Kikombe cha chai

decomm

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
726
655
MBEYA VIJIJINI

Mwalimu 'mwenyeji' wa darasa la kwanza ameandika ubaoni:-

"Kikombe cha chai"

Mwalimu anawaambia wanafunzi:-

Mwalimu: 'wanafunzi somemi ubaoni'
Wanafunzi: 'Ikikombe kya kyai'

Mwl: 'Hapana siyo ikikombe kya kyai, semeni ikikombe kya kyai'

Mwl: 'Haya someni wote'
Wanafunzi: ' Ikikombe kya kyai'

Bahati nzuri kukawa na mwanafunzi mgeni aliyetoka mkoa mwingine. Akanyoosha kidole.

Mwl: 'Enhe wewe mwanfunzi mgeni unasemaje?'
Mwanafunzi: 'Samahani mwalimu, inatamkwa KIKOMBE CHA CHAI'

Mwl: 'Sawa kabisa, mmemsikia mwenzenu amesoma vizuri?'
Wanafunzi: 'Ndiyoooo'
Mwl: 'Enhe, someni wote'
Wanafunzi: 'Ikikombe kya kyai'
Mwl: 'Aaaargh! Siyo IKIKOMBE KYA KYAI, semeni ikikombe kya kyai!
Wanafunzi: 'Ikikombe kya kyai'
_____

Ulimi ukielemewa na lahaja, kutamka maneno ya lugha nyingine mara nyingi inakuwa si rahisi kutamka sawasawa.

decomm!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom