Kikwete aagiza Nyumba za Serikali zilizouzwa zirejeshwe

tibwilitibwili

Senior Member
Sep 12, 2006
181
10
Hatimaye Kikwete Afanya Kweli


  • Aagiza Nyumba za Serikali Zilizouzwa Zirejeshwe

Na Mwandishi Wetu

Rais Jakaya Kikwete ameanza mchakato wa kuhakikisha nyumba za serikali zilizouzwa kwa watumishi wake wakati wa uongozi wa Awamu ya Tatu, zirejeshwa serikalini.


Habari za uhakika kutoka baadhi ya maofisa waandamizi serikalini zinasema Rais Kikwete ameamua kuzirejesha nyumba hizo katika mikono ya serikali kwa kuzinunua upya kutoka kwa watumishi waliokwisha kuzinunua.


Kwa mujibu wa habari hizo Rais Kikwete ameiamuru Wizara ya Miundombinu kufanya tathmini ya kina ya ununuzi wa nyumba hizo kubaini ni kiasi gani kinastahili kurejeshwa kwa wote walionunua nyumba hizo ili hatimaye zirejeshwe Serikalini.


Inaelezwa ya kuwa kitakachotathmiwa ni kiasi gani cha fedha kilichokwisha lipwa na kila aliyenunua, ikizingatiwa ya kuwa si wote ambao wamekwisha kumaliza kuzilipia nyumba hizo.


Habari ndani ya Wizara ya Miundombinu zinaeleza ya kuwa waliozinunua watatakiwa kuzirejesha na kulipwa kiasi ambacho kila mmoja alikuwa amekwishalipa kwa mujibu ya mikataba waliyopewa.


Inaelezwa kwamba Rais Kikwete ameamua kuzirejesha nyumba hizo Serikalini kwa vile hivi sasa Serikali inakabiliwa na uhaba mkubwa wa nyumba kwa watumishi wake wanaoteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali na wanaohamishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine.


Kwa sababu hiyo serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuwapangisha katika hoteli wafanyakazi wengi wapya wanaokosa nyumba katika maeneo wanayopangiwa kufanya kazi, kimesema chanzo chetu cha habari.


Sababu nyingine ni kwamba Serikali imeona kwamba nyumba hizo bado zinatakiwa kuendelea kubakia katika mikono ya serikali kwa sababu ziko katika maeneo yaliyotengwa na maalumu kwa ajili ya viongozi na watumishi wa Serikali.


Chanzo chetu cha habari kilisema kwamba tathmini ya nyumba hizo imeanza kufanywa na Wizara ya Miundombinu ambayo itawasilisha ripoti yake kwa Rais Kikwete kwa ajili ya utekelezaji.


Waziri wa Miundombinu, Basil Mramba hakuweza kupatikana kwa njia ya simu kwa vile anafuatana na Waziri Mkuu Edward Lowassa katika ziara Mkoani Kigoma.


Naibu Waziri wa Miundombinu Dk Makongoro Mahanga alipoulizwa hakukataa wala kukubali kuhusiana na suala hilo.


Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa nyumba za serikali zilizouzwa nchi nzima tangu mwaka 2002 ni 6,000.


Mauzo ya nyumba hizo yalikuwa yakifanywa kwa awamu na Wakala wa Nyumba za Serikali chini ya Ofisa Mkuu Mtendaji wake, Togolai Kimweri.


Serikali ya awamu ya Tatu ilisema wakati huo ya kuwa fedha zilizopatikana zingetumika kujengea nyumba nyingine kwa ajili ya watumishi wa serikali katika maeneo mbali mbali kama Dar es Salaaam, Arusha, Dodoma na Mwanza.


Baadhi ya nyumba hizo zimekwisha kujengwa Dar es Salaam kwa ajili ya maofisa waandamazi wa Serikali wakiwamo Mawaziri.


