Kikosi cha wachezaji 21 wa Al Ahly kinachokuja Tanzania Dhidi ya Simba

dos santos

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
256
128
Kocha wa Al Ahly Martin Lasarte ametaja majina ya kikosi chake cha wachezaji 21 ambacho kimesafirisha usiku huu kuja Tanzania ili kukabiliana na Simba SC katika mechi ya hatua za makundi ya klabu bingwa Afrika itakayopigwa Jumanne tarehe 12.

Al Ahly katika mchezo uliopita waliitandika Simba kwa jumla ya Mabao 5-0 nchini Misri.

Katika kikosi kitakachokuja TZ Al Ahly itamkosa Nahodha wake Hossam Ashour ambaye ni majeruhi pamoja na wachezaji Walid Azaro, Ahmed Fathi, Walid Soliman, na Marwan Mohsen nao hawatakuwepo.

Aidha mchezaji Yasser Ibrahim baada ya kupoteza michezo mitatu ya mwisho kwa sababu ya kuumia amerejea kikosini pamoja na Mohamed Sherif. Pia mshambuliaji Ramadhan Sobhi amejumuishwa kwenye kikosi baada ya kuukosa mchezo wa kwanza nchini Misri kwa kuwa majeruhi.

Kikosi kamili cha Al Ahly Sc kilichosafiri kuja Tanzania ni:
Magolikipa: Sherif Ekramy, Mohamed El Shennawy, and Ali Lotfi.

Walinzi: Saad Samir, Rami Rabia, Ayman Ashraf, Ali Maaloul, Mahmoud Wahid, Mohamed Hany, Yasser Ibrahim.

Viungo: Amr El-Sulya, Karim Nedved, Hamdi Fathi, Islam Mohareb, Hussein El-Shahat, Ramadhan Sobhi, Nasser Maher, Mohamed Sherif, Hesham Mohamed.

Washambuliaji: Salah Mohsen, Junior Ajayi.
 
Ngoja tuone itakuaje hiyo j4 maana du ngoma inaweza kuwa ni 50/50
 
Daa tunaobeti jumanne kuna fursa tena.... Fursa ikija itumie ipasavyo
Fursa kama hii
IMG-20190202-WA0015.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom