Kikwete aahirisha ziara ya Mbeya

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,391
39,490
Ziara ya Rais Kikwete kutembelea Mkoa wa Mbeya iliyokuwa ianze tarehe 2 mwezi ujao imeahirishwa. Hii ni mara ya tatu kwa Rais Kikwete kuahirisha ziara yake mkoani Mbeya kwa sababu mbalimbali. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Mwakipesile amesema kuwa ziara hiyo imeahirishwa kwa sababu kuna mambo mbalimbali ya kitaifa yanaanza wakati huo ikiwemo mitihani ya darasa la saba na kuanza kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Amesema ziara hiyo itapangiwa wakati mwingine.
 
Alivyopata mualiko wa kwenda US on a state visit, inaelekea ilibidi wabadili hiyo mipango mingine maana nafikiri atakuwa huko kwa juma zima la wiki ijayo!
 
Tumemchoka huyu wakala wa mafisadi... wala asije... abaki hukohuko ukwereni na mambo yake ya kikwerekwere...
 
Kuna watu humu mumemkalia rais kwa rohombaya na chiku lakini mungu atamlinda kwa ulinzi wake mmekuwa hamsharifiki kama vile kidonda ndugu wache kumdhalilisha nyie au ndio choyo cha makundi
 
Hili ni tusi kubwa kwa raisi wetu tafadhali punguza jazba mpe heshima yake kama binadamu

Nimpe heshima mlinda wezi????????? Wezi hupelekwa mahakamani au hubembelezwa?? Athari za ujinga anayofanya zinakwenda mbali!! Watoto wanaokuwa tunawafundisha nini? Kwamba ukitaka mafanikio ufanye kazi au uibe???
 
Kuna watu humu mumemkalia rais kwa rohombaya na chiku lakini mungu atamlinda kwa ulinzi wake mmekuwa hamsharifiki kama vile kidonda ndugu wache kumdhalilisha nyie au ndio choyo cha makundi

Jaribu kujiunga na elimu ya watu wazima kama hukubahatika ku-attend primary school!!
 
Kuna nini Kikwete na Mbeya??
Kama hataki asiende kabisa nafikiri wana Mbeya wamechoka kusubiri
 
...hii ziara ya mbeya ..inategemea ramli nini..maana kila wakati inaahirishwa bila sababu...mbeya jamani mmemfanya nini huyu mwoga ..... Mbona mikoa mingine ameshatembelea kwa ziara rasmi hadi mara 3.....mbeya kunani..????..au ni nchi nyingine??
 
Kuna nini Kikwete na Mbeya??
Kama hataki asiende kabisa nafikiri wana Mbeya wamechoka kusubiri

Si unajua Mbeya inaweza ikatoa competor 2010 ndani ya Chama. Na jamaa wa Mbeya wala Hawamfagilii. Unakumbuka yule mshikaji mwingine alizomewa Mbeya. Kuna wasiwasi kuwa hili litajitokeza tena.
 
Watu wa Mbeya wana rais wao. Muungwana hawamtambui na hawamtaki. Hata mkuu wa mkoa aliyempeleka huko hawamtaki. Muungwana alimpeleka kwa malengo yake ya kufuatilia nyendo za rais wa Mbeya.
 
Hili ni tusi kubwa kwa raisi wetu tafadhali punguza jazba mpe heshima yake kama binadamuSisi tulimheshimu sana kwa kumpa ushindi wa kishindo na sasa amevunja ile heshma tuliyompa anatuona wajinga kwa kutudanganya kama watoto huku maswahiba wake wanapeta kwa ufisadi walioufanya.amekuwa kuwadi wa mafisadi kwa sababu naye ni mmoja wao. kama anataka tuendele kumheshimu awachukulie hatua za kisheria na atekeleze yale maazimio ya kamati ya mwakyembe. la sivyo 2010 asitegemee kurudi pale feri.
 
Alivyopata mualiko wa kwenda US on a state visit, inaelekea ilibidi wabadili hiyo mipango mingine maana nafikiri atakuwa huko kwa juma zima la wiki ijayo!

Swala la yeye kwenda US halikuja leo, mwingine kasema kutakuwa na mitihani ya darasa la saba, siku za mitihani hazikupangwa leo, pia kuhusu mfungo sio jambo geni wala si kwamba hawakujua itakuwa wakati gani. Vinginveyo mseme kwamba wanaoandaa hizo ziara za Kikwete ni wajinga wa kalenda ya nchi hii maana hawajui kutakuwa na nini kesho wala keshokutwa. Kuna jambo hapo, kama sio kugongana vichwa basi huenda ni hofu ya kuzomewa aliyoitaja mwenzetu mwingine hapa, hii nayo ni silaha nzuri. Tunaomba tuitumie tupatapo nafasi, natamani ingekuwa imetumika bungeni akihutubia.
 
Tumemchoka huyu wakala wa mafisadi... wala asije... abaki hukohuko ukwereni na mambo yake ya kikwerekwere...

Mkuu,

Kweli kuna haja ya kutumia lugha kama hiyo dhidi ya rais wa nchi? Pia lazima ujue kwamba statement kama hiyo sio tu kwamba unamtukana JK peke yake lakini unalitukana na kabila lake lote. Iweje makosa ya JK yaingie kwenye kabila zima?

Uhuru bila nidhamu ni fujo.
 
Kikwete amejiaibisha mwenyewe, kabila lake na taifa zima kwa ujumla. Kwanini hatuwapendi wahindi kiasi cha kuwaongelea kwenye vyombo vya habari? Ni kwasababu majambazi wakubwa nchi hii ni wahindi, kwahiyo imekuwa wahindi wote ni wezi kimawazo. Hakuna tofauti na huyo aliyesema Kikwete apeleke tabia zake kwao kwa wakwere, ni kwasababu kwa njia yeyote ile wakwere watampokea maana kimsingi alivyoiba atapeleka kwao. Samahani kama wewe ni mkwere mkuu, kimsingi usitegemee sifa kwa JK tena kwa sasa.

Ukitaka heshima jiheshimu, Cheo ni Dhamana.
 
Nimpe heshima mlinda wezi????????? Wezi hupelekwa mahakamani au hubembelezwa?? Athari za ujinga anayofanya zinakwenda mbali!! Watoto wanaokuwa tunawafundisha nini? Kwamba ukitaka mafanikio ufanye kazi au uibe???

Big point mkuu,,,anaye kubeza sidhani kama analitambua hili kwa kizazi cha baadae.
 
Kuna nini Kikwete na Mbeya??
Kama hataki asiende kabisa nafikiri wana Mbeya wamechoka kusubiri

Kati ya mikoa iliyo mpa wakati mgumu Mkapa na sasa JK ni Mbeya na Iringa ndo maana fikiria toka aingie madarakani hajazuru mikoa hii ndio juzi kaenda Iringa kuzuga....ila MBY ndo hivyo lakini waulize Marekani kaenda mara ngapi watakupa jibu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom