Kikwete aacha deni la sh. milioni 53.6 za wasanii Ikulu

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Ikulu imeahidi kufanyia kazi mdai ya Chama cha Wasanii Wachoraji Tanzania(CHAWATA), ambayo waliyawasilisha jana, ikilalamikiwa ofisi hiyo katika awamu ya nne iliyokuwa chini ya Raisi Jakaya Kikwete, kuwachelewa malipo yao ya shilingi Milioni 53.6

Chanzo: Nipashe
 
Nani alikuwa mtendaji wake mkuu wakati wa utawala wake? Kama hili lina ukweli huyo jamaa atumbuliwe kwani jipu lililoiva.
 
Nipashe hili gazeti la wachaga wanahasira sana na jk lakini ndiyo kafanya kazi yake kamaliza kwa heshima kubwa pole yako wewe unayeamini nipashe.
Naunga mkono hoja yako wachaga wana hasira na ccm wameiadhibu majimbo yote saba ya uchagani yameenda Ukawa. Ila wale kina Davis Mosha ni wakwele? Na mnasubili nini kufunga ofisi zote za ccm uchagani? Hii ndio kazi aliyowasifu mkwele kwamba mlikibeba chama? Insanity.
 
Nipashe hili gazeti la wachaga wanahasira sana na jk lakini ndiyo kafanya kazi yake kamaliza kwa heshima kubwa pole yako wewe unayeamini nipashe.
Mkuu salama? Mwaka jana kama sikosei, Feb au Mar uliwahi kutuletea uzi fulani kuwa Tanesco ilikuwa inajiandaa kupunguza gharama za umeme kwa kiasi kikubwa na kuwa tungepata neema kubwa sana na hiyo ulisema ni kutokana na gesi ya Mtwara, mbona kimya tu hadi leo? Upo uzi humu JF, wazoefu wanaweza kuutafuta. Kama si wewe samahani sana, atakuwa ni kada mwenzako
 
Nipashe hili gazeti la wachaga wanahasira sana na jk lakini ndiyo kafanya kazi yake kamaliza kwa heshima kubwa pole yako wewe unayeamini nipashe.
... 'kaimu mkurugenzi wa mawasiliano ya rais ikulu, Greyson Msigwa, alithibitisha kuwapo na madai hayo na kuliambia Nipashe yatafanyiwa kazi ndani ya wiki moja. Naye Katibu wa chama cha wasanii alisema' tuliuza kazi zetu ikulu kwa makubaluano ya kulipwa tangu August mwaka jana, hadi leo hatujaweza kupatiwa pesa zetu.
 
Mwenye A/c ya bank ya ikulu tafadhali aiweke hapa nilipe hilo deni!!
 
Nipashe hili gazeti la wachaga wanahasira sana na jk lakini ndiyo kafanya kazi yake kamaliza kwa heshima kubwa pole yako wewe unayeamini nipashe.

Yaani kwa CCM heshima kubwa ni kulea ule wizi wa Bandarini,TRA,ESCROW,RICHMOND,MEREMETA,DEEP GREEN,KIVUKO KIBOVU,MALIPO HEWA YA WAKANDARASI?

No wonder Ukiwa CCM ni zaidi ya shetani
 
Nipashe hili gazeti la wachaga wanahasira sana na jk lakini ndiyo kafanya kazi yake kamaliza kwa heshima kubwa pole yako wewe unayeamini nipashe.
Kuna watu mnaona fahari kuonyesha hadharani ujinga badala ya hekima. Unaposema Wachaga wanahasira na JK unamaanisha nini? Au Nipashe ni gazeti la wachaga unamaanisha nini? Hivi hujui kuwa pamoja na kushindwa majimbo mengi ya uchaguzi Kilimanjaro, CCM kule ni chama imara kuliko huko Dodoma,Katavi na kwingineko mnakoita ngome zenu?
Acheni ubaguzi unaotokana na fikra za kimaskini mlizo nazo, wamchukie JK ili iweje? aache kuchukiwa na watu wake wa Bagamoyo alioacha kuwafundisha kutafuta maendeleo zaidi ya kumwachia mwanae Ubunge?
 
... 'kaimu mkurugenzi wa mawasiliano ya rais ikulu, Greyson Msigwa, alithibitisha kuwapo na madai hayo na kuliambia Nipashe yatafanyiwa kazi ndani ya wiki moja. Naye Katibu wa chama cha wasanii alisema' tuliuza kazi zetu ikulu kwa makubaluano ya kulipwa tangu August mwaka jana, hadi leo hatujaweza kupatiwa pesa zetu.
Kumbe Ikulu nayo inadhulumu kazi za wasanii!
 
Back
Top Bottom