Uchunguzi unaonyesha ya kuwa wakati Kikwete akidhamiria kuzirejesha nyumba hizo Serikalini, baadhi ya watumishi wa Serikali waliozinunua wamezifanyia ukarabati.


Wengine wamejenga nyuma nyingine ndani ya viwanja vya nyumba hizo ambavyo ni vikubwa, yaani ‘low density'


Vivyo vivyo wengine wamepangisha kwa makampuni binafsi na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOs) na nyingine zimejengwa maduka ya biashara na ofisi kwenye uzio wa nyumba hizo, hususan zilizopo karibu na barabara.


Uuzaji wa nyumba hizo za Serikali ulioanza mwaka 2002 ulisababisha malumbano na mzozo mkubwa miongoni mwa watanzania, wakiwamo viongozi wa vyama vya siasa, baadhi wakipinga kuuzwa kwake.


Baadhi ya wananchi na viongozi wa vyama vya siasa walionyesha masikitiko yao kwa hatua ya kuuzwa nyumba hizo, hasa kwa bei ndogo, wakisema haikulingana na thamani na tathmini ya nyumba na viwanja vya nyumba hizo, kwa pamoja.


Wananchi pia walitaka uwepo uwazi wa majina ya watumishi waliouziwa nyumba hizo na bei waliyonunulia, jambo ambalo Serikali ilikataa kulitekeleza.


Serikali ya Awamu ya Tatu ilisisitiza kuziuza nyumba hizo, ikisema itakuwa ikijenga nyingine kutokana na malipo ya ununuzi wa nyumba hizo.


Miongoni mwa walionunua nyumba hizo ni mawaziri wengi, kama si wote, wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu, hasa katika Mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma, kwa kuwa walikuwa wakiishi katika nyumba hizo.


Chanzo: Mtanzania Jumapili Toleo Namba 3784
 
kama taarifa hii ni ya kweli basi utakuwa ni uamuzi wa kwanza mzuri kufanywa na rais kikwete.
tunaomba urudishwaji wa nyumba hizo usiwe wa upendeleo, tunaomba mawaziri woote walio nunua nyumba hizi wazireje serikalini,
na mfano mzuri uanze kwa kikwete mwenyewe kuirudisha ile nyumba yake.
na zaidi wale waliohusika kuuza nyumba hizi lazima wachukuliwe hatua kali.
tunaomba mheshimiwa raisi usiishie hapo tu endelea kufatilia mambo muhimu yanaonendelea kudhoofisha taifa hili.
watu waache kuleta mchezo na mali za serikali, tunaomba mrudishe nidhamu ya hali ya juu inapokuja kwenye mambo ya serikali na kodi za watanzania.
na hata hapo kwako ikulu matumizi kama hayo ya mkeo kutumia ndege ya serikali kwenda kuhudhulia vituko vya dictator mfalme swazi tunaomba muache,badala yake hizo pesa zitumiwe kwenye kutatua matatizo ya umeme nk.
nawakilisha
 
hapo ndipo kasheshe.. serikali itafikishwa mahakamani!!! kama serikali inaweza kukiuka mikataba namna hiyo, si tuone wanafanya hivyo kwenye madini...na masuala ya nishati.. au kwa vile hawa ni Watanzania wenzetu basi tunaweza kukiuka mikataba!! Sidhanii serikali itafanikiwa kwenye hili.. kilichoenda kwa mganga hakirudi!!!!
 
kama hizi habari ni za kweli,basi kweli JK anahitaji pongezi za hali ya juu! Kuuzwa kwa hizi kulikuwa kwa kifupi ni kichekesho, hasa ukizingatia bei ya hizo nyumba walivyouziana. Nyumba iko Oysterbay inauzwa milioni 18 au 20 mpaka 30,wakati mashirika kama TTCL waliuza nyumba hukohuko O/bay shs milioni 400!

