Kikwete aagiza misafara yake ya kwenda nje kupunguzwa

mshahara wake unaujua ni shing ngapi mkuu?nchi pekee duniani ambapo mshahara wa rais is classified...the matter of national security,foolish country,.stupid citizens

Aiseee kama Director wa Tanapa anakula 20m na NHC anakula 23m na Gavana anakula USD25k basi huyu jamaa atakua anacheza kwenye 30-50m je tukipangua 40% makato yani 12m mpaka 20m mpaka ziishe zote
 
Watanzania bwana, maana ya kulalamika safari zake zimezidi ilikuwa nini kama siyo kuzipunguza, kasema zipungue unaanza kujiuliza maswali. Kumbe ulikuwa unalalamikia tatizo ambalo hujui suluhisho lake?. Na hili ndilo tatizo letu. Unatakiwa unapoona tatizo , toa na mapendekezo nini kifanyike kumaliza tatizo. Sasa haya ndiyo madhara ya kulalamika bila kupendekeza suluhisho. Rais kaona kama safari zake ni kero basi zipungue badala ya kutoa comments juu ya hatua zilizochukuliwa unaanza kujiuliza, maana yake unalalamika tena kwa nini ameamua kuzipunguza siyo. Hatutaki watu wa aina hyo humu JF . Una upeo mdogo wa kuelewa, "acha kuchangia mada"
au ulitaka Rais aseme ziongezwe mara dufu ili ulalamike zaidi manake inaonekana wewe kulalamika ndiyo furaha yako na ni sehemu ya maisha yako na watu watashindwa kukuelewa unafanya hivyo kwa faida ya nani. Tusipo angalia wanasiasa wataliangamiza taifa hili kwa sababu , wale tunaojiita great thinkers sasa tumebadilishwa kuwa daraja la kukebehi kila jema lifanywalo na serikali ili wanasiasa wengine wapate umaarufu. Hiyo dhambi haitaishia hapo akija mwingine kama kiongozo tutaendelea na kuzunguka kwenye duara ili naye aonekane na serikali yake hawafai.

masaburi at work.unanufaika na hizo safari na misafara yake.nikuulize wewe mshauri wake haya hamkuyajua miaka yote?ni kweli mnamaanisha au ndo usanii?ushauri nyie si ndiyo mnatoa coz kama wananchi toka wameanza kulalamikia hili jambo limechukua aka 6 au comments za richard ndo zimefanyakazi?
 
Tatizo huyu jamaa huwa anagundua kasoro zake too late. Alishindwa nini kutamka haya miaka mitano iliyopita?

Kwani wakimpagia akakataa watamlazimisha mbona anataka kuwasingizia waratibu wake, halafu huyu jamaa kweli msanii anataka kujifanya pilato kwa kunawa mikono
 
katika magazeti ya leo kuna habari inayosema kikwete aagiza wanaoratibu misafara yake kwenda nje ya nchi kupunguzwa.
Mytake
1. Hivi ni kweli alikuwa ajui kuwa misafara yake ni mikubwa?
2. Kilio cha wananchi kimekuwa yeye kusafiri mara kwa mara nje ya nchi
3. Je kwa hilo agizo lake litakuwa mwarobaini kwa kilio cha wananchi?

Mkweree anakumbuka shuka wakati kumekucha!! Amekwisha ifilisi hazina ndio anataka misafara yake ipunguzwe!!
 
anatakiwa asiende kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! sio kupunguza hamna faida yoyote tunayopata zaidi ya kutumia tu pesa za walipa kodi!
 
watanzania ni watu wa ajabu sana rais kasikia kilio chenu mnataka nini nyie. meomba katiba mchakato unaendelea, mmeomba kukutana naye amewakubalia, jamani ee e e e e e e ee e e e

Hata mimi nawashangaa badala ya kumpongeza kwa hatua hiyo mnaendelea kulalamika
 
hata hiyo BBC na NY Times hayasomi kabisa bcs angepata japo habari za kimataifa kidogo tatizo huwa anaangalia wakina 50cents tuu, yeye ni music na movies tuuu!
Na Ze-Comedy, jamani apunguze na safari pia sio ukubwa wa msafara wake.
 
sad to say, is it not 'better late than never'? He deserves more prayers than criticism
 
katika magazeti ya leo kuna habari inayosema kikwete aagiza wanaoratibu misafara yake kwenda nje ya nchi kupunguzwa.
Mytake
1. Hivi ni kweli alikuwa ajui kuwa misafara yake ni mikubwa?
2. Kilio cha wananchi kimekuwa yeye kusafiri mara kwa mara nje ya nchi
3. Je kwa hilo agizo lake litakuwa mwarobaini kwa kilio cha wananchi?

Kwa hiyo kimsingi idadi ya safari za nje inaweza ikabaki palepale au hata kuongezeka ila waratibu ndiyo watakaopunguzwa.
 
Mkweree anakumbuka shuka wakati kumekucha!! Amekwisha ifilisi hazina ndio anataka misafara yake ipunguzwe!!

Mkuu hujaelewa thread. Kwa mujibu wa mtoa hoja kinachopunguzwa siyo misafara bali ni waratibu wa misafara. Misafara inaweza kabisa kubaki ileile au hata kuongezeka.
 
Watanzania bwana, maana ya kulalamika safari zake zimezidi ilikuwa nini kama siyo kuzipunguza, kasema zipungue unaanza kujiuliza maswali. Kumbe ulikuwa unalalamikia tatizo ambalo hujui suluhisho lake?. Na hili ndilo tatizo letu. Unatakiwa unapoona tatizo , toa na mapendekezo nini kifanyike kumaliza tatizo. Sasa haya ndiyo madhara ya kulalamika bila kupendekeza suluhisho. Rais kaona kama safari zake ni kero basi zipungue badala ya kutoa comments juu ya hatua zilizochukuliwa unaanza kujiuliza, maana yake unalalamika tena kwa nini ameamua kuzipunguza siyo. Hatutaki watu wa aina hyo humu JF . Una upeo mdogo wa kuelewa, "acha kuchangia mada"
au ulitaka Rais aseme ziongezwe mara dufu ili ulalamike zaidi manake inaonekana wewe kulalamika ndiyo furaha yako na ni sehemu ya maisha yako na watu watashindwa kukuelewa unafanya hivyo kwa faida ya nani. Tusipo angalia wanasiasa wataliangamiza taifa hili kwa sababu , wale tunaojiita great thinkers sasa tumebadilishwa kuwa daraja la kukebehi kila jema lifanywalo na serikali ili wanasiasa wengine wapate umaarufu. Hiyo dhambi haitaishia hapo akija mwingine kama kiongozo tutaendelea na kuzunguka kwenye duara ili naye aonekane na serikali yake hawafai.

Sasa we kilaza hujioni kuwa wewe ndiye ulodandia mada bila kuielewa kwa kuendekeza ushabiki wa kipumbavu kabisa. Thread inazungumzia juu ya kupungua kwa idadi ya watu ktk misafara ya nje ya rais na siyo kupunguzwa kwa misafara kilaza wewe.

Unakuwa na akili kama wabunge wa ccm why? Ulivyo mbwiga ati povu lakutoka mdomoni kumwita mwenzio anaupeo mdogo, kweli nimeamini nyani haoni kundule.
 
JF NA UKOSOAJI MCHUNGU ULIOTUKUKA: RAIS KIKWETE SASA APATA DIRA MPYA KUTUPUNGUZIA MZIGO WA SAFARI ZA NJE WALIPAKODI WA TANZANIA KUFUATIA MICHARAZO BILA HURUMA YA MTANDAO HUU

MhRais Kkikwete,

Nakushukuru sana katika hili la kusoma sehemu ya ukosoaji wetu hapa JF na hatimaye kuona mantiki ya kupunguza idadi ya watu unaosafiri nao kwenda nchi za nje.

