Kikongwe amlilia Rais Magufuli Mwenyekiti wa kijiji anataka nife

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Kikongwe wa miaka 94 mkazi wa Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara Martha Kuzilwa amuangukia Mh Rais Magufuli kuingilia kati tena maisha yake Mara baada ya kutishiwa kifo na Mwenyekiti wa serikali ya kijiji wakishirikiana na mtendaji wa kata ya Nasinyai kumpora Ardhi yake na kuuza kwa nguvu kwa matajiri

Kikongwe uyu amesema Mwenyekiti wa kijiji kwa kushirikiana na mtendaji wa kijiji kwa pamoja wamemtaka kuachia shamba lenye ukubwa wa ekari 300 na kutafuta makazi mapya kwakua yeye sio mmasai ni mkabila wa kuja

Amesema mpaka sasa amesha tishiwa maisha na kunusurika kufa Mara baada ya kuvamiwa na Mwenyekiti akishirikiana na kamati ya serikali ya mtaa na wajumbe wake wote kumtishia maisha endapo ataondoka katika eno hilo.

''Nimenusurika kupigwa panga la uso na vijana ambao ni watoto wa Mwenyekiti wa kijiji chetu cha nasinyai wakilazimisha niondoke eneo hili namuomba Mh Rais anisaidie kwani Nina maisha magumu sana na Mimi ni mjane alisema Martha Kuzilwa kikongwe wa miaka 94

Mh Rais Magufuli alimaliza mgogoro huo na kuagiza kikongwe kupewa eneo hilo lakini mpaka sasa kumekua na sinto fahamu ya kupewa eneo lake na kumwomba Rais Magufuli kuingilia kati tena kwani sasa viongozi wa kijiji wanataka kukatiza Maisha yangu



IMG_20201218_113156_0.jpg
IMG_20201218_120853_5.jpg
InShot_20201218_154142254.jpg
IMG_20201218_120842_8.jpg
 
Polepole yupo live jmosi,watumishi wanaojidai dai watanikoma,lazima niwaripue dadadeki
 
Back
Top Bottom