Ukiangalia kwa upande mwingine,wale wazee waliokuwa wa kwanza kukaa kwenye hizo nyumba,baada ya uhuru,wao pia walifikiriwa?

Maana mtu kama Balozi Sharif,aliyekuwa waziri mdogo wa mambo ya Nje,amekaa nje ya nchi hii miaka yote,na inasemekana ana passport ya uingereza pia,anarudi hapa na kuuziwa nyumba kwa bei ya kutupa,matokeo yake kaitengeneza na kuupangisha ubalozi wa UAE pale Kaunda Drive,kwanza walivyouza si walisema zile nyumba wanauziwa ili wakae wenyewe na hawaruhusiwi kupangisha...sasa mtu ananunua nyumba milioni 20,anapangisha kwa dola 5,000 kwa mwezi,hapo haki iko wapi?Miezi 4 pesa yake imerudi!

Hao wazee waliogombea uhuru mpaka nchi hii ikawa huru si ndio angalau wangestahili kupewa hizo nyumba kwa kuuziwa na kuwekewa utaratibu mzuri ambao ungewafanya waweze kuzilipia hizo nyumba...wengi wao wako hoi tu maskini,na hio sio lazima wapewe za O/bay. Bila ya wao hizo nyumba za kuuzwa zingetoka wapi?

Sasa logic iko wapi,unamtoa waziri O/bay unampeleka Kijitonyama,kwa kuuza nyumba ambayo angekaa,na kutumia pesa zaidi kumjengea nyumba kwenye sehemu ambayo kihistoria haikutengwa kukaa viongozi?

Mawaziri wengi wamegoma kuhamia nyumba hizo mpya kwa sababu wanasema hakuna privacy,maana wote wamewekwa kwenye kijiji!Hivi Mwalimu alivyosema 'i wont let my country go to the dogs..' reading between the lines u get a different perspective!

Pongezi sana JK na hao waliotoa hio stori kwenye gazeti,maana sisi Watanzania have been taken for a ride for too long.Na kwa sababu kawaida yetu,tutanung'unika,then yatapita.Tuna sifa hizo,hata sasa hivi issue ya umeme,hio Kiwira Coal Mine has been there miaka nenda rudi,leo ndio wanasema wanauwezo huo na Serikali finally imekubali,lakini hakuna mtu anayehoji,jamani mpaka IPTL inaingia nchi hii, (hakuna lolote wanalofanya),kumbe kulikuwa hakuna haja ya wao kuja kama hawa Kiwira wanasema wana uwezo wa kuzalisha megawatt 200! Na ni kwamba wana uwezo wa kuzalisha zaidi ila serikali imewapa kibali cha kuzalisha umeme huo tu!

Hili la nyumba watu walinung'unika na likapita.Nchi nyingine hata hizo nyumba zingepigwa mawe! Leo Mtanzania wa kawaida kupata mkopo wa kununua nyumba ni mbinde,na yeye analipa kodi,NSSF na vurugu nyingine nyingi tu,lakini huko juu,watu wanakopeshana majumba,tena they have the luxury of choosing where they want to live.Sasa most of those are no longer in the government,they are now ordinary citizens with mansions in Oysterbay,not in their wildest dreams did most of them ever think they would own property in such a prime location...

Maana ule ulikuwa ni mradi wa Tajirika na Serikali ya Awamu ya Tatu! Ila sasa huo utaratibu wa kuzinunua upya hizo nyumba nao usiwe tena mradi wa Tajirika ......
 
Sitasema hongera hadi nione kweli kama nyumba zinarudi .JK alitamka baada ya kuchaguliwa kwamba hakuwa na mpango wa kutidisha nyumba hizo maana kufanya hivyo kungali sababisha vita .Nikajiuliza hiyo vita na nani hasa .JK ana nyumba alinunua .JK uamuzi wa kununua nyumba aliushiriki.Je kwa nini serikal inunue hizo nyumba badala ya kuwaridishia ambao wamemaliza madeni yao na ambao hawajamaliza badala ya kutafunta njia ya kuwa pooza kwa kununua hizo nyumba? Sijaona nia ya JK hadi muda huu .
 
