Kikundi kipya kilichoundwa na Iran huko Iraq chaapa kuikomboa Milima ya Golan ya Syria

Samson Ngomboli

JF-Expert Member
Oct 30, 2019
763
1,000
😂😂😂😂hadithi za abunuwasi za kujifariji moyo,kama mataifa matano na sapoti ya mataifa kibao walishindwa kuifuta Israel ikiwa changa,sembuse hivyo vikundi vya kihuni,endeleeni kujidanganya,Israel ipo hapo Hadi ukamilifu wa nyakati.
MUNGU IBARIKI ISRAEL,MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 

profesawaaganojipya

JF-Expert Member
Apr 21, 2015
618
1,000
Ha ha ha h ha pia mkumbuke makundi yanayoundwa na iran si mchezo kama mtakumbuka israel walipewa kipigo na hezbullah mpaka marekan ikaogopa kuingilia kati hezbullah walivyokuwa washez wakakomboa miji yote iliyotekwa ha ha ha pia wakafanikiwa kuteka kijiji kimoja ndani ya israel
dah,ila mahaba niue ni hatari sana..
 

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
14,319
2,000
Kikundi kipya kilichoundwa na Iran huko Iraq chaapa kuikomboa Milima ya Golan ya Syria inayokaliwa kimabavu na Israel

Ama kweli mbombo ngafuiran na hamas mpya ndani ya Iraq na Syria daaah wazayuni kazi wanayo

Lebanon kuna Hezbollah

Gaza kuna Hamas

Yemen kuna Answarullah

Haya Syria na iraq kuna kikundi chengine

Na vyote hivi vitapambana na Israel

Nimeamini ule msemo wa Israel haitokuwepo miaka 25 ijayo.

Yajayo yanafurahisha.

Nujabaa ya Iraq: Tuko tayari kuikomboa Miinuko ya Golan ya Syria

Msemaji wa Harakati ya Muqawama ya Iraq ya al-Nujabaa ambayo ni sehemu ya harakati ya wananchi ya Hashdu sh-Sha'abi ya nchi hiyo ametangaza utayarifu wa harakati yake kwa ajili ya kuikomboa Miinuko ya Golan ya Syria.

Nasr al-Shammari amesema hayo katika mahojiano na tovuti ya habari ya al-Ahad yenye makao yake Lebanon na kusisitiza kuwa, harakati hiyo ya kupambana na magenge ya kigaidi imejiandaa kikamilifu kuikomboa Golan inayokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel, na kwamba utawala huo uko katika ncha ya kuporomoka.

Ameashiria namna harakati hiyo ilivyounda Brigedi ya Ukombozi wa Golan mwaka 2017 na kueleleza bayana kuwa, "licha ya harakati ya al-Nujabaa kuwa amilifu katika vita dhidi ya magenge ya kitakfiri nchini Syria, lakini Brigedi hii iliundwa makhsusi kwa ajili ya kupambana na utawala wa Kizayuni, na hilo litasalia kuwa hivyo."

Msemaji wa harakati ya al-Nujabaa ya Iraq amebainisha kuwa, baada ya kambi ya muqawama kupata ushindi mkubwa katika Operesheni ya Panga la Quds huko Gaza hivi karibuni, vita vijavyo vitapenya ndani zaidi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni maghasibu, katika maeneo yanayozungukwa na Mto Nile na Furati (Euphrates).

Askari na bendera ya Syria katika Miinuko ya Golan

Ikumbukwe kuwa, mwaka 1967, utawala wa Kizayuni wa Israel uliteka karibu kilomita 1200 za ardhi ya Syria katika Milima ya Golan na baada ya kupita muda uliyaingiza maeneo hayo katika ardhi nyingine zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni na kupachikwa jina la Israel.

Jamii ya kimataifa daima inasisitiza kuwa Milima ya Golan ya Syria itaendelea milele kuwa milki ya nchi hiyo ya Kiarabu. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia limetoa maazimio kadhaa ya kuthibitisha kuwa utawala wa Kizayuni unaikalia kwa mabavu miinuko hiyo.

Tags
 

Kosugi

JF-Expert Member
Sep 2, 2019
2,657
2,000
Myahudi akitoa kpgo mnadai marekani kasaidia wakati huohuo mnadai Iran anampiga marekani na Hezbollah anamuweza myahudi sa kwann hao Iran na Hezbollah wasiungane wawapge hao Israel na marekani ukizngatia Wana backup ya urusi au nn kinasubiriwa hapo myahudi kuondoshwa hapo middle East
MKUU ISRAEL ANA BACKUP YA KARIBIA MATAIFA YOTE YA ULAYA NA USA.
ILHALI IRAN ANA BACKUP YA SILAHA TU KUTOKA URUSI.
NA URUSI HAWEZ KUJIINGIZA KIMAZIMA KM NATO WATAKAVYOJIINGIZA KUMSAIDIA ISRAEL.
KAA UKIJUA HILO.
 

Swet-R

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
4,459
2,000
1973 Cuba ilikuwa taifa la kwanza kupeleka makomandoo wake elfu tano mabingwa wa vifaru kuikomboa milima ya golan, yaani walifyekwa wote na hakuna hata mmoja aliyerudi hai wala makaburi yao kuonekana.leo unaniambia eti wanamgambo wa IRAN wataikomboa Golan, hicho ni kichekesho cha maiti kucheza disco! kumbuka kwamba kila vita ipiganapwo Israel na mwarabu, umoja wa mataifa unazuia baadhi ya siraha kali za israel zisitumike. mkimchokoza sana ipo siku mpaka wa israel na na africa utakuwa pale uganda kwa kusini na kaskazini Ugiriki!!!
Ahahaaaaa....mpaka utakuwa uganda kusini na kaskazini ugiriki
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom