Kikosi JWTZ kuwa na askari Takribani 200 tu Mpakani ni masihara

Mara nyingi huwa nashindwa kuwaelewa watanzania wenzangu, maana ukweli ukisemwa wao wanapinga na kusema sio vizuri, wengi wa wachangiaji wa hii mada ni wale wale waliokuwa wanataka kujua kuhusu mishahara ya wanajeshi, walipoambiwa ni siri wakataka waambiwe tu eti kwa kisingizio mbona hata marekani mishahara ya wanajeshi iko wazi, sasa leo hii rais ameambiwa idadi ya wanajeshi walio mpakani wanasema tena kwamba ooh hakupaswa kuambiwa ukweli kwa usalama wa taifa letu.
Tuwe na msimamo mmoja koye kote tusipende kujua yaliyo siri.
By the way mr P kadanganywa hakuna ukweli hapo. ngoja nivute kwanza maana bangi yangi yangu inaungua kwa spidi na kila nikiweka mate bado inazidi kuungua

sent from my Samsung smart tv using JamiiForums
 
Acha Kufanisha JWTZ na KDF wewe

Ninavyojua Kigoma Na Tabora kuna Kambi Kubwa sana za JWTZ Binafsi Wakati nasoma Tabora Boys kwa miaka Kama 6 Ule Mji Unakutana na wanajeshi tuu Kutwa Nzima

Kuna kambi kama Tatu pale Tabora nawaamia JWTZ hata wakiwa 100
View attachment 546702
Mkuu kula like yangu.
Yaani hiyo gwanda hapo inavyonivutia basi tuu nishakuwa mhenga
 
Unacho kijadili hukijui
hivyo Akili yako ilipo ishia ndio uhalisia unapo anzia
hutapata majibu
Tanzania ipo Imara
hakuna wakutuchezea Ktk mipaka yetu yote
e96674d0154711cd60a4ab484d67109c.jpg
 
Kila kikosi cha kijeshi kipo hapo kwa sababu zake maalumu, na kazi zake maalum. Inawezekana kabisa kikawa na hao 200 au hata pungufu kulingana na shughuli gani wanafanya.
 
Nilipoona kichwa cha habar cha hii post niliufungua uzi nikiwa na hamu ya kukupa jibu LA kitaalamu kuhusu suala Hilo,lakini nilipousoma nikagundua lengo lako sio kupata Hilo jibu ila kuelezea chuki zako binafsi tu kwa wanajeshi so nimeona niudharau tu
 
Askari 200 Ni wachache sana kwa mpaka Mkubwa wa Jiji kubwa la Dsm.
Waongezeke zaidi tena wapunguze kuvaa mavazi ya Kijeshi ili wafanye kazi vizuri kwa ufanisi zaidi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
!
!
Dunia imebadilika. Siku hizi ulinzi sio maguvu ni teknolojia tu. Kuwa na wanajeshi wengi kama kwenye picha za wavetenam haikuhakikishii ulinzi madhubuti. Ukute huo mpaka unaweza kulindwa na watu ishirini tu wenye teknolojia na vifaa sahihi. Wale wapasua mawe kwa vichwa hawana nafasi katika dunia hii ya unmanned aerial vehicles
Teknilojia hiyo tunayo?
 
Katika mazungumzo yake Rais Magufuli na wananchi leo Mjini Ngara, amemuuliza mkuu wa kambi ya jeshi iliopo kwenye mpaka unao unganisha mataifa mawili ya Burundi na Rwanda kuwa kikosi chake kina wanajeshi wangapi?

Mkuu huyo wa kambi kwa kukiuka Taratibu pia na yeye akaropoka kuwa wapo takribani 200. kwanza taarifa hii ni hatari kwa Taifa kwani siku zote taarifa za askari wa taifa hasa hasa wanajeshi huwa ni siri sana.

Pia vikosi vya vingi vilivyopo kwenye mipaka huwa ni vikosi vikubwa kwendana na mahitaji kiukweli kwa nchi hii kuwa na askari jeshi 200 kwa mpaka wenye nchi mbili ni dharau kubwa kwa watanzania.

Askari jeshi wengi wamejaa Dsm na wanashinda "kona bar, Afrikasana, Buguruni- kimboka" kazi kutembea na madada poa.

Je, mishahara wanayolipwa ni kwa kazi ipi waifanyayo?
Acha KUROPOKA unaona mwenyewe siiiiiifa kuandika kwa vihisia vyako. Nchi nzima unajua wanajeshi wapo wangapi? Na wamegawanywaje??? Taratibu zakijeshi unazijua ktk kuwagawanya?? Au unatoa bandiko tu ili watu wacomment?? Haya bana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
!
!
Dunia imebadilika. Siku hizi ulinzi sio maguvu ni teknolojia tu. Kuwa na wanajeshi wengi kama kwenye picha za wavetenam haikuhakikishii ulinzi madhubuti. Ukute huo mpaka unaweza kulindwa na watu ishirini tu wenye teknolojia na vifaa sahihi. Wale wapasua mawe kwa vichwa hawana nafasi katika dunia hii ya unmanned aerial vehicles
Good bro

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom