na Tamali Vullu, Mbulu
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, amesema serikali yake ijayo itazipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini ziwe za rufaa, ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Kikwete alitoa ahadi hiyo jana wilayani Mbulu, alipokuwa akizungumza na wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Tarafa ya Haydom ambapo alisema lengo la kufanya hivyo ni kuboresha huduma za afya hapa nchini.
Alizitaja hospitali zitakazopandishwa hadhi ni ile ya Haydom, Arusha Lutheran, St Gasper iliyopo Itigi, St Francis iliyopo Ifakara, mkoani Morogoro, Ndada iliyopo mkoani Mtwara, Hospitali ya Peramiho (Ruvuma) na Hospitali ya Irembula iliyopo mkoani Iringa.
Alisema kuwa baada ya hospitali hizo kupandishwa hadhi hivi karibuni, zitakuwa na uwezo wa kuhudumia wanachi wengi na kutoa mfano kuwa Hospitali ya Haydom ikipadishwa hadhi itaweza kuhudumia wakazi wa Singida na Shinyanga.
"Tutataka kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ili iweze kushughulikia magonjwa makubwa yaliyoshindikana badala ya wanachi kwenda kutibiwa nje ya nchi. Hospitali hizi maalumu tutakazozipandisha hadhi na kuwa za rufaa, zitahudumia wagonjwa ya kawaida," alisema.
Aliongeza kuwa mbali na kuzipandisha hadhi hospitali hizo pia wataboresha mazingira ya kazi katika hospitali hizo, ili madaktari waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.
Kikwete pia alipata fursa ya kuzungumza na wakazi wa Kata ya Muslur, ambapo walimueleza kuwa tatizo la kutokuwapo kwa hosteli zimechangia kwa kiasi kikubwa watoto wa kike kupata mimba na kumuomba awasaidie wajenge hosteli.
"Mheshimiwa hapa tuna tatizo la watoto wetu kupata mimba, kwani wanaishi kwenye magheto, tunaomba utusaidie tupate hosteli, ili tuwaokoe watoto wetu," alisema mkazi mmoja wa eneo hilo.
Kikwete alisema yupo tayari kuwasaidia katika ujenzi wa hosteli lakini ni lazima wakusanye nguvu na kuanza ujenzi wa hosteli hizo.
Hivi si alipokuwa Moshi alisema ataipandisha Mawenzi Hospital kuwa ya rufaa? so keshawapiga wananchi wa Moshi changa la macho? Halafu hili la mimba na hostel si alishasema watoto wa kike wanapata mimba kwa kuwa wana kiherehere, mbona alivyojibu swali hakusema hivyo this time? Kweli JK ni kiboko, sijui kwa nini atautafuta uraisi kwa kishindo namna hiyo jamani, i am so worried na Tanzania baada ya October 31st lol