kilagalila
JF-Expert Member
- Nov 8, 2018
- 320
- 154
Kamishna wa operesheni na mafunzo ya jeshi la polisi nchini NSATO MARIJANI akiwa na wataalamu wengine wa intelijensia wamefika mkoani Njombe ili kuungana na jeshi la polisi mkoani humo katika kupambana na mauaji dhidi ya watoto wadogo.
kikosi hicho maalumu kimewasili mkoani Njombe Ikiwa ni siku moja imepita tangu naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi amuagize IGP SIMON SIRRO kutuma kikosi maalumu cha kiintelijensia kuongeza nguvu katika uchunguzi wa watekaji na wauaji wilayani Njombe.
Akizungumza katika mkutano wa dharura na wananchi katika kituo kikuu cha mabasi mkoani Njombe mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka wakati akitamburisha kikosi hicho kilichosheheni wataalamu mbalimbali kutoka vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama nchini amewataka wananchi kutoa ushirikiano ili kuwabaini wahusika wa maovu hayo huku akidai hakuna mtu atakae achwa salama kama amehusika na mauaji.
"Naamini kwa sasa zoezi la kuwapata wahusika wote itakamilika mapema na kazi hii itafanywa kwa namna ambayo mtaiona hasira ya serikali yenu kwa wendawazimu hawa,serikali ya dk.JOHN POMBE MAGUFULI haitakubali damu ya mtanzania aendelee kuumia hapa kwa kisingizio chochote mufilisi"Olesendeka aliwaambia wananchi
Katika mkutano huo pia Olesendeka amemuagiza kamanda wa polisi mkoa wa Njombe RPC Renatha Mzinga kumkamata mara moja aliyekuwa mratibu wa tiba mbadala na asilia mkoa wa Njombe ,baada ya kulalamikiwa na waganga wataalamu wa tiba asili na mbadala kuwa amekuwa chanzo cha kusababisha migogoro katika chama chao pamoja kufanya usajiri holela wa waganga hao.
Nae kamanda wa kikosi hicho maalumu Nsato Marijani ambaye ni Kamishna wa operesheni na mafunzo wa jeshi la polisi nchini alisema kuwa kikosi hicho kimekuja kwa kazi ya kuwasaka wahusika wa mauaji na kwamba kitawasaka popote walipo kwa hiari au shari.
"Naamini kabisa sisi sote tuliopo hapa tutashirikiana katika kufanya kazi na tukifanya kazi kwa ushirikianao haiwezekani mtu akajificha labda atajificha kwenu kwasababu mmoja wenu hataki kutoa taarifa,sasa mimi nitapata taarifa kwa hiari au kwa shari lakini nikipita huko kwa shari wapo wengine watu wema watakaoumia sasa ili wale wema wasiumie ni heli tukatoa taarifa mapema ili mimi nikashughulika na wale wabaya"alisema kamishna MARIJANI
Kwa upande wananchi wanapongeza serikali kwa kuchukua hatua za haraka za kukabiliana na vitendo hivyo vya ukatili dhidi ya watoto.
MC.AMIRI/MR.MTAANI