Hadi hapa naomba naye mama yetu, Mchungaji Mama Lwakatare, aliyekaririwa majuzi kutamani kuona mtandao wetu huu wa JF ikifungwa atambue kwamba hata na sisi huku TUNAFAIDI KWA WATANZANIA tena kuliko hata uwakilishi wao bungeni huku sisi tukiwa hatulipwi mshahara na mtu yeyote wala hizo posho wanazozigombania hivi sasa huko mjengoni Domz.

Nasema mama yetu huyu naye sasa aone jinsi gani Rais Kikwete anavyotumia mtandao huu wa JF kurekebisha mambo hata kule ndani mwake Magogoni.

Ni majuzi tu hapa tumemtifua kweli kweli RaisKikwete juu ya safari zake nje ya nchi na tukahoji tupewe mchanganuo wa faida na tija tulizozipata kutokana na safari zake hizo tangu aingie madarakani ikilinganishwa na thamani ya gharama tulizozitumia kama walipa kodi kufadhili safari hizo.

Isitoshe, tulikwenda mbali kidogo kwa kutahadharisha ya kwamba walipakodi wa nchi hii tusije tukajikuta
tukifika mahali sawa na KUUZA ZIZI ZIMA LA NG'OMBE WETU WA PEKEE KUTUMIKA KUFADHILI SAFARI ZA RAIS NA JOPO LAKE KUBWA AMBALO MWISHO WA SIKU TUNAJIKUTA IKITULETEA FAIDA YENYE THAMANI YA YAI LA KUKU. This was a very candid and bitter criticism on President Kikwete BUT with a bottomline of AGGITATING FOR A CHANGE FOR THE BETTER.

Hadi hapa nimefarijika kugundua kwamba kumbe Mkulu hata ulivyo huko Davos kumbe bado uliweza kujipatia japo kijinafasi (kama mwana JF mwenzetu Prof Mwandosia alipokua matibabuni India) walau kuchungulia humu na kukutana na jinsi nilivyokukosoa kwa HASIRA ZOTE na wala haujachukulia chuki badala yake umeamua kuchukua hatua kurekebisha mambo.

Kimsingi Rais wetu, kama ulikua hujui, ujue leo kwamba hatufurahishwi hata chembe na uvujishaji wa kodi zetu bila kutuletea tija ya kuonekana. Madaktari wanatiji kubwa kwetu; kawaboreshee malipo yao, wabunge hasa wa CCM ni mzigo kwetu kwa tabia yao ya kugeuka muhuri wako kupitisha kila uchafu serikalini; kawapokonye posho zote, rekebisha mfumo wa mishahara na marupurupu kitaifa kuleta uwiano na kulinda morali ya watumishi wetu wa serikali

Jamii isiokua na kundi lenye kujenga mawazo tofauti yenye kukosoa kwa nia ya kujinga ni sawa na jamii iliokufa. Mimi ni mwananchi wako mkereka na mambo mengi ya hovyo pamoja na ufisadi serikalini na mkosoaji wako mwaminifui nisiyekuonea haya hata kidogo katia jambo lolote lile lenye kubeba MASLAHI MAPANA YA UMMA.

Hivyo, katika hatua yako hii ya kuwazia kutupunguzia mzigo wa safri za nje, nasema asante kwa kupokea ukosoaji wangu mchungu sana na kuligeuza kuwa ni sehemu ya ratiba yako kuturekebishia mambo.

Endelea kutarajia mashambulizi zaidi kwako na kwa serikali yako toka kwangu endapo kuna mahala mambo wala si mambo, na ninakutakia safari njema nyumbani uje ukamalize ubishi wa posho za wabunge kwa kuendana na matarajio ya umma na ukawalipe zaidi madaktari wetu.

Mwananchi Wako,

UWEZO TUNAO

Back
Top Bottom