Kikwazo cha ufumbuzi wa mgogoro wa Zanzibar nini hasa?

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
1,789
Mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar unawaumiza vichwa watu kwa vile ufumbuzi wake umekuwa kitendawili. Tena kitendawili tega mfumbuzi afumbue, na mfumbuzi akishindwa basi hupewa mji wa mbali kwa alieweka kitendawili kutembelea na hatimae kitendawili hukiteguwa.

Kitendawili cha Zanzibar hakihitaji mtu kupewa mji kuteguliwa. Tukijuuuliza tu kwa nini wagombea wote wawili wamekuwa wagumu kuregeza misimamo yao ya kisiasa? Ni kwa sababu ya maslahi? hili linawezekana kutokana mitizamo mitatu tofauti lakini inayolingana

  1. mikataba ya kisheria (MoU) waliokubaliana kuhusu uchimbaji wa mafuta n a makampuni makubwa yenye ushawishi duniani yumkini ndio unaowavuruga wanasiasa hawa.
  2. Nchi nyengine kubwa duniani ambazo zinakodolea macho mikataba kama hiyo na kuona ufinyu wao kupata au kufikiriwa kushiriki katika mchkato huo nao wametia mikono yao. Ikumbukwe kuwa utafutaji wa mafuta na kuthibitishwa kuwepo umeshafanywa na serikali ya kikoloni ya kingereza kupitia BP Shell kwenye miaka ya 50 na viashiria hivyo kuwekewa "beacon" sehemu tofauti visiwani. Katika kitabu cha ramani"atlas" ya Zanzibar iliokuwa inasom eshwa mashule mwanzoni wa miaka ya 60, beacons hizo ziliitwa "oil reserve"
  3. mtizamo wa tatu ambao unaonekana una nguvu zaidi ni ule ulioweza kuharakisha kuliondoa kinyemela bila ya kufuata katiba suala la mafuta kuwa jambo la muungano. Hili limefanyika baada ya kuonekana kuwa kusubiri katiba mpya kutachukua muda mrefu au uwezekano wa kukwama.
Ni dhairi kuwa mbadiliko wa uongozi utaathiri sana mitazamo hiyo na hivyo ni status quo tu. MAPINDUZI DAIMA

Nami nasema Zanzibar ni zaidi ya mafuta na gesi
 
Tatizo la wenzetu hawa huwa hawasemi ukweli kuhusu kiini cha kutoelewana baina ya wakazi/raia ambao asili zao ni tofauti, hapa watasema visingizio chungu mzima hata masuala ya mafuta ni kiini macho tu - mimi naona tatizo kubwa la Visiwani limejikita zaidi kwenye masuala ya ubaguzi tu baina waswahili na raia wenye asili ya Oman au Yemen,suala hili liko embeded kweli kweli kwenye mawazo/akili za baadhi ya raia na wanamapinduzi - hao uwambii kitu - wako radhi tukose misaada, tutengwe na International community - Taifa letu lidhalilike kwa kuendekeza matakwa ya watu wachache wasiopenda kubadirika!

Tusipokuwa makini heshima aliyo kuwa anajijengea Dk.Magufuli kamataifa itakwenda na maji kutokana na masuala/matatizo ya Zanzibar ya mara kwa mara, inakuwaje kila zinapo pigwa kura za kuchagua Urais huko Zanzibar lazima patokee mushkeli miaka nenda rudi - wana end up kwa malidhiano - sasa kama mambo yenyewe ndio haya kulikuwa na haja gani ya kupiga kura in the first place!
 
sifikirii kuwa hiyo ni sababu kuu. watu wengi waliokuwa na asili ya nchi hizo wamejikusanya kwenye jimbo moa kuu nal ni mji mkongwe. Lakini CCM imepoteza viti tisa(9) Unguja ambayo inakaliwa na waasisi (wahadimu) wa Zanzibar.

Tatizo ni maslahi napressure inayopatakutoka kwa wakubwa
 
Kwani hii zaba ya mfumo wa vyama vingi zanzibar ipo na je inakubalika? Kwa wale wanaozunguka sanaa kutafuta suluhisho la zanzibar .simple warudi katikatika dhana ya demokrasia ya vyama vingi nini kusudio la vyama vyingi .kwanini watu wanazunguka sana
 
sifikirii kuwa hiyo ni sababu kuu. watu wengi waliokuwa na asili ya nchi hizo wamejikusanya kwenye jimbo moa kuu nal ni mji mkongwe. Lakini CCM imepoteza viti tisa(9) Unguja ambayo inakaliwa na waasisi (wahadimu) wa Zanzibar.

Tatizo ni maslahi napressure inayopatakutoka kwa wakubwa
Mkuu mimi nilikuwa nazungumzia zaidi yanapo kuja masuala ya nini kifanyike kumaliza migogoro hisiyo la lazima linapokuja saula la kutangaza nani kahibuka mshindi katika kinyanganyilo cha URASI. Tangu kuruhusiwa kwa vyama vya upinzani Nchini - Zanzibar huwa ina kawaida yakuwa na kigugumizi linapo kuja suala la kutangaza Mshindi - mara zote wanavutana mwisho wa siku utawasikia wanasema wamefikia maridhiano - Demokrasia gani inaendeshwa kwa maridhiano, kama vipi Wazanzibari wasiwe wanapig kura za kuchagua RAIS wao basi.
 
Last edited:
Tatizo liliopo Zanzibar ni tatizo ambalo lipo katika nchi nyingi za ki Africa, ni kutokubaliana na ukweli kuwa kila kitu kina mwisho, ipo siku hamtokuwa nyinyi tena, watu watataka mabadiliko.
 
Mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar unawaumiza vichwa watu kwa vile ufumbuzi wake umekuwa kitendawili. Tena kitendawili tega mfumbuzi afumbue, na mfumbuzi akishindwa basi hupewa mji wa mbali kwa alieweka kitendawili kutembelea na hatimae kitendawili hukiteguwa.

Kitendawili cha Zanzibar hakihitaji mtu kupewa mji kuteguliwa. Tukijuuuliza tu kwa nini wagombea wote wawili wamekuwa wagumu kuregeza misimamo yao ya kisiasa? Ni kwa sababu ya maslahi? hili linawezekana kutokana mitizamo mitatu tofauti lakini inayolingana

  1. mikataba ya kisheria (MoU) waliokubaliana kuhusu uchimbaji wa mafuta n a makampuni makubwa yenye ushawishi duniani yumkini ndio unaowavuruga wanasiasa hawa.
  2. Nchi nyengine kubwa duniani ambazo zinakodolea macho mikataba kama hiyo na kuona ufinyu wao kupata au kufikiriwa kushiriki katika mchkato huo nao wametia mikono yao. Ikumbukwe kuwa utafutaji wa mafuta na kuthibitishwa kuwepo umeshafanywa na serikali ya kikoloni ya kingereza kupitia BP Shell kwenye miaka ya 50 na viashiria hivyo kuwekewa "beacon" sehemu tofauti visiwani. Katika kitabu cha ramani"atlas" ya Zanzibar iliokuwa inasom eshwa mashule mwanzoni wa miaka ya 60, beacons hizo ziliitwa "oil reserve"
  3. mtizamo wa tatu ambao unaonekana una nguvu zaidi ni ule ulioweza kuharakisha kuliondoa kinyemela bila ya kufuata katiba suala la mafuta kuwa jambo la muungano. Hili limefanyika baada ya kuonekana kuwa kusubiri katiba mpya kutachukua muda mrefu au uwezekano wa kukwama.
Ni dhairi kuwa mbadiliko wa uongozi utaathiri sana mitazamo hiyo na hivyo ni status quo tu. MAPINDUZI DAIMA

Nami nasema Zanzibar ni zaidi ya mafuta na gesi
Tatizo la Zanzibar ni la wazanzibari wenyewe.
Wasitegemee mtu toka nje awategulie vitendawili walivyoviunda wenyewe huku wakijijua wanafanya makosa.

Zanzibar ni Nchi ati!
Kwa umoja wenu wote CF na CCM Zanzibar mlitengeneza katiba iliyoitenga Bara, sasa mlijishonea kanzu hamna budi kuivaa msitirike, au la mtembee uchi mje Magogoni kuomba nguo.
 
Back
Top Bottom