`Kikwete acha kigugumizi` - LIPUMBA amchana Jakaya

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,611
1,250
7th December 2014

Lipumba amtaka achukue maamuzi magumu

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amemtaka Rais Jakaya Kikwete, kuacha kigugumizi katika kufanya maamuzi ya hatma sakata la Escrow.

Akihutubia mkutano wa hadhara wilayani Sikonge, mkoani Tabora jana, Prof. Lipumba alisema kigugumizi cha Rais Kikwete kinatokana na shinikizo analopata kutoka Chama cha Mapinduzi(CCM) na ushiriki wa baadhi ya watendaji wake katika sakata hilo.

Alisema kuhusishwa kwa mawaziri katika sakata la Escrow kunazidi kuichafua nchi kimataifa hivyo kuchelewa kutoa maamuzi kunazidi kuwapa hofu jumuiya mbalimbali za kimataifa.
Alisema Rais Kikwete alikuwa na kila sababu ya kuchukua hatua za haraka kwa kuzingatia maazimio ya bunge ili kuepusha msuguano baina ya Watanzania na jumuiya ya kimataifa.
"Ndugu zangu, Watanzania wenzangu, Katibu wa Rais aliandika barua kuafiki fedha za Escrow zitolewe kama Mwanasheria Mkuu alivyopendekeza, kwa maana ya kawaida ni kuwa kama Katibu wa Rais alikuwa akifahamu suala hilo kimaandishi hivyo hata Rais analifahamu ndio maana anapata kigugumizi," alisema Lipumba.

Lipumba alishangazwa na kitendo kilichoripotiwa na gazeti moja nchini kuwa Waziri wa Nishati na Madini kupewa ziara ya kiserikali nchini Norway, hali ya kuwa ni miongoni mwa waliotajwa kuhusika katika ufujaji wa fedha za serikali kupitia Escrow ambayo kwa mujibu wa maazimio ya bunge waliohusika walitakiwa kusimamishwa kazi kwa mujibu wa taratibu za kiserikali.
Alisema anayehusika kuidhinisha ziara ya kiserikali kwa viongozi wa nchi ni Rais lakini pamoja kuchelea kufanya maamuzi amemruhusu Waziri Muhongo kwenda kikazi nchini Norway.

Prof. Lipumba aliitaadharisha serikali kuwa endapo haitachukua maamuzi magumu dhidi ya maamuzi yaliyotolewa na bunge, wataitisha maandamano yatakayowahusisha wananchi kushinikiza serikali kuchukua hatua dhidi ya waliohusika.
Pia aliwataka wananchi wa Tabora kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kuiondoa CCM.

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,250
lipumba nakuunga mkono asimilia mia please we have to give him ultimatum mwezi ukitimia toka arudi marekani please please tuongoze tuserebuke na maandamano please viongozi kama dizani ya jk hawaendi bila pressure nyuma yao huenda yeye jk akawa anatusubiri sisi tuliwashe ili atutumie kama excuse ya kuwaambia jamaa zake kuwa wananchi wanataka wajiuzulu kwahiyo Lipumba nakupongeza kwa wazo lets excute the plan
 
Songoro

JF-Expert Member
May 27, 2009
4,126
0
Lipumba ni kama mkojo wa punda haitibu walau mafua ya vumbi seuzekifua, akome kutoa maelekezo na kashfa kwa mtetezi nakipenzi cha wengi. Lipumba kaanza kugombea Urais August 1995 wakati huo jk akiwa wazieri wa fedha leo jk anaelekeakustaafu kazi yaheshima bado yeye kashindwa walau kupata diwani kijijini kwake.Lipumba hukubaliki rudi kale vumbi la chaki
 
Kimilidzo

JF-Expert Member
Jan 3, 2011
1,346
1,225
Labda dhamira inamsuta JK kwa kuwa mkwe wake Albert Marwa mume WA Salama Kikwete ndiye alichukua zile bilioni 73 pale Stanbic. Hivyo basi anaogopa watu kumwaga mboga akimwaga ugali
 
Nicksixyo

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
949
500
Lipumba ni kama mkojo wa punda haitibu walau mafua ya vumbi seuzekifua, akome kutoa maelekezo na kashfa kwa mtetezi nakipenzi cha wengi. Lipumba kaanza kugombea Urais August 1995 wakati huo jk akiwa wazieri wa fedha leo jk anaelekeakustaafu kazi yaheshima bado yeye kashindwa walau kupata diwani kijijini kwake.Lipumba hukubaliki rudi kale vumbi la chaki
Maaaaaafiii wewe na hao unaowalinda majizi. Nilidhani mwanamke ungeweza kuwa na uchungu na nchi kumbe ----- hivi mmmffyuuuu!!!
 
politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,250
Maaaaaafiii wewe na hao unaowalinda majizi. Nilidhani mwanamke ungeweza kuwa na uchungu na nchi kumbe ----- hivi mmmffyuuuu!!!
inashangza sana hasa ukizingatia wanawake ndio wanaongoza kwa mateso makubwa hasa huko vijijini na mijini kwa kujifungua bila vifaa
 
Mtama kwa watoto

JF-Expert Member
Mar 31, 2014
394
0
Labda dhamira inamsuta JK kwa kuwa mkwe wake Albert Marwa mume WA Salama Kikwete ndiye alichukua zile bilioni 73 pale Stanbic. Hivyo basi anaogopa watu kumwaga mboga akimwaga ugali
Wacha weeeeee! 🙆Yani mambo ni sisi Kwa sisi sirizetu twajuana eeeh!!!
 
Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,939
2,000
Ujue lipumba ni sawa na homa ya vipindi mtu ameanza kugombea uongozi tangu mwaka 1995 lakini idadi ya kura zake hazijawahi kufika hata laki moja kwa mda wote huo,

kama lipumba angekuwa mboga angekuwa mlenda kabisa anatema mate bure tu.
 
Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,939
2,000
Ujue lipumba bora anyamaze tu kama kashindwa hata kumudu familia yake huku kwenye siasa sijui anafanya nini sijawahi kuona akizungumza hoja hata siku moja anaishiaga kutema mate hovyo tu.
 
Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
7,603
2,000
Lipumba ni kama mkojo wa punda haitibu walau mafua ya vumbi seuzekifua, akome kutoa maelekezo na kashfa kwa mtetezi nakipenzi cha wengi. Lipumba kaanza kugombea Urais August 1995 wakati huo jk akiwa wazieri wa fedha leo jk anaelekeakustaafu kazi yaheshima bado yeye kashindwa walau kupata diwani kijijini kwake.Lipumba hukubaliki rudi kale vumbi la chaki
Naziona akili za Mbunge Asumpta,
Naona mipasho ya Mbunge Asumpta,
Naona akili za mbunge asumpta zimewapata wana CCM wote.
Naona watanzania walivyopoteza matumaini na ngonjera za watu wenye akili za Asumpta!
 
spiritual hero

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
354
0
Lipumba ni kama mkojo wa punda haitibu walau mafua ya vumbi seuzekifua, akome kutoa maelekezo na kashfa kwa mtetezi nakipenzi cha wengi. Lipumba kaanza kugombea Urais August 1995 wakati huo jk akiwa wazieri wa fedha leo jk anaelekeakustaafu kazi yaheshima bado yeye kashindwa walau kupata diwani kijijini kwake.Lipumba hukubaliki rudi kale vumbi la chaki
Umemaanisha nini kusema arudi akale vumbi la chaki. Au umepata ashki tu ukaamua kuongea.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom