Kikosi kazi kufuatilia mawaziri goigoi, fisadi kikiongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikosi kazi kufuatilia mawaziri goigoi, fisadi kikiongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 19, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mwandishi Wetu

  Mei 18, 2011

  [​IMG]Serikali yakiri baadhi ya wawekezaji ni matapeli

  KIKOSI kazi maalumu kinatarajiwa kuundwa, hivi karibuni, kikiongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi ili kufuatilia utendaji wa mawaziri, makatibu wakuu na manaibu wao, kwa mujibu wa maazimio ya semina elekezi iliyofanyika hivi karibuni mkoani Dodoma, Raia Mwema limeelezwa.

  Kutokana na kikosi kazi hicho ambacho kinatarajiwa kuhusisha baadhi ya watendaji makini serikalini, hali sasa inatajwa kuwa tete kwa mawaziri na makatibu wakuu wanaoongoza wizara ambazo kwa muda mrefu zimeguswa kwa kashfa za ufisadi na ambazo hazina taswira nzuri mbele ya umma.

  Hatua hiyo imefikiwa wakati Serikali ikitangaza kumudu bajeti yake kwa asilimia 90 ifikapo, mwaka ambao Rais Jakaya Kikwete anaondoka madarakani (2015). Kwa sasa Serikali inamudu bajeti kwa asilimia zisizopungua 60 na zinazosalia hutolewa na wafadhili.

  Moja ya kazi ya kikosi kazi hicho ni kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa maazimio 14 yaliyotokana na semina elekezi kwa viongozi na watendaji wakuu serikalini, iliyofanyika Mei 9 hadi 14, mwaka huu, mkoani Dodoma, hoteli ya Mtakatifu Gaspar.

  Tayari Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, amethibitisha mkakati huo alipokuwa akisoma maazimio ya semina elekezi Dodoma.

  "Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi itaweka na kusimamia utaratibu wa utekelezaji na ufuatiliaji (maazimio). Viongozi na watendaji wakuu watatakiwa kuwasilisha taarifa za utekelezaji katika maeneo yao kila robo mwaka kwenye Baraza la Mawaziri," alisema Luhanjo.

  Pamoja na mkakati huo, taarifa kutoka ndani ya semina elekezi zinabainisha kuwa Serikali imepanga kuwageukia na kuwachunguza zaidi wawekezaji wanaoingia nchini kwa ajili ya kuwekeza na hasa kwa kuingia ubia na Serikali.

  Katika semina hiyo elekezi imeelezwa kuwa Serikali ililega lega katika kuwachuja wawekezaji wanaongia nchini na matokeo yake, taswira ya Tanzania katika kupata wawekezaji makini si nzuri kimataifa.

  "Tumelegalega katika kuwachuja wawekezaji. Bahati mbaya kuna wengine ni matapeli na baadhi hawakuwa hata na mitaji ya kutosha. Wameingia nchini kama wawekezaji na kujikuta katika ubia na Serikali na mwishowe ni kuibuka kwa kashfa.

  "Sasa tunataka kujipanga kama Serikali kuhakikisha wawekezaji wanaoingia nchini ni makini, wenye rekodi ya uadilifu na si wababaishaji ambao baadhi tumebaini wamekuwa wakishirikiana na baadhi ya viongozi kuwekeza katika misingi ya ubabaishaji," alisema mmoja wa makatibu wakuu aliyeshiriki semina hiyo elekezi.

  Wakati uamuzi huo wa ‘kupembua' wawekezaji wa kigeni nchini ukiwa umejadiliwa kwa kina kwenye semina elekezi, taarifa zinabainisha kuwa ingawa baadhi ya mawaziri wameanza kuchukua hatua, zipo wizara vinara kwa kashfa zinazonyooshewa vidole na umma.

  Wizara hizo ambazo zimekubuhu katika kashfa za ufisadi wa mabilioni ya fedha ni pamoja na Wizara ya Nishati na Madini inayogubikwa kwa kashfa za miradi ya umeme wa dharura.

  Wizara nyingine ni Nyumba na Maendeleo ya Makazi inayozongwa na utoaji hati za umiliki ardhi kwa mtu zaidi ya mmoja na pia kugawa maeneo ya wazi, kashfa inayogusa pia halmashauri kadhaa nchini.

  Wizara ya Miundombinu imo katika orodha hiyo ikinuka kashfa za kuingia mkataba na wawekezaji wenye utata, hasa wa Rites waliongia nchini kuendesha lililokuwa Shirika la Reli (TRC), nyingine ni Wizara ya Ujenzi, ambayo kupitia Wakala wa Barabara, imesababishia hasara ya mabilioni Serikali kwa kuingia au kuvunja mikataba na makandarasi bila umakini.

  Wizara ya Maliasili na Utalii inaguswa kwa kashfa za vitalu vya uwindaji na usafirishaji haramu wa maliasili za nchi hasa mazao ya misitu. Menejimenti ya Utumishi wa Umma inakabiliwa na kashfa ya ulipaji mishahara hewa.

  Katika mwelekeo huo huo wa kudhibiti nyendo za mawaziri, makatibu wakuu na manaibu wao, Rais Jakaya Kikwete, amekwishakuwaelekeza kuwa licha ya mabango ya kupinga rushwa katika wizara zao lakini rushwa inatendeka kwenye wizara hizo.

