Kikosi Cha Taifa Stars Kuelekea Kombe la Dunia Chatajwa, Chombo Lidondo atajwa

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,206
4,696
Orodha kamili imeshatolewa muda mfupi uliopita na Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF)

Maandalizi za mechi
za kufuzu Fainali za Kombe bill Dunia dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( DRC) na Madagascar

Sura mpya Ramadhi Chombo Lidondo (Super Midfielder)

Wadau karibuni mtoe maoni

FDGBQPLX0AkdMGJ
 
Kuna baadhi ya wachezaji hapo hawana jipya. Ni bora kuita wachezaji wachache tu wenye tija, badala ya kubeba tu kila mtu.
 
Orodha kamili imeshatolewa muda mfupi uliopita na Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF)

Maandalizi za mechi
za kufuzu Fainali za Kombe bill Dunia dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( DRC) na Madagascar

Sura mpya Ramadhi Chombo Lidondo (Super Midfielder)

Wadau karibuni mtoe maoni

FDGBQPLX0AkdMGJ
Hivi hapa duniani kulishawahi kuwa na Mchezaji aitwae Lidondo? Hivi yule Kiungo Fundi wa Hispania Redondo siku hizi yuko wapi?
 
Orodha kamili imeshatolewa muda mfupi uliopita na Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF)

Maandalizi za mechi
za kufuzu Fainali za Kombe bill Dunia dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( DRC) na Madagascar

Sura mpya Ramadhi Chombo Lidondo (Super Midfielder)

Wadau karibuni mtoe maoni

FDGBQPLX0AkdMGJ
Lidondo anacheza timu gani mkuu maana sijawahi kumsikia huyu mchezaji
 
Kuna kitu huwa kinanishangaza. Israel Mwenda huwa hachezi sana Simba, ila naona Taifa stars kaaminiwa kuliko Kapombe.

Sasa najiuliza, kwa nini Mwenda hapati namba muda mwingi Simba, ili atumike pia Taifa stars kwani Kapombe ameishazeeka!

Ukiangalia mechi za Simba ( ikiwemo ya Jwaneng) na Taifa stars , magoli kadhaa huwa yanapitia kwa Kapombe, ambapo huwa anafanya makosa ikiwemo kupanda bila mpangalio na hivyo kuacha gap nyuma, tofauti na Mwenda ambapo hata game ya Benin aliwamudu sana washambuliaji wa Benin, ijapokuwa walikuwa wanapitia upande wake wakiwa wengi.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Nimpongeze kocha KP Kim Poulsen kwa kuendelea kuwaamini vijana wake aliowafundisha Serengeti Boys iliyoshiriki AFCON U17 2017:~

Ramadhan Kabwili
Israel Mwenda
Kibwana Shomari
Nickson Kibabage
Dickson Job n.k

Hakika anatutengenezea taratibu kizazi cha kuwarithi hawa waliozeeka. Hii ndio sababu inayonifanya niendelee kumuamini Kim miaka 100. Waliomfukuza mwanzo waliharibu sana project za huyu mwamba.
 
Tubakie kuwa Wazalendo wakweli LAKINI sio vibaya kuuangalia wasifu Kocha wa DRC Congo. Huyu mtu Hector Cuper nimemshuhudia mara kadhaa akiziongoza timu za spain na Italia kufanya vizuri katika Europa league na UEFA Champion League. Huu ndio wasifu wake

Yule dogo Kelvin John mbona huwa hamumuiti?
Au hajafikia umri wa kucheza taifa stars utasikia wanasifia sana kwenye magazeti halafu stars hola...naamini vijana wanatakiwa kupewa nafasi sasa sio kukariri wachezaji wazee tu...spain imefanya vizuri hivi karibuni ikiwa na kikosi cha vijana wengi na wakongwe wachache....kocha awe anamuanzisha benchi Samata ili apate uchungu wa kupambana.
 
Back
Top Bottom