Mzee Mwanakijiji,
Usishangazwe na "mbwembwe" kama hizo. Kumbuka enzi za Mwalimu, na hata Mzee wa Lupaso naye alianza na mtindo huo wa kutangaza mambo fulani "mazito" akiwa nje ya nchi au nje ya Dar.

Sasa usishangae pia pale JK atakaporejea toka majuu umati wa wakazi wa Dar ukaenda kumlaki kwa maandamano uwanja wa ndege, kama sio maandamano ya kumuunga mkono huko mikoani!
 
Huu ni usanii tu wa serikali ya JK. Sasa hivi kuna ishu nyeti kama umeme na madini; na foreign reserves zinakwenda kama maji. Hakuna solution huko. Badala yake ndio kuwadanganya wadanganyika na kanyaboya hilo. Ama kweli sisi watitu tu mambumbumbu.
 
Kama habari hii ni ya kweli narudia tena kama habari hii ni ya kweli huu hutakuwa ni uamuzi wa kwanza mzuri kufanywa na JK.

Lakini nani kaandika hii habari?
 
Wee tibwiltibwili,

anyway yetu masikio na macho. kama ni kweli, utakuwa ni uamuzi wa busara.

Mzee Mwanakijiji
endapo JK ameamua hivyo basi hiyo itakuwa ni indiketa kwenye mikataba mingine i guess!!
 
Hivi hiyo ni akili au matope?Serikali iliuza nyumba kwa watumishi wake,pengine kwa kisingizio kwamba imeshindwa kuziendesha.Leo hii muuzaji anataka kununua alichokiuza kwa madai ya kubadilika kwa mazingira ya wakati mauzo yanafanyika!!!Tanzania haiishi vituko.Kwa taarifa yenu,hata kama zoezi hilo litafanyika (i doubt if it will ever) utafanyika usanii hapo wa watu kujichotea mamilioni ya fedha kama fidia.Huu ni mradi wa kisanii uliobuniwa kuwasaidia vigogo (ambao ndio asilimia kubwa ya wanunuzi wa nyumba hizo) kupata fedha za kulipa madeni waliyotengeneza kwenye kampeni.
 
Sisi watanzania walalahoi nyumba hizo zinatuuma sana. hainiingii akilini kuuza nyumba kwa mfano, Oysterbay, kisha kujenga nymba tena kijitonyama. Hata kama serikali itaingia hasara, nymba hizo zikirudishwa ni bora. Nangojea magorofa aliyonunu Mama BWM yarudishwe. Ndipo nitapata matumaini kuwa vile vile itafukuliwa mikataba feki ya kina Kigoda, Mama Ndossi(IPTL), Ami Mpungwe, na majambazi/mafisadi /walafi wengine kama hao.
Najua baadhi ya walionunua nyumba hizo wamo humu. Lakini ndiyo hivyo lazima watambue mali za uma ni vizuri zikiuzwa kwa ridhaa ya umma (Bunge), hata kama ni bunge bomu kama la CCM.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Jana nilimfikishia posting yako BWANA MKUBWA, na posting za issue ya bajeti yetu, heshima niyngi kwenye hiyo issue ziende kwa Mzee Augustine Moshi na argument zake, na hasa namba za inflation zilimshitua sana!

Ninarudia tena Bravo, wekeni vitu hapa hakuna kulala!
 
Yangu Macho na masikio nikisubiria.

Kama atazirudisha itakuwa BIG PLUS!

Tayari ninaona waliozinunua au ndugu zao wameanza kulala humu!

Ila sina imani kama zitarudi. Hii source ni ya lini na ni katika gazeti gani?

