Kikosi kazi cha Rais cha kukusanya maoni ya Katiba Mpya

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Chonde chonde tunaiomba kikosi kazi cha Mhe. Rais kinachokusanya maoni ya katiba mpya ipite kwenye Wilaya zote na ratiba iwekwe kwenye magazeti na matangazo kupitia vyombo vya habari. Mhe. Rais sisi wananchi tunataka Katiba mpya kabla ya uchaguzi wa 2025. Uchaguzi wa 2025 katiba mpya ndiyo itumike.
 
Mm katiba mpya ikajadiliwe na wale waruka karakasi bungeni? Katiba mpya kwa sasa itakuwa ni kutengeneza bomu la kututesa kwa miaka 50 ijayo.
Kuna vichwa havipo hapo bongeni kwajili ya kuja na hoja na michango mizito
 
Katiba mpya itagusa muungano ndiyo maana CCM kamwe hawatakubali. Nyerere aliwaonya CCM wasiuguse muungano.
 
Katiba Mpya ni suala nyeti haliwezi kujadiliwa na wale waruka acrobatic bungeni waliozoea kujadili vioja badala ya hoja. .. 'Tanzania got talent show' iko bungeni.
 
Chonde chonde tunaiomba kikosi kazi cha Mhe. Rais kinachokusanya maoni ya katiba mpya ipite kwenye Wilaya zote na ratiba iwekwe kwenye magazeti na matangazo kupitia vyombo vya habari. Mhe. Rais sisi wananchi tunataka Katiba mpya kabla ya uchaguzi wa 2025. Uchaguzi wa 2025 katiba mpya ndiyo itumike.
Kwa hiyo Yale mamia ya mabilioni yalitotumika kwenye tume ya Jaji Warioba yalipotea bure!!!!!
 
Ni Kupoteza Muda na raslimali tu. Raslimali ya Katiba mpya ipo, kinachotakiwa ni kuweka utaratibu wa kuhama kutoka katiba ya zamani na kuanza kutumia hiyo mpya. In fact Mzee Waryoba aliiandika vizuri sana, ikapitiwa na Bunge maalum la Katiba (Samia mwenyewe akiwa Mwenyekiti) lakini Kikwete akaifukia uvunguni halafu Magufuli akapokea serikali kama vile rasimu hiyo haipo kabisa; yaani haikuwa kati ya instruments alizopokea kutoka kwa Kikwete.
 
Jiwe aliwahi kusema kuwa,asiulizwe masuala ya katiba mpya coz kwenye kampeni zake hakuwahi kuahidi hilo suala.na everyone akaufyata.
 
Chonde chonde tunaiomba kikosi kazi cha Mhe. Rais kinachokusanya maoni ya katiba mpya ipite kwenye Wilaya zote na ratiba iwekwe kwenye magazeti na matangazo kupitia vyombo vya habari. Mhe. Rais sisi wananchi tunataka Katiba mpya kabla ya uchaguzi wa 2025. Uchaguzi wa 2025 katiba mpya ndiyo itumike.
Nchi haina fedha lakini Hangaya kwa kushauriwa na Kikwete anapoteza fedha zingine ili hali wananchi nchi nzima waliisha toa maoni juu ya Katiba waitakayo!!! Rasimu ya Warioba ipo, sasa Hangaya na hilo genge alilounda watafanya kazi zaidi ya ile iliyofanywa na wataalam wa kundi la Warioba? Hao Watu wa hicho kikosi kazi kwanza hawana weledi wa mambo ya Katiba ; ni watu ambao Kikwete kawakusanya na kumpa Hangaya eti wakusanye maoni ya Katiba mpya ; yote hiyo ni kupoteza Wakati ili ifikapo 2025 watakuwa hawajafanya kazi yeyote na nchi itakwenda kwenye uchaguzi ikitumia hii katiba ya mafisadi!!

Kikwete anataka sifa kuwa yeye akimuogoza Hangaya ndio architect wa Katiba mpya ili hali ni yeye Kikwete huyo huyo ndio alihujumu katba mpya kupatikana wakati huo akiwa Rais. Kikwete hana moral authority hata kujifanya anawapa muongozo hao mercenaries wao mnaowaita kikosi kazi kwani mpaka sasa hajatubu kwanini alihujumu ile rasimu ya Warioba!!! For all intentions and purposes mwanasiasa adui mkubwa wa maendeleo ya Tanzania ni huyu mkwere na anafanya hivyo for his own selfish reasons!
 
Katiba mpya itagusa muungano ndiyo maana CCM kamwe hawatakubali. Nyerere aliwaonya CCM wasiuguse muungano.

Sawa suala la muungano ni contestions lakini hiyo haizuii kuadopt rasimu ya Katiba ya Warioba!!! Mambo contentious kwa Mfano kuwa na serikali ngapi yanaweza kujadiliwa bila ya kupoteza fedha nyingine kwenye hicho kikundi mnachosema Hangaya amesema kinalinda shamba lake mpaka 2030!!
 
Jiwe aliwahi kusema kuwa,asiulizwe masuala ya katiba mpya coz kwenye kampeni zake hakuwahi kuahidi hilo suala.na everyone akaufyata.

Sawa sasa huyo Jiwe kwa kupinga Katiba mpya ameishia wapi? Na wote watakaohujumu matakwa ya wengi wataishia huko huko kwani SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU!
 
Kikwete mbona bado anadunda mpaka leo?
 
Sawa suala la muungano ni contestions lakini hiyo haizuii kuadopt rasimu ya Katiba ya Warioba!!! Mambo contentious kwa Mfano kuwa na serikali ngapi yanaweza kujadiliwa bila ya kupoteza fedha nyingine kwenye hicho kikundi mnachosema Hangaya amesema kinalinda shamba lake mpaka 2030!!
Haya madaraka makubwa aliyopewa raisi kwenye katiba ndiyo inayompa kufanya haya bila kuzingatia maoni ya Watanzania.Ametuona wote mazuzu tu.Lakini itafika wakati tutasema sasa vatosha.Ikifikia hapo tutaelewana tu.

Vikosi kazi hivi ni ulaji na matumizi mabaya ya kodi za Watanzania.Maoni ya kutosha tulikwishatoa,tena kwa utaratibu mzuri.Huku ni kuhalalisha kufanya uchaguzi bila katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Najaribu kuona huu usanii sioni mwisho wake.Mbona tumekamuliwa na tunaendelea kukamuliwa,tutafunga mikanda mpaka lini wakati hali ya maisha inakuwa ngumu hivi.Hapa kijijini hakuna anayeweza tena kula chakula chenye mafuta.Badala ya kutatua hili,anawatengenezea watu ulaji usiokuwa wa lazima tena kwa jambo lililokwishafanyika.

Unategemea hicho kikosi alichokichagua yeye kije na mapendekezo ya wananchi kuwa wamependekeza mamlaka makubwa ya raisi yapitiwe upya na kuyapunguza watathubutu kuyatoa?

Tunaumia kwenye matozo,matozo,matozo kila mahali.Jamani,raisi wa wanyonge yuko wapi.Tulifika mahali tukakataa kuitwa wanyonge,naona inabidi tukubali tu kuwa sisi ni wanyonge.Tumelemewa sana tena kila mahali.
 
Kwa hiyo Yale mamia ya mabilioni yalitotumika kwenye tume ya Jaji Warioba yalipotea bure!!!!!
Baada ya kukusanya maoni kipindi kilichopita na Bunge la katiba kufanya kikao chake kilichotakiwa ni kufanyiwa kazi kwa Yale yaliyojadiliwa hii ya Sasa ni delaying tactics na matumizi mabaya ya rasilimali za nchi hakuna jipya hapo
 
Chonde chonde tunaiomba kikosi kazi cha Mhe. Rais kinachokusanya maoni ya katiba mpya ipite kwenye Wilaya zote na ratiba iwekwe kwenye magazeti na matangazo kupitia vyombo vya habari. Mhe. Rais sisi wananchi tunataka Katiba mpya kabla ya uchaguzi wa 2025. Uchaguzi wa 2025 katiba mpya ndiyo itumike.
Maoni gani mapya yanayotafutwa!! Mbona tume iliwahi kuundwa miaka michache tu iliyopita na maoni yapo. Si wamwulize mzee Warioba maoni ya wananchi!! Hii pesa waliyopanga kutumia si waipeleke kwenye ruzuku ya mafuta ya gari! Huu ni UBADHIRIFU wa fedha!!
 
Baada ya kukusanya maoni kipindi kilichopita na Bunge la katiba kufanya kikao chake kilichotakiwa ni kufanyiwa kazi kwa Yale yaliyojadiliwa hii ya Sasa ni delaying tactics na matumizi mabaya ya rasilimali za nchi hakuna jipya hapo

Kikwete ameiteka ccm kwa kumrudisha Kinana kama makamu wa Mwenyekiti na hivyo kuwa ndio de facto mwemyekiti kwani Hangaya hana Mbele wala nyuma!! Kikwete ndiyo anaendesha ccm kwa utashi wake Hivi sasa; wapambe wake wametapakaa nchi Nzima kuhakikisha kwenye chaguzi za ccm zinazoendelea wanachaguliwa watu wao waliowadhamini kwa fedha!! Hivi sasa Watu wa mtandao wakina Nchimbi ndio kazi wanayoifanya kwa maelekezo ya Kikwete!!! Mungu aijalie nchi ipate kiongozi mwingine jasiri lakini mwenye roho ya utu aweze kukabiliana na uozo huu!
 
Back
Top Bottom