KIKOSI cha wachezaji 27 wa timu ya soka ya taifa ya Ivory Coast, cha tua Dar

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
KIKOSI cha wachezaji 27 wa timu ya soka ya taifa ya Ivory Coast, Tembo kimewasili usikuhuu Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam kikitokea Abidjan na kupitia Kongo Brazaville, tayari kwa mchezo wa Kundi C Jumapili kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwakani, dhidi ya wenyeji Tanzania, Taifa Stars.
Kikosi hicho kilitua JNIA majiraya saa 4:15 usiku na kutumia zaidi ya saa 1:30 ndani ya Uwanja wa Ndege kwa taratibu za kukaguliwa kabla ya kupanda basi la kisasa la klabu Azam FC kupelekwa katika hoteli ya Bahari Beach, Dar es Salaam.

Nyota waliowasili na kikosi hicho ni Nahodha, Yaya Toure, Akpa Akpro Jean-Daniel Dave Lewis, Angoua Brou Benjamin,Arouna Kone, Aurier Serge Alain Stephane, Bamba Souleman, Barry Boubacar, Boka Etienne Arthur, Bolly Mathis Gazoa Kippersund, Bony Wilfried Guemiand, Cisse Abdoul Karim, Diarrassou Ousmane Viera na Dja Djedje Brice Florentin.
Wengine ni Doumbia Seydou, Gbohouo Guelassiognon Sylvain, Kalou Salomon, Armand Magloire, N’dri Koffi Christian Romaric, Sangare Badra, Serey Die Gnonzaroua Geoffroy, Sio Giovanni, Tiote Cheik Ismael, Traore Lacina, Ya Konan Didier, Yao Kouassi Gervais na Zokora Deguy Alain Didier.
Tembo wa Ivory Coast watafanya mazoezi Ijumaa kwenye Uwanja wa Ghymkhana na Jumamosi watafanya kwenye Uwanja waTaifa.
Wenyeji Taifa Stars wako kambini katika hoteli ya Tansoma, katikati ya Jiji tangu warejee kutoka Marakech, Morocco Jumatatu ambako Jumamosi walifungwa na wenyeji, Simba wa Atlasi mabao 2-1, siku ambayo Ivory Coast iliifunga Gambia 3-0 katika mchezo mwingine wa Kundi hilo.
Stars, inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ambayo ikifanya mazoezi Uwanja wa Karume, Ijumaa itapumzika na Jumamosi itahamia kwenye Uwanja wa Taifa.
Makocha wa timu zote mbili (Taifa Stars na Tembo) watakutana na waandishi wa habari Jumamosi Saa 4:00 asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF kuzungumzia jinsi walivyojiandaa kwa mechi hiyo.
Mechi hiyo itachezwa Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 9:00 Alasiri, na itachezeshwa na Charef Mehdi Abdi kutoka Algeria.
Kiingilio cha chini katika mechi hiyo ni Sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani, Viti vya kijani katika uwanja huo wenye uwezo wa kumeza watazamaji 60,000 viko 19,648. Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu ambavyo viko 17,045 ni sh. 7,000. Kiingilio kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897ni sh. 10,000.
Viingilio vya daraja la juu ni; VIP C yenye watazamaji 4,060 ni sh. 15,000 wakati sh. 20,000 ni kwa VIP B yenye watazamaji4,160. VIP A yenye watazamaji 748 kiingilio chake ni sh. 30,000

Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zitaanza kuuzwa siku mbili kabla ya mchezo (Ijumaa na Jumamosi) katika vituo vifuatavyo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala na BMM Saloniliyoko Sinza Madukani.
Katika vituo hivyo tiketi zitauzwa katika magari maalumu, ambayo pia yatafanya mauzo ya tiketi uwanjani siku ya mechi.
Ivory Coast ndio wanaongoza Kundi hilo kwa pointi zao 10, wakifuatiwa na Tanzania yenye pointi sita, wakati Morocco yenye pointi tano ni ya tatu na Gambia inashika mkia.
Stars inahitaji kushinda Jumapili ili kufikisha pointi tisa na ishinde tena mechi ya mwisho dhidi ya Gambia, hukuikiiombea Ivory Coast ifungwe au kutoa sare na Morocco ili kuongoza Kundi hilo.
Ikifanikiwa kuongoza kundi hilo, Stars itaingia hatua ya pilina ya mwisho ya kuwania tiketi ya Brazil mwakani kwa kucheza na moja ya timu nyingine tisa zilizoongoza makundi mengine ambapo ikishinda milango ya Brazil itakuwa wazi kwao na kuweka historia ya kufuzu kwenye michuano hiyo kwa mara ya kwanza.
Hata hivyo, kabla ya kuja Dar es Salaam mchezaji chipukizi wa Manchester City, Abdul Razak aliondolewa kwenye kikosi hicho kwa kupigana na mchezaji mwenzake mazoezini.
Kiungo huyo mwenye umri wamiaka 20, aliadhibiwa kwa kumpiga Jean-Jacques Gosso, anayecheza Mersin Idmanyurdu ya Uturuki, ambaye naye ameeenguliwa pia.
 
J/pili ushindi ni lazima. Tuta mgonga goli moja (1) bila, litakalo fungwa na Salum Abubakar ktk kipindi cha kwanza.
 
Back
Top Bottom