Elections 2010 Kikwete aapa kwa kutumia katiba

kibunda

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
403
52
Ndugu wadau, kama mnafuatilia vizuri, hawa jamaa, leo wana apa kutumia katiba, siyo vitabu vya dini. Je, hii ina maana gani?
 
hata mi nilijiuliza hilo, lakini nikawa ka najijibu flani hivi, sio kwamba wanaapa kwa kutumia katiba, wanaapa kwamba watailinda katiba, kile walichoshika ka ndo katiba yenyewe au ni biblia hiyo sina uhakika sana
 
JK hawezi kuapa kwa kutumia Quruan yake ya Kiislamu hata wanasiasa wengi walio Wakristo hawawezi kuthubutu kutumia Biblia.
Kama wapo ni minority few! You know what?
Wengi ya wanasiasa si wakweli wala waaminifu KWASABABU WENGI WAO WANAINGIA KWA KURA ZA WIZI NA UDIKTETA.
Kwa hiyo they are clever enough to know that once they touch those SACRED BOOKS, surely they gonna be punished by the Author of those Books Who is GOD Himself!!!

Hivi wewe unategemea Kikwete ashike msahafu wakti DHAMIRA YAKE INAMSUTA KUWA KAINGIA MADARAKANI KWA KURA ZA WIZI??Hawezi.
Mungu anajua mioyo ya Watu kwa hiyo hawawezi kutumia Biblia or Kuruani.

NI DR.SLAA PEKE YAKE ANGELIWEZA KUAPA KWA KUTUMIA BIBLIA KWASABABU NI MCHA MUNGU!!!!.
 
Mimi nimefuatilia kwa makini. Hata MC ndiye alinishtua, alitangaza wanaapa kutumia Katiba! Hoja, tunazojenga ni nzuri, lakini kitu cha Muhimu ni kujua maana ya kiapo. Ukweli ni kwamba Kiapo ni tamko rasmi. Na limewekwa kisheria. Na katika sheria ndiyo imeelezwa kuwa waape kutumia vitabu vya dini. Ndiyo maana baada ya kuapa ndipo hukabidhiwa Katiba. Lakini leo kwa kuwa waliapa kwa katiba hawakuwa na kitu cha kukabidhiwa zaidi ya huo mkuki na Ngao. Hivi sasa jk amenza kuhutubia. ngoja tumsikilize!
 
Kama utakumbukua hotuba ya Mwl Nyerere alisema "akiwa Mwisilamu ataapa kwa kurani, akiwa mkristu ataapa kwa Biblia na kama hana dini atatafutiwa namna ya kuapa lakini lazima aape"
 
Ni kweli, alisema hivyo. Lakini, kikubwa zaidi, jambo hili limeanishwa kwenye sheria ya viapo. Sasa sijui kuapa kwa katiba kuna maana gani? Labda Kama sheria imebadilishwa. Anyway, tutafuatilia zaidi......
 
SaSa hapa ni katiba/sheria imevunjwa au sanaa gani tena hii.Tunachojua walitakiwa kuapa kwa misahafu.Pia JK ameahidi kuyafanya yale aliyoyafanya kipindi chake kilichoisha,kwa maneno hayo tutegemee nini?Tumlilie Mungu jamani tumekwisha.
 
Ndugu wadau, kama mnafuatilia vizuri, hawa jamaa, leo wana apa kutumia katiba, siyo vitabu vya dini. Je, hii ina maana gani?

Nchi inaongozwa kwa katiba na wala sio bibilia au kurani. Wapiga kura watamhukumu kwa katiba sio vitabu vingine (positive law vs natural law). Pili kuna ,mdau kasema hapo juu kuwa kama umeshinda kwa kuchakachua kura utaapaje kwa bibilia au kurani?
 
Tufahamu kuwa, tuna apa kuilinda katiba, lakini hatuapi kwa kutumia katiba. Kiapo, ni komitment inayoambatana na imani ya mtu. Ndiyo maana hata mahakamani mtu anapotaka kutoa ushahidi ana apishwa. Hivyo, si sahihi kuapa kwa kutumia katiba.
 
hawa jamaa huwa ni wasanii sana wameona hali ilivyo na shutuma kuwa na udini ndio maana wanakwepa lakini pia kushika vitabu vitakatifu na umetenda dhambi yanaweza kukurudi
 
Kingunge Ngombale Mwiru alishawahi kuapa kwa kunyoosha mkono bila kushika kitabu "kitukufu" au "kitakatifu" au katiba kama mawaziri wengine walivyofanya.
 
Tufahamu kuwa, tuna apa kuilinda katiba, lakini hatuapi kwa kutumia katiba. Kiapo, ni komitment inayoambatana na imani ya mtu. Ndiyo maana hata mahakamani mtu anapotaka kutoa ushahidi ana apishwa. Hivyo, si sahihi kuapa kwa kutumia katiba.

Ibara ya 42(5) ya Katiba inasema "Kila Rais mteule na kila mtu atakayeshikilia kiti cha Rais, kabla ya kushika madaraka ya Rais, ataapa mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, kiapo cha uaminifu na kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge." Hakuna sehemu katiba inasema kuwa rais atumie kitabu cha dini kula kiapo. Labda kama kuna mtu anajua sheria ya Viapo na Matamko ya Kisheria ya mwaka 1966 inasemaje kuhusiana na kiapo cha rais mteule?
 
Ni kweli, Kingunge alishatangaza kuwa yeye haamini dini yoyote. Sheria inasema asiye amini ana "affirm". Kwa kiasi fulani hii inafanana wa waislam ambao nao wana "affirm". Wakristo wana "swear". wote wanatumia vitabu vya dini. Hapo ndipo wakivunja kiapo linakua ni kosa la jinai kwani limeainishwa kwenye Penal Code. Hilo sheria linakitambua. Hoja yangu ni kwamba, huwezi kuapa kwa kutumia katiba. Hilo ndiyo tulifuatilie linakuwaje?
 
Kheri kaapa kwa kutumia Katibaa waachane na vitabu vutukufu vya MUUMBA bse anaweza shusaha radi bse ya madudu wanayoyafanya
 
Wanatumia katiba kwa sababu wanajua kwamba wakiapa kwa vitabu vya dini zao baas laana ua Mola itawaangukia.
Inahitaji ujasiri kuapa kwa kumshirikisha Mungu.

WIZI WA KURA NDO UMEWASABABISHA WAOGOPE HATA KUSHIKA KURAN.

kitu kingine ni changa la macho kwani hao walumendago ni wadini kupindukia. mtaona jinsi ambavyo misikiti itamea kila kona nchini ilhali makanisa wakinyimwa viwanja. siku zinakuja nasema
 
Back
Top Bottom