Kikosi Kazi: Tanzania ianze mchakato wa kupata Katiba Mpya baada ya Uchaguzi Mkuu 2025

Kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa kilichoundwa na Rais Samia Suluhu leo kinawasilisha taarifa ya yake na mapendezo kwa Rais Ikulu, Dar es Salaam.

Kikosi kazi chini ya mwenyekiti wake, Rewakaza Mkandala kimependekeza Tanzania ianze mchakato wa kupata katiba mpya baada ya uchaguzi mkuu 2025.
======

Rwekaza Mkandala: Mwisho mheshimiwa Rais ni suala la muda mrefu, mwaka 2011 Tanzania ilianza mchakato wa kutunga katiba mpya kwa kutunga sheria ya mabadiliko ya katiba namba 83 ya mwaka 2011.

Oktoba 2, 2014 Bunge maalum la katiba lilipiga kura kupitisha katiba inayopendekezwa ambayo ilipaswa kupigiwa kura ya maoni na wananchi ili kuithibitisha lakini mpaka sasa suala hilo halijafanyika.

Changamoto mheshimiwa Rais ni mbili
  1. Kuna wale ambao wanasema hakuna haja kuwa na katiba mpya kwani katiba ya sasa inaweza kufanyiwa marekebisho kukidhi mahitaji ya sasa na baadae.
  2. Mchakato wa kupata katiba pendekezwa haukuwa shirikishi vya kutosha kwasababu baadhi ya wajumbe wa bunge la katiba walisusia hivyo katiba hiyo kupitishwa na wajumbe waliobaki.
Pia kuna madai mchakato wa kupata katiba mpya haujakamilika, umesimama muda mrefu tangu mwaka 2014 hivyo unapaswa kukwamuliwa.

Pia kuna maoni katiba pendekezwa imeacha mambo ya msingi yaliyomo katika rasimu ya katiba pendekezwa.

Pia kuna suala la katiba mpya kwamba ni muhimu lakini halina haraka kwakuwa katiba ya sasa inafanya kazi vizuri.

Kuna wale wanaosema kuna mahitaji mengi ya wananchi ya maendeleo kuliko uhitaji wa katiba mpya hivyo ni vyema kutumia muda huu kujikita katika kuleta maendeleo ya wananchi.

Mwisho kuna wale wanaodai katiba mpya sio suluhisho ya kila changamoto zinazotukabili, zipo nchi zinazosemekana kuwa na katiba nzuri lakini bado kuna malalamiko kuhusu masuala kadhaa ikiwemo masuala ya uchaguzi.

Hapa suala la kufanyiwa kazi mheshimiwa Rais ni kupendekeza utaratibu wa mchakato wa kutiba mpya na muda wa kufanyiwa kazi.

Kikosi kazi kinapendekeza kwamba Tanzania ianze mchakato wa kupata katiba mpya mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Mapendekezo ya namna mbalimbali ya kushughulika na suala la katiba mpya baada ya uchaguzi mkuu wa 2025

Pendekezo linatokana na sababu kuu nne
  1. Kuna haja ya kuainisha dira kuu ya maendeleo kwa miaka ijayo itakayotoa muelekeo kwa katiba mpya.
  2. Kukosekana kwa muda wa kutosha kuanza kutumia katiba mpya ndani ya kalenda ya uchaguzi wa 2025
  3. Kuna haja ya kutoa fursa kwa marekebisho ya sheria ya uchaguzi na sheria ya vyama vya siasa.
  4. Kuna haja ya kutoa fursa ya kutosha kufanyia kazi masuala ya muda wa kati ikiwa ni pamoja na kuanisha dira mpya ya maendeleo.
Hiki ni kikosi kazi cha ssh anataka kubaki madarakani mpaka 2030 na ana hofu katiba mpya inaweza kumtibulia urafiki wake wa madaraka
 
Kuna vitu ukitulia na kufikiri kwa kina vinakatisha tamaa kabisa.

Mfano Mama kwa mamlaka aliyonayo aamuru mchakato wa katiba uanze mara moja au uendelee hivi hili bunge la Magufuli si ndio kisheria la kuidhinisha hiyo rasimu?

Wabunge wenyewe si ndio hawa kina Babu Tale na Covid 19?

Mimi nashauri tumuache mama tu afanye kazi tumeliwa, madhara ya Magufuli yataigharimu nchi kwa miaka mingi sana ijayo.
 
Kuna vitu ukitulia na kufikiri kwa kina vinakatisha tamaa kabisa.

Mfano Mama kwa mamlaka aliyonayo aamuru mchakato wa katiba uanze mara moja au uendelee hivi hili bunge la Magufuli si ndio kisheria la kuidhinisha hiyo rasimu? Wabunge wenyewe si ndio hawa kina Babu Tale na Covid 19?

Mimi nashauri tumuache mama tu afanye kazi tumeliwa, madhara ya Magufuli yataigharimu nchi kwa miaka mingi sana ijayo.
Lazima kuwe na bunge maalum tofauti na hilo baraza kuu la CCM
 
Back
Top Bottom