Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 749
- 1,797
Kikongwe mwenye umri wa Miaka 94,Ndesinio Ndewario Nko Mkazi wa Kijiji cha Nkoaranga,Wilayani Arumeru ,Mkoani Arusha,amemwomba rais John Magufuli kumsaidia kupata eneo lake baada ya kushinda kesi mahakamani lakini uongozi wa wilaya umeshindwa kutekeleza amri ya Mahakama.
Akiongea kwa uchungu na vyombo vya habari ,Ndesinio alisema kuwa alishitakiana na mtoto wake aitwaye Emmanuel Nko ambaye aliuza kinyemela eneo hilo lenye ukubwa wa ekari moja lililopo eneo la Kiwawa wilayani humo.
Alisema katika kesi mbalimbali zilizounguruma kuanzia baraza la Ardhi la Kata,baraza la wilaya, Mahakama kuu na Mahakama ya Rufaa alishinda na Mahakama hizo kumtambua yeye kama mmiliki halali wa eneo husika.
Kikongwe huyo alieleza kuwa kijana wake huyo aliuza eneo hilo kinyemela mwaka 2012 kwa Ester Palangyo (Mama chai Jana) mkazi wa Maji ya chai wilayani humo bila kuishirikisha familia wakati akijua si Mali yake nani kinyume cha sheria.
Baada ya kumalizika kwa kesi hiyo ,Mahakama ya rufaa ilitoa maelekezo kesi hiyo irejeshwe baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ambao walitekeleza amri ya mahakama ya rufani kwa kukabidhi eneo kwa mdai.
Baraza hilo la Ardhi na Nyumba la wilaya la Arusha lilimwandikia barua Mkuu wa wilaya ya Arumeru yenye kumbukumbu namba DLHT/MISC.APP.NO.48 ya mwaka 2013 kuitambulisha kampuni ya udalali ya REGIZ COMPANY LTD kwa ajili ya utekelezaji wa Amri ya baraza katika shauri namba 48/2013 ya mdai Ndesinio Ndewario dhidi ya mdaiwa Immanuel Ndewario Nko.
Alisema kuwa Kampuni ya udalali ya Regiz kupitia barua yake yenye kumbukumbu namba RGZ/AR/48/2020 ilitekeleza hukumu ya shauri hilo namba 48/2013 ikiwa ni pamoja na kuondoa nyumba zilizokuwa zimejengwa na kumkabidhi mdai mbele ya watendaji wa ofisi ya kata ya Imbaseni.
Bibi huyo alidai kwamba julai 23,2020 alipokea barua kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Jerry Muro yenye kumbukumbu namba DC/ARUM/W.10/1XL/62 ya kusitisha kufika katika eneo hilo jambo ambalo amedai ni ukiukwaji wa amri ya Mahakama na kumtaka rais John Magufuli kuingilia kati na msaidia kupata eneo lake kwani ofisi ya Mkuu wa wilaya inajinufaisha kupitia mgogoro huo uliokuwa umemalizwa na Mahakama.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akiongelea suala hilo ofisini kwake alisema kuwa ni kweli ofisi yake imesitisha utekelezaji wa Amri hiyo ya mahakama baada ya kuwepo kwa viashiria ya uvunjifu wa amani.
Akiongelea suala hilo alisema kuwa hawezi kutekeleza amri ya sasa inayotoka baraza la Ardhi wakati kuna amri nyingine ya nyuma ya Mahakama kuu juu ya shauri hilo ambayo ulitolewa na ilikuwa haijatekelezwa.
"Hapa lazima muelewe kwamba kuna amri mbili zilizotolewa na mimi naanza kutekeleza amri ya Mahakama ndio maana nimesitisha kwanza amri ya sasa ya baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya "alisema Murro
Kabla ya kusitisha kwa Amri hiyo Mkuu huyo wa wilaya aliwahi kusaini hati ya utekelezaji wa Amri ya Baraza Kupitia barua ya kampuni ya udalali ya REGIZ yenye kumbukumbu namba RGZ/MB/AR/48/2020 iliyosaimiwa Mei 19 ,Mwaka huu 2020.
Ends.....