Kikibaki chama kimoja ndio Upinzani wa kweli utaposhika hatamu

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
11,192
15,892
Sasa hivi ili uwe mwana CCM wa kweli na mzalendo basi ni lazima ukitetee chama chako cha CCM dhidi ya Wapinzani na kuwapinga katika hoja zao.

Jambo hili linafanya wapinzani wahangaike katika kukosoa mambo ya maendeleo kweli wakati huo chama tawala wanahangaika katika kusifia tu na kuwajibu wapinzani.

Itakapofikia hatua ya chama kuwa kimoja hapo sasa hakutakuwa na mpinzani wa kunyooshewa vidole ili wewe mnyoosha vidole uonekane unajali maslahi ya chama na taifa.

Hapo sasa ndipo watu wa chama hiko watatafuta nafasi ama cha kusema ili waonekane wazalendo wa kweli katika nchi ama katika chama.

Hapo sasa ndipo ukosoaji wa ndani ya chama utaanza na watu wataanza kukosoa ili waonekane wanapenda maendeleo ya kweli.

Kila mmoja atataka kuongea aonekane kaongea na mtaka maendeleo, jambo hili litafanya mambo mawili yatokee.

1. Ikiwa rais aliyeko atakuwa ni dikteta na mgumu atawafukuza uwanachama hawa watu kwa sababu ni kikwazo katika tawala yake.

Na hii inaweza kupelekea kuundwa kwa chama kingine tena cha upinzani ambacho kitakuwa na vikwazo vingi sana kutokana na asili yake ile ilikotoka.

2. Ikiwa ni raisi poa atamuacha aendelee huyu mtu na atazidi kukubalika na wanachi na hapo wengine wataona kuwa kumbe hii ni njia ya kukubalika kwa wanachi na chama changu hakichukui hatua yeyote,na hapo wengine wataanza kujitokeza kuanza kukosoa zaidi na zaidi.
 
Nakubaliana na wewe kwa sasa hakuna upinzani wa kweli bali kuna wababaishaji tu.
Huu ni upinzani lakini sasa haiwezi kuwa na nguvu kwa sababu kuna ambao wanatumia upinzani wao kuonesha na kuvuna uzalendo.
 
Inawezekana umri wako ni mdogo sana! Unakotaka ndiyo tumetoka miaka siyo mingi, tahadhari usiturudishe huko acha tusonge mbele, watu walihangaika sana kuondoka huko! P/se.
 
Baadaye mtataka ukoloni na hatimaye uchifu urudi! Vijana bunini vitu vipya vizuri, msitamani kurudi kwa mababu zenu, someni historia chukueni machache mazuri!
 
Baadaye mtataka ukoloni na hatimaye uchifu urudi! Vijana bunini vitu vipya vizuri, msitamani kurudi kwa mababu zenu, someni historia chukueni machache mazuri!
Kwani hapa ambapo hakuna ukoloni mbona lawama ni zile zile tu kmaa zile za ukoloni katika kushika madaraka ?

Unadhani nini tatizo ?
 
Kwani hapa ambapo hakuna ukoloni mbona lawama ni zile zile tu kmaa zile za ukoloni katika kushika madaraka ?

Unadhani nini tatizo ?
Tatizo watu wengi hasa wazee walio kwenye tawala wana tamaa, wanaona ile hali inawasaidia wao kubaki madarakani. Hawako tayari kushindana kwenye demokrasia ya sasa! Boresheni msirudi nyuma ambako tuliimba zidumu fikra za mwenyekiti.
 
Je hilo la kuwa wazee wa sasa wanatamaa na hawako tayari kuachia madaraka je jambo hili wakoloni hawakuwa nalo ?
 
Itakapofikia hatua ya chama kuwa kimoja hapo sasa hakutakuwa na mpinzani wa kunyooshewa vidole ili wewe mnyoosha vidole uonekane unajali maslahi ya chama na taifa.

Huko tumetoka juzi tu hatuwezi kurudi tena bila kulazimishwa. Mungu wetu alipo tuumba alituwezesha na kutujenga tuwe na mawazo tofauti kama hiyo ni kweli si vizuri kutulazimisha tuwe na chama kimoja.

The iron rule of oligarchy inatueleza ndani ya chama kutaibuka kundi la watu ambao watakinasa chama ikimaanisha wenye mawazo tofauti watapigwa kitasa. Vyama vingi ni njia mojawapo ya nchi kupumuakisiasa. Hivyo mkuu unachotaka ni kuturudisha nyuma na kuleta mfarakano.

Kuna kundi hapa nchini bado hawaja amini kuwa tunatakiwa kuwa na utawala na katiba inayoruhusu vyama vingi. Katiba yetu na watawala bado wanamentality ya chama kimoja.
 
Huko tumetoka juzi tu hatuwezi kurudi tena bila kulazimishwa. Mungu wetu alipo tuumba alituwezesha na kutujenga tuwe na mawazo tofauti kama hiyo ni kweli si vizuri kutulazimisha tuwe na chama kimoja. The iron rule of oligarchy inatueleza ndani ya chama kutaibuka kundi la watu ambao watakinasa chama ikimaanisha wenye mawazo tofauti watapigwa kitasa. Vyama vingi ni njia mojawapo ya nchi kupumuakisiasa. Hivyo mkuu unachotaka ni kuturudisha nyuma na kuleta mfarakano.
Kuna kundi hapa nchini bado hawaja amini kuwa tunatakiwa kuwa na utawala na katiba inayoruhusu vyama vingi. Katiba yetu na watawala bado wanamentality ya chama kimoja.
kwani mkuu ikiwa vyama ni vingi na kiongozi hataki mawazo tofauti na anatumia dola kuzuia mawazo hayo unadhani huo mfumo wa vyama vingi utasaidia kutufikisha tunapopataka ?
 
kwani mkuu ikiwa vyama ni vingi na kiongozi hataki mawazo tofauti na anatumia dola kuzuia mawazo hayo unadhani huo mfumo wa vyama vingi utasaidia kutufikisha tunapopataka ?
Kama siyo "uKondoo wa Nyerere" nguvu ya umma inaweza kutumika kuinyoosha serikali, kwani katiba inatambua uwepo wa vyama vingi.
 
Kama siyo "uKondoo wa Nyerere" nguvu ya umma inaweza kutumika kuinyoosha serikali, kwani katiba inatambua uwepo wa vyama vingi.
nguvu ya ummah kwa nini ilishindwa kuinyoosha ukondoo wa nyerere tokea hapo mwanzo ?
 
Kuwe na upinzani wa kweli au la, inategemea na kujitambua kwa wananchi.
Wananchi wasiojua hata haki zao za msingi ni zipi, angalau wazitetee, upinzani utawaambia nini wakati chama tawala kinawaminya (uhuru na haki mbalimbali kusiginwa) na kuwapuliza (kupeleka huduma mahsusi kwa kundi la wananchi licha ya kuwa ni haki yao na ni wajibu wa serikali)
Chama kimoja kiongozwe na malaika ambazo kwa dhati watajiwekea mpaka na kuwakumbuka walalahoi, lakini kikiongozwa na mashetani, basi wananchi wajue hawana lao, sheria kandamizi kwa wananchi na za kuwatetea watawala ndio zitakazotungwa, majeshi ya kuwatumia na kuwaadhibu wananchi na kulinda maslahi ya watawala, mishahara na posho za ajabu kwa watawala, kwa wananchi mkia wa mbuzi.
 
Back
Top Bottom