Kikokotoo cha kustaafu kisilete ubishi

Hakuna ambae hatastaafu kazi, kesho kama sio wewe utakaestaafu basi atastaafu baba yako, shangazi, babu, mama mkubwa, dada, kaka, mama, baba mdogo, jirani nk. Hivyo, haki lazima itendeke hata kwa anaeachishwa au kuacha Kazi mwenyewe apewe chake.

Kitu cha msingi ni elimu ya kustaafu kazi itolewe kwenye mitaala yetu ya sekondari ili kila MTU bila kujali anafanya Kazi gani afahamu namna ya kushughulikia kustaafu kwake Kazi.

Kila mfanyakazi na kila kijana wa Leo lazima afahamu kuwa iko siku siku atazeeka na kushindwa kufanya hiki anachokifanya Leo kupata chakula, malazi, mavazi, matibabu na starehe, hivyo aanze kuanzia sasa kuwaza na kuchukua hatua juu ya namna atavyopata chakula, malazi, mavazi na matibabu yake siku akiacha Kazi kwa uzee au ugonjwa, au kuachishwa Kazi.

Kikokotoo kisiwe na mizengwe ndani yake, kikokotoo lazima kijikumbushe kuwa hata hii misharahara wanayopewa watumishi Leo ni midogo sana kuliko uhalisia, wanapunjwa sana sana sana. Hii sio mishahara bali ni posho tu wanapewa. Hivyo kikokotoo kilenge pia kurekebisha athari za mishahara mishahara midogo wanayolipwa watumishi.

Hivyo hakuna mtumishi awe waziri, mbunge, mkuu wa majeshi au mwalimu asiyetaka kikokotoo kinachompa ahueni pale atakapostaafu.
Halafu Watumishi wa Umma wanaokwenda kupewa Mafao ya Kikokotoo kuanzIa July 2022 hawakupewa Nyongeza ya mshahara miaka 6 wala kupandishwa madaraja. Kikokokotoo kinaenda kuwapeleka kwenye Umaskini wa Uzeeni kama walivyoishi kimaskini kwa mishahara kiduchu. Kama Serikali ndio imepandisha Mshahara July 2022 kwa nini wasisubiri effect ya Nyongeza ya Mishahara itunishe Pensheni za Wastaafu at least 3 years ndio Kikokotoo kama lazima. TUCTA CWT, TUGHE mko wapi?
 
Wawape TU hela Yao yote, kama mshahara hautoshi vipi pension ya kikokotoo? Kwani wakulima Wanapewa pension? Miaka 6 mtu hajapandishwa mshahara Wala daraja na mnajua namna pension inavyokokotolewa, na kikokotoo kinanza July mosi. Huko ni kudharau wananchi.
 
Pe
Uharibifu alofanya bwana yule kwa miaka 5,utatuvhukua zaidi ya miaka 50 kurekebisha!! Alaaniwe huko alipo
Pension inamaana kama mshahara wako ulimudu kukupatia nyumba, shamba, trecta, ghala la kuhifadhia mazao, lori na kusomesha watoto wako. Watu wanataka hela Yao kwa mkupuo kwakuwa mishahara ya miaka 40 ilishindwa kumuandaa kustaafu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom