na huyo Mpaka Kieleweke inaonekana ameamka nao
   
 8. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #8
  Mar 5, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,160
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mkuu Huduma,

  Sidhani kama nitakuwa nimekusoma vizuri .......huu mchango wako unahusiana vipi na ''Rais kuongeza umri wa kustaafu kwa wanajeshi'' angalia mkuu usije kuwa umeingia choo cha jinsia tofauti na yako!

  Cheers
   
 9. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,135
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Hapa naona kuwa wewe ndio umeamka nalo kwani wewe ndio huelewi kinachoendelea .

  Jua kuwa sheria ya utumishi wa umma ndio ambayo inatoa ukomo wa kustaafu kwa mujibu wa sheria .

  Kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma ni kuwa kima cha juu cha umri wa kustaafu ni miaka 55. sasa JK kaamua kutangaza kabla sheria haijabadilishwa ni kwanini?

  Alipaswa amtake waziri wake apeleke mswada bungeni ndipo upitishwe na Bunge ndio aseme .

  Kutangaza kabla ni kulidharau Bunge , na kuamini kuwa litakubaliana naye kwa lazima .

  Bunge linapaswa kiuheshimiwa, ni lazima Bunge lichukue nafasi yake wakati huu na mhimili wa utawala lazima uheshimu muhimili huu muhimu wa Bunge.
   
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,625
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Nadhani hapa ndio umeeleweka ulikusudia kusema nini! yaani maelezo yako meeeengi MK na hasa kusudi lilikuwa hili?
  Hapa nimekupata na hata mimi nashangaa labda kama kuna sheria nyingine ambazo rais ana ruhusa kutunga bila kushirikisha bunge. Wanasheria tuelezeni
   
 11. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu Mpaka Kieleweke, naomba kukusahihisha. Sheria ya umri wa kustaafu ilibadilishwa na kuwa miaka 60 muda mrefu tu.
   
 12. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #12
  Mar 5, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 9,222
  Likes Received: 4,112
  Trophy Points: 280
  Jamani sio rais huwa anatangaza tu ni kwamba lazima iwe imejadiliwa kwa kirefu na kujadiliwa na makamanda...nadhani itawasaidia hiyo miaka 3 si midogo...ingawa wanatakiwa kujiandaa mapema zaidi maana maisha uraiani yanawashinda kabisa....
   
 13. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #13
  Mar 5, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 201
  Trophy Points: 160
  Sheria ameshavunja ana orodha kibao za wahujumu uchumi ana orodha ya majina ya matajiri wa supadust ,yote ameyaweka ndani ya droo ,akiendelea kukandia na kuongeza muda wa serikali kuendelea kula hasara.
  Ni kosa kuficha wahujumu uchumi wakati unawakua ni sawa na kuwahifadhi sasa kuna kuvunja sheria zaidi ya hilo ,Kikwete anavunja sheria huku akijua kufanya hivyo ni kosa la jinai.
   
 14. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #14
  Mar 6, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,169
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 180
  Umri aliokuwa nao alipong'atuka Jeshi Kanali Kikwete ndio umri muafaka wa kung'atuka upiganaji.

  Kung'atuka jeshi sio sawa na kung'atuka utumishi mwingine wa uma. Wanajeshi ni wapiganaji na maafisa wao. Maafisa wanaweza kuwa wazee lakini mpiganaji lazima awe kijana.

  Mzee wa miaka 59 hatakiwi kupiga kwata, na hawezi kupigana. Kwa hivyo, wapiganaji wangeng'atuka wafikapo miaka 50, na majenerali waweze kukaa hadi wafike miaka 65.

  Life expectancy ya Manzania ni miaka 52. Katika hali hiyo, ni ajabu kusema wapiganaji wakae jeshini hadi wafike miaka 60. Watanzania wenye mika 60 ni technically dead.

  Nafahamu Canada (at least when I was there) wanajeshi wa anga wanatakiwa kung'atuka wafikapo miaka 45. Kuna sababu nzuri.

  Wengi tulioko hapa JF tulikuwa kwenye reserve army ya Tanzania (by virtue of our having been inducted through JKT) mpaka tulipofika 35. Ilitambulika kwamba huo ulikuwa umri wa kuacha kuwa mpiganaji wa akiba.
   
 15. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #15
  Mar 6, 2009
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wakati mwingine mjaribu kupunguza upinzani sio kwa kila kitu.
  Tanzania twasema tuna human resource ndogo kila mahala jeshi letu kwa mfano ni dogo kuliko hata la Rwanda. na sehemu nyingine kibao tuna upungufu wa watu. Sasa, umri wa miaka 60 watu kibao bado wanaweza kufanya kazi, sasa kuna noma hapo kuongeza umri wa kustaafu?!
  Ukienda nchi zingine, zilizoendelea kwa mfano UK, US - watu wazee kabisa kama babu na bibi yako wanachapa mzigo kama kawa.
  Huwezi kutumia sababu ya oooh life expectancy ni 52 kwa hiyo by 60 technically uko dead - haya si MAGAZIJUTO!
  Wakati mwingine mambo mnayoyashikilia bango yanaboa kweli kweli-
   
 16. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #16
  Mar 6, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,169
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 180
  Kwa nini nisiweze? Sisemi mtu mzee hawezi kufanya kazi. Nasema hawezi kupigana. Hiyo ni kazi ya vijana.

  Hizi vita za akina sisi za askari kutembea kwa mguu toka Mtukula mpaka kaskazini mwa Uganda waachiwe vijana.
   
 17. 3

  3 kids Member

  #17
  Mar 6, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapo chacha......sema wewe kiazi nikisema mie muhogo nina mzizi.....mmmhhhh!!!!!!!!!!
   
 18. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #18
  Mar 6, 2009
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kazi zingine technical, na hasa enzi hizi za ki-electronic haihitaji kutembea kwa mguu ama kwenda kupigana huko, unacheza na coordinates tu na ma-trajectories!
  na life expectancy ya 52 ni average ya wadau wote wa TZ, watu fit kama jeshini huko na watu ambao wako juu kidogo "ki-socioeconomic" wanaishi miaka kibao zaidi ya hapo.
   
 19. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #19
  Mar 6, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 4,960
  Likes Received: 448
  Trophy Points: 180
  Zidhani kama hiyo ndo ilikua point ya mleta mada.
  Yeye anachopinga ni raisi kubadili sheria kwa matamko badala ya kufuata utaratibu wa jinsi sheria inavyotakiwa kutungwa.
  Swala la kubadili umri wa kustaafu kuwa ni zuri au baya halihusiki, bado sheria inabidi ifuatwe.
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Mar 6, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 23,003
  Likes Received: 12,622
  Trophy Points: 280
  Naanzia na jeshi, umri wa kustaafu junior oficers (2nd Lt, Lt na Capt.) ni miaka 38 sasa itakuwa 41. Senior oficers (Maj, Lt.Col na Col) miaka 47 sasa miaka 50. Staff Oficers (Brig, Maj. Gen na Gen) miaka 57 sasa 60.

  Rais ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuongeza umri wa kustaafu hajavunja sheria yoyote bali ametumia mamlaka yake kwa majubu wa Katiba.
   
Loading...