Kikwete aanguka ghafla Jangwani...! (CLOSED)

Status
Not open for further replies.
Ni kweli ameanguka -- hii ni mara ya 3 sasa anadondoka kwenye majukwaa in 5 years. Tatizo kubwa ni kwamba wananchi hatuambiwi kinagaubaga anaumwa kitu gani. Leo tumeambiwa ni kwa sababu ya swaumu ya Ramadhani -- yaani anashindwa kumudu swaumu?

Mwaka 2005 hapo hapo Jangwani alidondoka na baadaye tukaambiwa ni kutokana na kufunga (haikuwa mwezi wa Ramadhani). Kuna uvumi kwamba ana kisukari cha kushuka. Kama ni hivyo kwani kisukari ni ugonjwa wa siri? Si waseme tu, wanaficha nini?
 
do u buy this?? of all days why today?? kwani ramadhani imeanzaa leo!! ***** mix with urs!!!
Anazingua tu... kipindi kile ilkuwa wakat wa kumaliza kampeni hapohapo jangwani...leo wakt wa kuanza kampeni hapo hapo jangwani....
 
Amerudi Jukwaani akahutubia kidogo tu kisha akaaga na kuondoka. Mkutano wa CCM kufungua kampeni Jangwani umwekwisha kwenye saa TISA NA NUSU MCHANA!
 
Inawezekana ikawa ni saumu kutokana na mazingira yaliyopo. Bila shaka tangu asubuhi alikuwa na kazi nzito za kichama katika kuhakikisha maandalizi yanaenda vizuri. Pole yake.
 
Du! Naanza kuamini kwamba Jangwani kuna nguvu ya Upako wa Mungu. Atokaye kwa kina Sangoma S/wanga, B/moyo, Tanga na Pemba asitie mguu kamwe
 
amesononeka roho alipoona watu walio mbele yake wanavyoshangilia katikati ya umasikini unaotokana na ufisadi anaouchekea. ndio, amesononeka hadi kuanguka, e Bwana mrehemu kiumbe wako huyu. amen
 
..amerudi jukwaani akahutubia kidogo tu kisha akaaga na kuondoka. Mkutano wa ccm kufungua kampeni jangwani umwekwisha kwenye saa tisa na nusu mchana!
jamaa anumwa wanatuambia swaumu....hwa watu vp bana...asisngizie swaumu
 
hivi kwa nini waislam wengine hawadondoki dondoki wakati wa mfungo??? au wanafunga kinafiki? au wanakula kwa siri??
 
Kama ni kweli basi hali yake ya kiafya si njema kabisa. Mtu huwezi ukawa unaanguka anguka hivyo kama uko na hali nzuri ya afya...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom