Kikwete aagiza Nyumba za Serikali zilizouzwa zirejeshwe

NDIYO!
Nyumba zinaweza zisirudi,

Lakini cha kujifunza hapa na kaTika hii forum ni kuona kuwa mtu anaweza kuwa anamwaga MAVITUZI HAPA! LAKINI LIKIJA SUALA LA MASLAHI BINAFSI aaaaaaaaaa!! MTU HUYO HUYO ATAPOTEZA MWELEKEAO KABISA! HIVI HIZO NYUMBA ZILIUZWA KWA SHERIA IPI? NA NINA NANI ANATUNGA SHERIA?? JE BARAKA ZA KUUZA NYUMBA ZILITOLEWA NA BUNGE!

NDUGU ZANGU TUOMBE MUNGU TU NYUMBA TULIZONUNUA AU AMBAZO NDIGU AU MARAFIKI ZETU WALIUZIWA ZISIRUDI LAKINI SIO KUSEMA HILI SERKALI INARUHUSIWA KISHERIA NA HILI SERIKALI HAIRUHUSIWI!

NI SISI HAWA HAWA TUKIPTA MADARAKA BASI KELELE ZOTE TUNATUPA CHOONI!
 
Mkira, hapo umenena!


ubinafsi unatumaliza na utaendelea kufanya hivyo kwa muda mrefu hadi lyamba!
 
Kikwete: Nyumba zilizouzwa maeneo nyeti zitarudishwa

Na Jacqueline Liana (source - uhuru la leo)


RAIS Jakaya Kikwete amesema baadhi ya nyumba za serikali zilizouzwa kwa maofisa wake wakati wa uongozi wa awamu ya tatu, zitarudishwa serikalini.


Alisema hayo jana alipokuwa akilihutubia Taifa katika utaratibu aliojiwekea wa kuzungumza na wananchi kila mwisho wa mwezi.

Jana alifanya hivyo Ikulu jijini Dar es Salaam katika tukio lililohudhuriwa na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari na baadaye Rais Kikwete kujibu maswali baada ya hotuba yake.

Alisema si nyumba zote zilizouzwa kwa watumishi hao wa serikali zitarudishwa serikalini, bali zilizopo katika maeneo ambayo yanasababisha hali isiyo kuwa ya kawaida katika utendaji kazi wa serikali.

"Nyumba hizi zimeuzwa, kwa kweli hatukusudii kuzichukua nyumba zote, lakini kuna maeneo tuna matatizo nayo," alisema Rais Kikwete.

Alitoa mfano wa hali hiyo kwa kusema kwamba utakuta nyumba ya kamanda wa polisi wa wilaya ameuziwa kamanda huyo na nyumba yenyewe iko ndani ya kituo cha polisi.

"OCD kauziwa nyumba ya OCD, eneo la kituo cha polisi... OCD yule kahama katoka Mafia kahamia Mtwara au kastaafu nyumba ile kapangisha, sasa yule aliyepangishwa pale kituoni... haya ni maeneo ambayo tunapaswa kuingilia kati," alisema Rais Kikwete na kusababisha kicheko miongoni mwa wahariri.

Rais alisisitiza kwamba, kitakachofanyika ni kuangalia maeneo yale ambayo serikali haina budi kuyafanyia marekebisho.

"Hili ndilo jambo kwa kweli sasa hivi tunalolishugulikia," alisema Rais Kikwete.

Akizungumzia mashirika yasiyo ya kiserikali, Rais Kikwete alisema baadhi ya NGO's zimeundwa kwa ajili ya kuwapatia watu ajira na si dhamira ya dhati ya kushughulikia makusudio ya kuanzishwa kwa taasisi husika.

Alisema alipokuwa Marekani katika moja ya mikutano, mmoja wa marais alitaka NGO's ziwe na uwazi wa kueleza pesa wanazopokea na miradi wanayoitekeleza.

Kuhusu wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu 'machinga', Rais alisema anashukuru utaratibu wa kuwaondoa katika maeneo yasiyoruhusiwa, umefanyika kwa amani, na kuitaka halmashauri ya jiji la Dar es Salaam iendeleze maeneo waliyohamia wafanyabiashara hao.

"Viko viwango vya kufanya hizi shughuli na sisi tukiendelea kufanya hizi kazi katika mazingira ya udongo tutachelewa sana kufikia viwango vinavyotakiwa kimataifa," alisema Rais Kikwete.

Aliagiza Jiji kuhakikisha kuwa huduma muhimu kama vyoo na maji zinapatikana katika maeneo walikohamia machinga, hatua za kuwapa elimu ya biashara zichukuliwe ili wapatiwapo mikopo waitumie vyema.

"Maadam, sasa wametulia na wana anuani ni fursa ya kuangali na kutoa kipaumbele katika mafunzo ya kufanya biashara na mikopo, ili shughuli zao ziweze kukua ifikie siku ambayo mtu anatoka Mchikichini, anaanzisha duka lake," alisema Rais Kikwete.
 
Mkira,
Ukisoma between the lines inaonekana zitarudi chache sana.
Sana sana watanyang'anywa wale waliopangisha katika maeneo ya "vituo vya polisi."
 
Kuna wakuu wa mikoa walionunua nyumba.. sasa wamestaafu na wengine wameamishwa.. nao pia wapo katika huko mkumbo..
 
JeiKei wrote:
Kuna wakuu wa mikoa walionunua nyumba.. sasa wamestaafu na wengine wameamishwa.. nao pia wapo katika huko mkumbo..

hoja hiyo hiyo unaweza kuitumia kwa makatibu wakuu, mawaziri, waziri mkuu, na hata Raisi........
 
Naona waathirika wa uamuzi huu ni wale wale wakina pangu pakavu...kama walikuwa na haki ya kuuziwa sioni sababu ya kunyang'anywa, kama sababu ni za usalama basi waanze kuwajibishwa wale walioidhinisha uuzwaji huo kabla ya kuwaadhibu wanunuaji.
 
Jasusi,

kama atafanya hivyo utakuwa uhuni wa aina yake!


Kwanza kama ni kweli naye alinunua nyumba ni vema airudishe kwanza. maana haitumii kwa kipindi cha miaka 10 ijayo na anaweza kujenga nyingine!

Isije ikawa ni yale yale ya PCB kuumiza watendaji wa kata na mahakimu wa wa mahakama za mwanzo! Ngoja tusubiri.


Ni kweli waliofanya uamuzi wa kuziuza watashughulikiwa tu siku za baadaye siyo lazima awe JK.
 
Huu ni usanii. Haoneshi kujutia uamuzi uliofanywa na serikali. Anachokifnaya ni kuwatoa kafara baadhi ya maafisa wazamani ikiwa ni jitahida zilezile za kutafuta sifa, ila nia sio njema!
 
Kwa wale walionunua nyumba lazima zitawauma sana. Lakini lazima ufahamu ukitaka kupona malaria sugu lazima unywe kwinini au utundikiwe drip la kwinini. Kila mtu anajua kwinini ni chungu sana. Baada ya kupona unaweza ukawa kiziwi kwa siku kadhaa, lakini mwisho utapona. Sasa ile dawa ya ufisadi wa TZ ndiyo hiyooooooooooooooo. Chungu sana. Kina ES, mlalahoi na Moshi kule Papua New Guinea wanaogopa kuinywa. Dalili zinaonyesha walinunua nyumba zetu makabwela. Kikwetu udumu. Tutakuombea usiku na mchna. Usitelekeza maneno utalaaniwa kama fisadi MKapa.
Kwa hiyo wale waliobangaiza kama kina ES na yule jamaa wa PNG pamoja na majambazi ninayoyotaja kila siku, yaani Baba lao Mkapa na Mama lao Anna Mkapa, washika mikoba kina Lowassa , Kigoda, jambazi Mary Ndossi, Aliyekimbia Sumaye n.k. wazirudishe nyumba kwa hiari.

Kikwete anajua kuuza nyumba za serika haikuwa sera ya CCM. Siyo mjinga kama wanavyodhani. Ila tu sasa hivi tunategemea kusikia kuwa MKapa yuko Milembe anatibiwa maradhi ya akili. Kwa sababu maamuzi ya kuuza hizo nyumba aliyofanya yanakufanywa na mtu mwenye ugonjwa wa akili. Namkumbukumbu ndugu mpenda haki na Mkweli Mbunge mmoja wa Kanda ya Ziwa, aliwahi hivi mnauza za serikali kama vile baada ya serikali ya Mkapa ndiyo mwisho wa dunia. Lakini BM aliziba masikio. Rudisheni nyumba mlionunua. Hata Bwana Mapesa, Cheyo alishawatahadharisha walionunua.
Kikwete Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.
 
Nimeona nichangie kidogo kwenye hili swala la nyumba.

Nakumbuka kule bcs times nilikuwa mmoja wa watu waloiunga mkono uuzaji wa hizi nyumba ila pale nilipoona wanauza nyumba na kuanza kujenga nyingine mpya nakajitoa katika hilo. Sababu zangu za kuunga mkono bado ziko valid kwa mfano kuna mtu humu amejiita mlalahoi ana uchungu na hizo nyumba, huo uchungu unatoka wapi? Wewe Mlalahoi ulishwahi kuvuta hata hilo geti la makuti na kwenda kuigusa hiyo nyumba na kudai hii nyumba ni yetu?

The real question is how do you benefit from those houses, somebody please tell me how? Je wewe mlalaho unajua serikali inatumia kiasi gani cha hela kuzihudumia hizo nyumba ambazo wanaishi mafisadi? Kwa nini tuwahudumie mafisadi?

Ni heri kuwapa hizo nyumba na kuacha kuwahudumia. Ningekuwa mimi ni rais ningegawa hizo nyumba bure! Kama hizo nyumba zingeuzwa millioni 400 hizo hela zingeenda wapi? Hata hizo hela zilizopatikana kwa uuzaji wa nyumba zimeenda wapi? Now you are thinking.

Eti una uchungu, uchungu wa kuliwa hela? Please someone tell me hizo nyumba zikirudishwa ni kivipi mlalahoi atafaidika? Naelewa watanzania ujamaa umewaingia sana eti nyumba zetu wakati hata geti huruhusiwi kugusa.

Baraza la mawaziri lilipitisha uuuzaji wa hizo nyumba kwa watumishi wa serikali. Pale nilipoona hata Mangula anauziwa nyumba wakati yeye alikuwa siyo mtumishi wa serikali nilibaki kinywa wazi. Kama kuna mkuu wa mkoa au wilaya aliuziwa nyumba basi hilo lilikuwa ni kosa na anastahili kunyang'anya auziwe mtumishi wa serikali.

Technically, wakuu wa mikoa na wilaya siyo watumishi wa serikali, vyeo vyao ni political position, hawakustahili kuuziwa nyumba. Nadhani nyumba hizo wanyang'anywe na wapewe watumishi wa serikali kama walimu kwa bei ya kutupa au ikiwezekana wapewe bure. Who is going to benefit anyway! Mimi naishauri serikali iachane na hii biashara ya nyumba, gharama ya uendeshaji wa nyumba itumike kujenga shule na mahospital.

Tumesikia mambo aliyosema JK kule NY kuwa hana mpango wa kumjengea mtu yeyote nyumba kila mtu ajitengeneze kwake nadhani nyie mnaojiita walalahoi hilo ndilo litakiwa kuwauma zaidi ni kivipi Libya iliamua kuwajengea watu wa kipato cha chini makazi ni kwa nini kila siku US wanahangaika kuwajengea walalahoi wa US nyumba! Serikali yetu haina mpango huo eti itakujengea barabara then what! Hata kama barabara ya ghorofa ikipita jirani yako haimaanishi kwamba utakuwa na uwezo wa kujenga nyumba wakati huna kipato cha kutosha na gharama za maisha zimepanda mara tatu na hakuna mtu anayeona hilo kwa ajili ya kumpenda sana rais.

Nadhani walalahoi ingewauma zaidi hiyo kuliko hili eti nyumba zinarudishwa na kupewa kundi jingine la mafisadi + kuhudumiwa pia na hela za toilet papers walahahoi hamyajui haya mnabaki tu nyumba zetu. Nyumba zenu! mwambieni rais awajenge za kwenu na nyie mjinafasi.
 
Lutuli,
I hope you are right. Lakini usijeshangaa ukikuta kuwa zile nyumba hazirudi. Hivi Mawaziri nao ni civil servants? Hawa ndio walikuwa wa kwanza kujinyakulia.
 