Siku moja nilikuwa nikiongea na mama mmoja ambaye naye alinunua nyumba ya serikali. Nilmwambia mama iko siku hizo nyumba tutazirudisha!!!!!!

Akasema kamwe haitawekezekana MAANA NYUMBA NIMEPEWA NA MUNGU!

HUYO MAMA NI MLOKOLE! LABDA MKAPA NI MUNGU WAKE!


Anyway, hata mimi sina imani kama nyumba zitarudi serikali hivi karibuni!
 
Inawezekana ni kweli nyumba zitarudi. "Maybe the son of Tanzania" ameamua kufanya kweli. Make your history JK.

Nimesikia leo redioni kupitikia kipindi cha magazeti. Kuna habari hii kayika gazeti la MTANZANIA LA LEO JUU YA hii ya serikali kufikiria kurudisha hasa zile za wakuu wa mikoa na viongozi waandamisi serikalini!

ILA CHA AJABU WAMESEMA KUWA JK ANASEMA ATAWAULIZA KWANZA WAIRI MAGUFULI NA MKAPA!

LINAPOKUJA SULA LA KURUDISHA NYUMBA! MAGUFULI HUWA ANAKUWA TYSON!

ILA PIA NIMESIKIA WALIOZINUNUA WANALALAMIKA KUWA SIYO VIZURI KUZIRUDISHA!

WENGI WANASEMA SERIKALI ILIKUWA IMESHINDWA KUZIHUDUMIA!

KWANI SERKALI ZILIZOPITA ZILISHINDWA HILO LA NYUMBA TU?! MBONA NI MENGI MBONA HAJAUZA YOTE HAYO! NI MENGI AMBAYO SERKALI ZILISHINDWA NA HADI SASA ZIMESHINDWA UMEME NK !

JK RUDISHA NYUMBA HIZO BILA KUANGALIA WATU HAO WACHACHE USONI HAWANA HAYA! WENGI WANAKUUNGA/WATAKUUNGA MKONO KWA HILO NA UTAACHA HISTORIA NZURI KWA HILO.
 
Hiki ni kiini macho .The son fo Tanzania kabeba watu kibao kwenda nao US huku wakiwa watupu hawaja jiandaa .Leo kurudi nyumba ni hadithi na urudishaji wa njia iliyo kuwa suggested kwangu naona ni kupotezeana muda kiini macho cha Siasa .Walio nunu hizo nyumba anawajua na alishiriki uuzaji wa nyumba maana lazima deal ilianzia na baraza la mawaziri yeye akiwemo mbona asitoe hoja huko huko na akaishia na nyumba pia ? Jamani hii ni comedy sina mataumaini kabisa.
 
You cannot eat your cake and have it. Ukishauza nyumba, basi sio yako tena! Huwezi kusema una haki ya kurudishiwa. Nyumba zilizouzwa na serikali sio za serikali tena, na serikali iache dhana potofu kwamba ni nyumba zake, irudishiwe.

The government can revoke ownership of land but not ownership of a house. Haina hiyo nguvu, na sheria zipo.

Tunazidi kuona mifano ya utawala hovyo. Ukishafanya uamuzi wa kuuza nyumba, na ukaziuza, basi zimeuzika. Tumia hizo fedha ujenge nyumba nyingine. Kama uliziuza bila kupokea fedha za kujengea nyumba nyingine, basi umekosa akili, na gharama ya huo upuuzi ni yako, sio ya wanunuzi. Acheni kubabaisha wananchi.

Augustine Moshi
 
Mwalimu Mushi
Unapoteza muda wako kuandika maneno mengi sana .Kwa kifupi hakutakuwa na nyumba kurudi . Maana kasema kabla ya kuanza kuzirudisha atamuuliza waziri wa ujenzi na BM naye ataulizwa sasa unategemea nini ? BM aseme rudisha ina maana nyumba yake pia itarudi .Sasa hiki si kichekesho ?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom