Kikosi cha Serengeti Boys kilichoibanjua Shelisheli ndicho kuanza kesho

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
serengeti-boys-2016_xdanl02rzd9h1iao9ghn6qgvm.jpg

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, Bakari Nyundo Shime, amesema hatarajii kuwa na mabadiliko makubwa ya kikosi katika mchezo dhidi ya vijana Shelisheli utakaopigwa kesho Jumamosi Julai 2, 2016 kwenye Uwanja wa Stade Linite mjini Victoria.

“Timu haitakuwa na mabadiliko makubwa. Almost kikosi kitakuwa ni kilekile cha Dar es Salaam kwa sababu nitampumzisha Job (Dickson Nickson) tu katika mchezo wa kesho, na nafasi yake atacheza Enrick (Vitalis Nkosi),” amesema Shime leo Julai 1, 2016 kabla ya kwenda kwenye mazoezi ya mwisho yatakayofanyika Uwanja wa Linite.

Soma zaidi hapa => Kikosi cha Serengeti Boys kilichoibanjua Shelisheli ndicho kuanza kesho | Fikra Pevu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom