Kikosi cha wachezaji 23 cha Taifa Stars AFCON 2019 chatajwa

Tutakaoiua stars tutatengeneza pesa ndefu wale wazee wenzangu wa kubeti
Abdi Banda ni mchezaji mzuri sana nafkiri kocha ana aleji naye, sioni sababu ya kuweka makipa 3 wakati hatuendi mbali, Nikiicheck Senegal naona hapa kuna mkono cku ya kwanza kucheza
 
Kichuya ana umuhimu wake kwenye mpira , tusitarajie hali ya mpira ikawa ni pass tuu, lakini kuna wakati kutokana mazingira ya mechi inahitaji mtu mwenye spidi , chenga na kinganganizi. Tatizo kubwa la AMUNIKE ana allegy na anamchukia KICHUYA kama ilivyo kwa ZAHERA na KAMUSOKO. Kichuya sio wa kisportsport kama kocha anavyomchukulia, ana umuhimu wake hata alipokuwa SIMBA sisi yanga tulikuwa tunakosa imani anaposhika mpira sasa kama unaua kipaji chake poa tuu OGAAAAA!!!!!!
wabongo tuna tatizo la kuishi kwa mazoea, Kichuya Banda siyo wale uliokuwa unawajua...Kichuya ndiyo kabisa hata hiyo speed sasahivi hana...zero offensive & defensive na cross accurate zake hamna kitu...Ajibu mwenyewe kwa mpira wa sasa sioni umuhimu wake...nadhani wote waliotemwa kasoro yule dogo Kelvin John kocha alikuwa sahihi.
 
Watanzania tunalalamika sababu tumezoea kulalamika na hata kulalamika hatulalamikii vitu vya msingi bali ni mazoea na ushabiki. Kwanza tujue Wachezaji wetu viwango vyao havipishani saana tofauti ni kujituma na exposure kidogo...
Tukianza na upande wa Goalkeeping makipa wote walioitwa ni wazuri na wana kiwango kikubwa sana wanastahili kuwepo ila wote wanakosa experience ni vijana wadogo na kukosa uzoefu ndo kutatucost lakini hamna Mtanzania alieliona hili na kulalamika KASEJA alistahili kuwepo hapa.
Tukija kwenye mabeki wa pembeni upande wa kulia ndo kuna mushkeli kidogo Kessy na Vincent Philipo hawajatulia kiviile Hapa PAUL GODFREY "boxer" alistahili kuwepo. Upande wa kushoto uko vizuri.
Ukija upande wa kati upo vizuri saana wengi wanalalamikia kutokuwepo kwa Banda lakini hata kitakwimu na kutazama soka Banda msimu huu hajafikia performance ya Nyoni, Moris, Yondani au Sonso kama kuna watazamaji wa TPL watakubaliana na mimi kuhusu performance ya Sonso sema wabongo tumekariri eti Banda afu advantage hapa Sonso na Nyoni wana uwezo wa kucheza namba sita (Kiungo mkabaji) na tumewaona wakicheza namba hizo vizuri tu kwenye timu zao.
Kwa upande wa viungo sijajua kwa nini SURE BOY, na MZAMIRU hawapo ila hata hao waliopo sio wabovu wanaweza kufit kutokana na viwango vya wachezaji wetu.
Kwa upande wa mawinga ni sawa kabisa Kichuya sio kivile ukilinganisha na Farid Musa ambaye kiwango chake kina improve. Watu wanalalamika pia Chilunda kuachwa ila huyu Chilunda wa sasa huwezi mlinganisha na Zayd hata kidogo no wonder Tenerife wamemtema.
Kwa upande wa washambuliaji nafasi ya Ulimwengu kocha angempa yule kinda wa U-17 ili apate uzoefu ni mzuri kuliko Ulimwengu mzee wa faulo.
Kwa MKUDE na AJIBU hao ni sawa tu kuachwa hawathamini vipaji vyao, tena kwa upande wa Ajibu nimemshuhudia mwenyewe na tabia zake kipindi akiwa Mwadui FC, anakuja zoezi anavaa viatu zaidi ya dk 45 akimaliza wenzake wnamalizia warm up akiambiwa anajibu anavyojua yeye.
Tukisapoti kikosi chetu ingawa kulingana na vipaji vya wachezaji wetu hatutoboi kokote hatushindi hata mechi moja na droo ni majaliwa
NB KAMA TUTAFUNGA GOLI/MAGOLI MSUVA NDO ATAKUWA TOP SCORER SIO SAMMATA Mark my words


Umeitendea haki JF kwa mchango makini na elekezi
 
Namshangaa coach,
Like tunaenda kujaribu vile,hata kama kuwa na imani ariff lakini c kwa hali hii. Banda,kichuya+
Duh!! GOD BLESS US......
hivi kichuya lini kacheza mpira wa maana?!..au kona aliyowafunga yanga?..kichuya atamkaba nani kwa umbo lile!!!?
 
wabongo tuna tatizo la kuishi kwa mazoea, Kichuya Banda siyo wale uliokuwa unawajua...Kichuya ndiyo kabisa hata hiyo speed sasahivi hana...zero offensive & defensive na cross accurate zake hamna kitu...Ajibu mwenyewe kwa mpira wa sasa sioni umuhimu wake...nadhani wote waliotemwa kasoro yule dogo Kelvin John kocha alikuwa sahihi.
Mbappe angeenda nafasi ya kipa mmoja.
 
Back
Top Bottom