Kikosi, Kikundi - Wataakamu wa jeshi karibu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikosi, Kikundi - Wataakamu wa jeshi karibu!

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Kipala, Jul 8, 2009.

 1. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Salaam wenzangu hasa wataalamu wa habari za kijeshi. Naomba msaada kuhusu maneno kwa ajili ya vitengo ya kijeshi.

  Kiingereza: Company, battalion, regiment, brigade, division, corps, army

  Nasikia kwa Kiswahili ni company= kikosi, battalion = kikundi. Nauliza je: inaeleweka?
  Maana kwa kugha ya kawaida wala kikosi wala kikundi ni idadi maalumu.
  Lakini kwa lugha cha kijeshi "company" inaeleweka ni takriban watu 80-200, na battalion ni jumla ya company 2-7 yaani watu 500-1500.
   
 2. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Na mimi naomba niongezee msemo ulioibuka hivi karibuni baada ya maafa ya Mbagala. Nini maana ya msemo "kusafisha kambi" ?
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  knowledge ndogo niliyoipata wakti nikipita JKT kwa mujibu wa sharia, Nikiwa kambi ya Ruvu chini a Afande Meena wakti huo CO na capt Othman kamanda wangu wa A coy, walitufundisha kama ifuatavyo:

  Company: hiki ni kikundi cha askari kinachoundwa na platuni tatu chini ya platuni kamanda. Sasa Company maana yake ni Kombania kwa kiswahili.

  battalion: hii maana yake ni kikosi chini ya mkuu wa kikosi ambeye ni CO. battarion inaundwa na kombania tano au sita. Mfano ruvu tulikuwa na kombania a mpaka f kisha kulikuwa na HQ coy. Hivi viliunda kikosi cha Ruvu JKT.

  regiment: hiki ni mikundi cha askari ( yaani wale wasio maofisa) katika kikosi. Nacho kinakuwa chini ya RSM ( Regiment surgin major)

  Brigade: hii ni muungano wa vikosi katika kanda fulani na vinaongozwa na brigade commander.

  Division: hii ni muungano wa vikosi vyenye kazi sawa. kama JKT vikosi vyote vikiungana wanafanya Division ya JKT nayo inaongozwa na Division kamanda, enzi zetu alikuwa Meja Gen Makame Rashid. Sijui Yupo wapi mtu huyu maana ake alikua mpenzi mkubwa saa wa taarab na ndie aliyeanzisha kikundicha JKT Taarabu chini ya Issa matona, Bia Hassan, Shakira Said n.k.


  Dr Hamza.
  Doha. Qatar


   
 4. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Asante Barubaru, nikielewa sawa JKT haina ngazi ya "regiment" (maana kwa kawaida regiment inaunganisha battalions). Ni sawa?
   
Loading...