Kikwete aagiza mkataba na Rites uvunjwe haraka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete aagiza mkataba na Rites uvunjwe haraka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Mar 24, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kikwete aagiza mkataba na Rites uvunjwe haraka

  RAIS Jakaya Kikwete ameiagiza Wizara ya Uchukuzi kuongeza kasi ya kuvunja mkataba baina ya Serikali na Kampuni ya Rites Consortium ya India uliounda Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), ili hatua nyingine za utendaji ziendelee.

  Akizungumza na watumishi wa Wizara ya Uchukuzi, Dar es Salaam ikiwa ni mfululizo wa ziara zake kutembelea wizara mbalimbali, Rais Kikwete amesema, amefarijika na utendaji kazi wa wizara hiyo, lakini bado kasi zaidi inahitajika ikiwa ni pamoja na ya kusitisha mkataba wa Rites.

  "Nimefarijika na utendaji wenu, ziara hii inalenga kujifunza na kuona yale tulioelezana awali kama mmeyafanyia kazi kwa kiasi gani, lengo ni kuwatumikia Watanzania….hili la Rites kasi ya kuachana nao muiongeze…iongezeke," amesema Rais Kikwete leo.

  Serikali iliingia mkataba Rites mwaka 2006 ambao ulisababisha kuvunjwa kwa Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kuunda TRL ambapo mbia huyo ana asilimia 51 huku Serikali ikiwa na uwekezaji wa asilimia 49.

  Mgogoro wa kutaka kuvunjwa kwa mkataba huo wa miaka 25, uliibuliwa na wafanyakazi wa TRL na kushika kasi mwishoni mwa mwaka 2009 baada ya Rites kushindwa kuwalipa wafanyakazi mishahara, lakini juhudi kadhaa zilichukuliwa na Serikali hadi hivi sasa inaposubiriwa kuvunjwa rasmi mkataba huo.

  Rais aliitaka wizara hiyo kuhakikisha kuwa inakomesha na kumaliza kero zinazochangia kuwepo kwa migomo na migogoro ya mara kwa mara baina ya wafanyakazi wa reli na menejimenti zao kama ilivyokuwa TRL na Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) kwa kuwa hali hiyo inarudisha nyuma ufanisi.

  Alisema, hataki kusikia tena hadithi ya migomo kwa kuwa sasa imekwisha na kuitaka Wizara kuangalia namna viongozi katika ngazi ya menejimenti wanavyochaguliwa kwani wengi wao wanakuwa ni makada wa vyama badala ya watendaji wenye ujuzi katika utawala na biashara.

  Akijibu hotuba ya Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu kuhusu tatizo la kimfumo linavyochangia mgogoro wa kiutendaji Tazara, Rais alisema, "Tatizo sidhani kuwa ni mfumo, unaweza kuwa na mfumo mzuri lakini watu wabaya, sisi ndiyo tuna shida, badala ya kuchagua wenye uwezo, tunachagua makada."

  Alisisitiza wizara ifikirie kwa makini suala la kuwaachisha kazi wafanyakazi wa Reli na kisha watu hao hao wanataka kuajiriwa tena na kutaka kitu cha kwanza kuwa maslahi ya Taifa mbele.

  Kuhusu Sumatra, awali Rais alihoji inapandishaje nauli, na alipewa mchanganuo na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Israel Sekirasa kuwa mamlaka ya kupanga nauli imepewa ngazi za mikoa, lakini alidai kuna mgongano wa kimaslahi unaotokana na baadhi ya maofisa wa polisi kumiliki daladala na magari ya abiria.

  "Kuna shida kubwa Mheshimiwa Rais, baadhi ya maofisa wa polisi ndiyo wamiliki wa vyombo vya usafiri vya abiria, hivyo hata vikikosea havikamatwi na ikitokea, vinaachiwa bila hatua yoyote," alidai Sekirasa.

  Kwa upande wake, Rais alicheka na kusema, "Ya leo kali" maneno yaliyosababisha hadhira yote kuangua kicheko.

  Katika hatua nyingine, Rais Kikwete aliitaka wizara iharakishe ujenzi wa Reli ya Kati na kubainisha namna ambavyo Serikali itahusika katika ujenzi kama ni kushirikiana na wawekezaji, kukopeshwa au sekta binafsi kujenga na kushirikiana kiuendesha.

