Mkimbizi
JF-Expert Member
- Aug 23, 2008
- 222
- 34
SERIKALI inatarajia kuanza kutumia njia ya reli kwa ajili ya kusafirisha abiria kwa mkoa wa Dar es Salaam ili kuondokana na adha ya foleni ambayo inazidi kila kukicha.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Rais Jakaya Kikwete wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa miundombinu kwa mabasi yaendayo kasi.
Rais Kikwete alisema kuwa suala hilo lilikubaliwa katika vikao vya Baraza la Mawaziri hivyo kinachosubiriwa ni Wizara ya Miundombinu kuangalia namna ya kuanza kulifanyia utekelezaji.
Alisema kuanza kutumia njia ya reli kutaleta manufaa na kupunguza foleni kwa wakazi wa jiji kwa kuwa kwa safari moja zaidi ya abiria ambao si chini ya elfu nne wataweza kusafirishwa.
"Mpango wa sasa tulionao ni kutumia njia ya reli kwa ajili ya kusafirisha abiria maana njia hiyo itasaidia kupunguza foleni na kwa wakati mmoja zaidi ya abiria elfu nne watasafirishwa, jambo hilo tulishakubaliana na Baraza la Mawaziri hivyo wizara husika tunaamini itakuwa imeanza kufanyia utekelezaji," alisema.
Haya ngoja tuone..! hahahahahahaha
Katika hatua hiyo Rais Kikwete alizindua awamu ya kwanza ya ujenzi wa Miundombinu ya Mradi wa Mabasi yaendayo kasi (DART) katika jiji la Dar es Salaam ambao utanatarajiwa kukamilika mwaka 2012.
Ujenzi huo unaoanzia eneo la feri na kuishia Kimara ambapo aliwataka wamiliki wa mabasi hayo makubwa kutumia gesi asilia ili kuondokana na uharibifu wa mazingira.
Mradi huo unaotekelezwa katika awamu sita, umefadhiliwa na Benki ya Dunia (WB) hadi kukamilika kwake utagharimu kiasi cha sh trilioni 7.3.
Source: Tanzania Daima
Kama hajadanganywa huyu sijui...! Mzee wa uzinduzi, alizindua feri, gari la wagonjwa, hoteli ya kitalii kule Arusha hahahahaha! Jamaa wasanii sana