BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,832
- 287,782
Kikwete aandamwa Marekani
na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima
USWAHIBA ambao Rais Jakaya Kikwete aliujenga na Watanzania wanaoshi nje ya nchi, sasa unaelekea kuanza kuyeyuka.
Hali hii imejitokeza hivi karibuni, baada ya Rais aliyeko katika ziara ya Marekani, kudaiwa kuondoka bila kuonana nao, kwa kile kinachodaiwa kwamba, kabla ya mkutano uliotarajiwa baina yao, walimpelekea maswali magumu na yasiyo ya kidiplomasia.
Habari ambazo Tanzania Daima Jumapili imezipata, zimeeleza kuwa Rais Kikwete ambaye tangu alipoingia madarakani, alijenga tabia ya kukutana na Watanzania walio nje ya nchi kila alipofanya ziara zake ughaibuni, safari hii amedaiwa kukataa kukutana na Watanzania wanaoishi nchini Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka mtandao wa Jambo, Rais Kikwete anadaiwa kukwepa kukutana na Watanzania wa huko ambao walikuwa wakitaka kupata ufanunuzi kutoka kwake kuhusu mwenendo wa mambo ulivyo hivi sasa katika serikali anayoiongoza.
Kikubwa kinachoelezwa katika taarifa hiyo ambacho Watanzania walikuwa wakitaka kumuuliza Rais Kikwete ni kuhusu utaratibu uliotumika kumsimamisha kuhudhuria shughuli za Bunge, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto.
Jambo jingine ambalo Watanzania hao walipanga kumuuliza rais ni ukweli kuhusu kusainiwa kwa mkataba wa Buzwagi nje ya nchi, na kama kweli una masilahi kwa taifa, kwa kurejea ahadi yake aliyoitoa ya kupitia upya mikataba ya madini ili kuifanya kuwa na manufaa kwa nchi.
Mbali na Watanzania hao kutaka kukutana na Rais Kikwete kwa lengo la kufanya naye mazungumzo, lakini bila mafanikio, waandishi wa habari nao walimsaka kwa mahojiano, na maswali yao yanadaiwa kulandana na yale ya Watanzania.
Taarifa zinaeleza kuwa waandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji la Sauti ya Amerika (VOA) walimtumia Rais Kikwete maswali ya kutaka ufafanuzi kuhusu kusimamishwa kwa Zitto kuhudhuria shughuli za Bunge pamoja na kashfa ya mkataba wa Buzwagi.
Zinaeleza kuwa Mwandishi wa Habari wa Rais ambaye awali aliwataka waandishi hao kuwasilisha maswali yao kwanza kabla ya kukutana naye, aliwajibu waandishi hao kuwa rais hawezi kuzungumzia masuala hayo.
Taarifa hiyo inaeleza zaidi kwamba Mwandishi wa Rais aliwajibu waandishi hao waliokuwa wakimvizia Rais Kikwete kwa ajili ya kuzungumza nao kuwa maswali yao hayana (diplomatic tone), yaani hayako katika mpangilio wa kidiplomasia, hivyo rais hawezi kuyazungumzia.
Kinachodaiwa kumtatiza Rais Kikwete katika maswali hayo ambayo mwandishi wake aliomba ayapate kwanza na kumpelekea kabla ya kukutana na waandishi kuyajibu, ni kuwamo yale yaliyokuwa yakihoji uhalali wa kusimamishwa Zitto na utata wa mkataba wa Buzwagi.
Si sahihi kumtaja Zitto mbele ya rais, kwa hiyo hakuna mahojiano na wewe ndugu mwandishi, inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Hii ni mara ya pili kwa Rais Kikwete kudaiwa kuwakimbia Watanzania wanaoishi nje ya nchi, wanaoonekana kutaka kumuuliza maswali ambayo majibu yake ni magumu.
Mara ya kwanza ilikuwa London, Uingereza mapema mwaka huu, ambapo inadaiwa Rais Kikwete aliwaacha solemba Watanzania wanaoishi nchini humo kwa kushindwa kujibu maswali katika mkutano nao, na kudaiwa kwamba ilielezwa anakwenda kwenye mkutano muhimu na Waziri wa Masuala ya Afrika.
Kinyume chake, katika muda ulioelezwa kuwa atakuwa katika mkutano na waziri huyo wa Uingereza, alionekana akishuhudia mechi ya Ligi Kuu ya England iliyoihusisha Tottenham Hotspur Spurs na Newcastle United.
Lakini katika majibu juu ya tuhuma hizo, mapema mwaka huu ilielezwa kwamba, Kikwete hakukataa kujibu maswali, bali muda haukumruhusu kujibu kutokana na msafara wake kuchelewa kuingia mkutanoni.
Suala la Buzwagi lililoibuliwa na Zitto baada ya kuhoji sababu za serikali kusaini mkataba nje ya nchi, tena hotelini huko London ilhali rais alizuia kusainiwa kwa mikataba ya madini hadi hapo itakapotazamwa na kupitiwa upya, limekuwa gumzo kwa sasa.
Kama lilivyo suala la Zitto, kutajwa kwa vigogo wanaotuhumiwa kwa ufisadi hivi karibuni, pia ni jambo zito katika siasa za Tanzania kwa sasa.