  Masuala mengine ambayo Rais aliitaka wizara kuyafanyia kazi baada ya hotuba ya Nundu, ni pamoja na kuboresha Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), kuondoa msongamano bandarini kwa mizigo kutokaa zaidi ya siku tano.

  Nundu katika hotuba yake pamoja na mambo mengine, alisema wana mpango wa kuanza kutumia treni kusafirisha abiria katika Jiji la Dar es Salaam katika kipindi cha miezi saba ijayo ikiwa zitapatikana Sh bilioni 4.7.
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hii ni kupongezwa sana. Hawa jamaa wanastahili adhabu kali kwa utapeli wao na kuirudisha nyuma sekta ya usafiri wa reli. Lakini hili linapaswa kuwa funzo kwa viongozi wetu ili lisitokee tena huko mbele ya safari!
   
 3. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kama mpaka leo zaidi ya miaka sita akiwa madarakani Rais bado anajifunza! Lini atafanya kazi aliyowaahidi Watanzania? Ama ndiyo ile bora liende siku ziishe aondoke!!!!
   
 4. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ni lini watanzania tutajifunza kuacha kufanyia siasa masuala yenye maslahi makubwa kwa taifa. Tuchukue hili suala la Rites,sasa ni zaidi ya miaka miwili tangu serikali itoe tamko kwamba ilikuwa imefikia uamuzi wa kuvuja mkataba wake na Rites; katika hali hiyo agizo la rais la hivi sasa linazua maswali mawili; kwanza ni je, hayo matamko ya serikali yanayotolewa mara kwa mara na mawaziri wake, rais anakuwa ana habari nayo? Na pili, kimsingi waziri ni mshauri wa rais, na hivyo katika hali halisi hoja zinapashwa ziibuliwe katika ngazi ya wizara na kupelekwa kwa rais. lakini kwa mtindo huu wa kutoa maagizo kwenye mkutano wa hadhara inakuwa kinyume chake, swali ni je katika hali hiyo kuna umuimu wowote wa kuwa na msululuwa mawizara?
   
 5. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Huyu Rais huyu was he not aware wakati Serikali inaingia mkataba na RITES??? Didn't he see all this coming?? For gods sake mnaingia mkataba wa miaka 25 na kampuni ambayo haiwezi kulipa watu mishahara, ahaaaaaa this country!!!!
   
 6. m

  muajemi Member

  #6
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  safiiiiiii
   
 7. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Naona kama JK anaweza ila pengine hajaamua tuu.
   
 8. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #8
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,401
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  uamuzi mzuri kwani sijaona wananchofanya hawa Rites zaidi ya kutufanya tuzidi kuwa maskini
   
 9. Mapi

  Mapi JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 6,871
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  Am afraid tz ishauzwa...mkataba miaka 25 bla kuifaham kampun vzur!! Haya n maslah ya taifa au 2mbo za wachache?
  Rais anatamka kwenye hadhara kuamuru mkataba uvunjwe as if hajui madhara ya kuvunja mkataba, kama vle hajui klchotupata from dowans na majnamiz mengne yanayotutafuna taratbu ambayo yeye na serkal yake walyazalsha na kuyalea.
  Tanzania tuamke..,tumelala ucngz wa pono...hata wanaojarbu kutuamsha walau kwa kutuchoma vjcndano hatushtuki,
   
 10. Mapi

  Mapi JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 6,871
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  Am afraid tz ishauzwa...mkataba miaka 25 bla kuifaham kampun vzur!! Haya n maslah ya taifa au 2mbo za wachache?
  Rais anatamka kwenye hadhara kuamuru mkataba uvunjwe as if hajui madhara ya kuvunja mkataba, kama vle hajui klchotupata from dowans na majnamiz mengne yanayotutafuna taratbu ambayo yeye na serkal yake walyazalsha na kuyalea.
  Tanzania tuamke..,tumelala ucngz wa pono...hata wanaojarbu kutuamsha walau kwa kutuchoma vjcndano hatushtuki,
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Yaani siku zote haujavunjwa tu? watumishi wake wanamfahamu alivyo mzee wa maneno tu usishangae ikifika mwaka kesho haujavunjwa!
   
Loading...