Hayumkiniki nyumba zitakazorudishwa ni zile za wasiokuwa wanamtandao wake! Ni kweli zipo zilizouzwa even line police, Lakini watakaobanwa kwanza ni wapinzani zwke kisiasa, maRPC alowapiga chini pia maRC hasa mbaya wake Banduka aliyejilimbikizia mali huko Lindi kwa wakwe zake Kikwete, Mashishanga and the like! Wengine waliobaki kwenye system wataendelea kupeta.


...................................
:U Can't Change The Nature:
 
All these guys are just playing with our minds. There's so many issues and you come out to announce this BS. I just read that few hundreds Form IV students won't be able to sit for their final national exams or some of the applicants for the higher learning won't be able to secure loans, what the hell is that? I think we just need to dissolve the whole government and stand people who can think and use their judgement.
 
unajua serikali ya ccm imesha zoea kutugeneralize sisi watanzania,
wao wanafikiri kuwa katika nchi hii wanaweza kufanya lolote na hakuna wakufanya kitu,
bila shaka wameshasahau historia ya watanganyika hawa,
hawa ndugu zetu walionunua hizi nyumba kama wanabusara ni bora wazirejeshe hizi nyumba kwasababu nyumba hizi zitarudi tu hata baada ya miaka 20 au 30, wanatakiwa walifahamu hilo vizuri sana.
hivi ni akili gani hiyo nyumba za serikali kule masaki zinauzwa kwa bei ya kutupa halafu wale walionunua hizo nyumba wanapangisha wazungu tena,
yaani maeneo ya kule masaki siku hizi mtanzania wa wakawaida unaogopa hata kutembelea maana unaweza kuumwa na mbwa wa wazungu, na ukiwa hiyo mitaa utafikiri haupo tanzania,tunaenda wapi?
yale yalikuwa ni maeneo ya viongozi wetu wa serikali kujivunia kule sasa hivi tumewarudisha wakoloni?
hivi mwalimu alipo waambia mtakuja kubinafsisha mpaka ikulu si ndio haya yametokea tayari?
kama mpaka nyumba ya dc inauzwa si ni ikulu hiyo?
jamani tuwe makini pengine hata serikali ilishauzwa siku nyingi hatuna habari.
 
Kama ni kubinafsisha kwa vile hawataki serikali iwe na mali zozote za kusimamia, basi wauze Ikulu na maofisi yote ya serikali kwa wawekezaji binafsi. Serikali iwe ikilipe kopi tu, in fact wanaweza kusevu sana badala ya kutumia mabilioni kununua vifaa vya kuzima moto ikulu, kazi hiyo akiachiwa mwekezaji atabana sana matumizi kusudi kuongeza faida.

Of course huo utakuwa ni wenda wazimu. Kwa hiyo hata hili la kuuza nyumba za serikali ni wenda wazimu. Hapa nilipo tunahangaika kumjengea kiranja wetu nyumba ya kukaa baada ya ile ya zamani kuonekana imepata upungufu. Swala la kumkodishia nyumba halipo kweneye equation.
 
Kuuzwa kwa nyumba za serikali ilikuwa ni shinikizo toka kwa IMF, na World Bank, but jinsi zilivyouzwa sivyo walivyokuwa wameambiwa!

Nashangaa wanavyooona aibu kukubali mbele ya umma!
 
Mzee Es, H
Hayo maneno, na huchukua vichwa kuweza kufumbua kisa mkasa!..
Viongozi wetu hutafuta kisababu tu cha wao kupindua...Kuna document moja ya Global Organization of Parliamentarians Against Corruption (GOPAC), imesisitiza neno moja tu kwa nchi masikini - ACCOUNTABILITY - the simple notion that - one is held accountable for their deeds and actions.
Guess it's about time we educate the mass about democracy..and that
Parliamentarians are elected by their constituents to publicly oversee the government...Na sio kinyume chake!..

Uncle! shukurani zaidi - You are reasonably independent, open, and transparent checking on government. That's what we need. kwa nini usiwe mbunge Uncle!
 
Mzee ES,
Kama ni shinikizo la IMF, World Bank ni nchi ngapi zinazoendelea ambazo zimefanya hivyo? Nadhani waliojiuzia hizo nyumba wanasema hivyo tu kuficha aibu zao. Nenda Singapore uone zile nyumba zilizojengwa na Waingereza kama zile za Oyster Bay bado ni mali ya serikali.
 
Back
Top Bottom