  "Rushwa inatendeka katika wizara zenu, katika idara chini yenu, hakuna mwingine mwenye dhamana zaidi yenu kuongoza mapambano haya, piganeni muonekane mnapigana ili kero hii tuimalize, au tuipunguze," alisema Kikwete katika hotuba yake ya kufunga semina elekezi Dodoma, mwishoni mwa wiki hii.

  Kikwete aliwataka mawaziri wake kuhakikisha mabango yanayokataza rushwa wizarani, yanafanana na tabia, mwenendo na sifa za anayefanya kazi katika ofisi hizo.

  "Maana kama ofisa anaendelea kudai rushwa katika ofisi hizo, mabango hayo yatakuwa kiini macho na kichekesho," alisema na kuongeza kuwa;

  "Wananchi wangependa kuona baada ya semina hii kasi na ufanisi wa kutekeleza majukumu yetu kwa umakini inaongezeka hasa katika uzalishaji na utoaji huduma huku mkizingatia utawala bora, utawala wa sheria, kuheshimu Katiba, nidhamu ya kazi na uwajibikaji."

  Katika semina elekezi Dodoma maazimio 14 yaliwekwa ambayo ni kutekeleza kwa ukamilifu, ufanisi na uadilifu majukumu serikalini kwa uelewano na kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.

  Maazimio mengine ni kuepuka misiguano au mivutano kati ya mihimili ya dola ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama; kwa kuzingatia dira ya maendeleo 2025, mpango wa miaka 15 utatayarishwa kupitia mipango ya kati wa miaka mitano mitano ili kufikia lengo la kipato cha kati kimataifa.

  Maazimio zaidi ni kuongeza mapato ya ndani na kudhibiti matumizi ili kupunguza kiwango cha misaada ya wahisani katika bajeti hadi kufikia kisichozidi asilimia 10, mwaka 2015.
   
 2. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hakuna cha maana kitakachofanywa na hicho kikosi. Kwani watu wa usalama kazi yao ni nini? Sana sana hicho kikosi kifanya ufisadi kwa kushirikiana na hao wanaowafuatiia.
   
 3. TITAN

  TITAN JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 309
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Porojo tuu kwani walikuwa wapi sikuzote!!!!
   
 4. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2011
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mchongo mwingine wa kumtengenezea luhanjo posho maridhawa kabla hajastaafu. heri yao watakaokuwamo humo kwenye kikosi kazi. nawaapia kama kuna ambaye hajajenga hadi leo basi ndio wakati wa kuporomosha kibanda huu. hahah msiache kutujuza kwa siku watakuwa wanalamba laki ngapi, luhanjo msiniambie, yeye najua kwa siku si chini ya 1M.

  ndo bongo hii mazee!
   
 5. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2011
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  cha maana kipo mkuu.

  wale amabo walikuwa hawajajenga, hakika safari hii watamaliza vibanda vyao kabisa!
   
 6. Landala

  Landala JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 938
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Wote wameisha jenga,zaidi wataongeza fedha za ufisadi watakaoufanya kwenye akaunti zao.
   
 7. p

  plawala JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama cha kufuatilia hela za EPA,kama waziri goigoi ameteuliwa kwa kazi gani au kwa nini
   
 8. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kikosi kazi cha nini wakati yupo Waziri mkuu?
   
 9. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #9
  May 19, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Waanze na rais
   
 10. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #10
  May 19, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  - Whaat a joke!

  William @ NYC, USA.
   
 11. A

  Ame JF-Expert Member

  #11
  May 19, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Tueleze mtetezi wa chama cha magamba; naona na wewe umeanza kuwashangaa magamba wenzako, magamba yamekataa kuvuka sasa inabidi mtengeneze parallel structure huku mkiwaacha magamba waendelee kula joto la damu ya watanzania. Haya wee subiri tuwakute hapo mtatukoma teh!
   
 12. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #12
  May 21, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  - I have said time and times again, mimi sio bendera inayokwenda bila kuuliza wala kufikiri, kwenye kujivua magamba CCM iko right on the track, lakini mengine kama haya ya Semina Elekezi na the rest ni pure waste of our National time and money!

  - Shule kubwa huku USA, nilijisomesha mwenyewe ili niweze kufikiri, kuchambua na kuona for my self, badala ya kufanyiwa na wengine na mimi kufuata upepo tu!


  William @ NYC, USA.
   
 13. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #13
  May 21, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kwenye hilo Raia Fulani tuko pamoja, hasa pale ndiyo pana ugoigoi
   
 14. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #14
  May 21, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kikosi kazi kinafatilia utendaji wa mawaziri wabovu. Hii nchi bwana hivi lini tutaacha usanii? Kwani wabunge kazi yao nini? Bunge kazi yake nini? Mianya ya ufisadi tu ndio imo ndani ya fikra zetu. Kikosi hicho ni another mrija wa ufisadi tu na waste of tax payers money.
   
 15. M

  Makupa JF-Expert Member

  #15
  May 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kaka hiki kikosi kazi cha kufuatilia utendaji wa mawaziri it is purely misuse of national resources nakuunga mkono kwa asilimis mia
   
 16. T

  T.K JF-Expert Member

  #16
  May 21, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 345
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Huyu Rais wa hii nchi bila shaka atakua na matatizo ya akili.......wote ho kawachagua yeye. akiona hawafai si awafukuze tu kuliko kutumia mali za umma eti kufatilia mawaziri alio wateua yy......hii ni big joke!
   
Loading...