Kikatiba, Urais wa Tanzania ni miaka mitano (5)

Raisi anaweza kutawala miaka 5 tu kwa mujibu wa katiba, miaka mingine 5 ni kama chama chake kitampitisha na kama p[ia atashinda uchaguzi kwa kura ndio atakuwa raisi kwa awamu ya 2 na mwisho!
 
Rais, akiwa na nia, sababu na wito wa kututumikia tena, atagombea tena mwaka 2020 na, kwa mazuri yake, tutamchagua tena. Kama wananchi tukiona hatoshi, tutamkataa kwa njia ya kura. Nasisitiza kuwa Urais ni miaka 5 na si miaka 10. Miaka 10 hutokana na utendaji mzuri wa Rais na nia yake ya kutaka kutuongoza tena.
Kwani tatizo lako nini?
Mbona hujakionesha kifungu kinachosema Rais atatumikia si zaidi ya vipindi viwili vya miaka kumi?vifungu hivyo vinasomeka sambamba lakini umeamua kukificha ili ufikie malengo yako ya kuwatoa watu kwenye reli
 
nakubaliana nawe mtoa hoja ,tatizo toka nchi yetu ianze hii systems of so called uchaguzi wa vyama vingi,chama dola kimeendelea kushinda na wagombea wake wamekuwa wanatumikia miaka kumi,mazoea yamekuwa sheria,as far as mfumo uliopo utaendelea our no 1 atachaguliwa tu kuwa rais,maana huyu bila shaka atagombea na kivuli kama ilivyokuwa Rwanda,tuangalie democracy za wenzetu pale Kenya,then Angola na watch out for tomorrow vote of no confidence against president Zuma,its pure democracy in the making.
 
Kikatiba na kimantiki, Urais ni miaka mitano. Lakini, kama haki iliyotolewa na Katiba, aliyekuwa Rais kwa muhula mmoja uliokwisha aweza kugombea na kuchaguliwa tena. Kuchaguliwa kwake mara ya pili kutakuwa ni mara moja tu. Ndiyo kusema, kama Rais amechaguliwa tena, ataishia miaka kumi (10) madarakani.

Rais, akiwa na nia, sababu na wito wa kututumikia tena, atagombea tena mwaka 2020 na, kwa mazuri yake, tutamchagua tena. Kama wananchi tukiona hatoshi, tutamkataa kwa njia ya kura. Nasisitiza kuwa Urais ni miaka 5 na si miaka 10. Miaka 10 hutokana na utendaji mzuri wa Rais na nia yake ya kutaka kutuongoza tena.

Umeshindwa vipi kusema: kwa mujibu wa katiba, muda wa chini wa Urais ni miaka mitano na ule wa juu ni miaka kumi. Na Rais anaweza kufikia ukomo endapo atachaguliwa kwa kipindi kingine kimoja. Kwa maana hii Rais anaweza kukaa madarakani kwa muda wa miaka mitano au miaka kumi. Hivyo katiba inatamka muda wa juu au ukomo wa mtu kuwa Rais.

Unaposema muda wa Rais ni miaka mitano, ni kwamba umeshindwa kufanya tafsiri ya kifungu au vifungu kwa ufasaha yaani logic ikiwemo na probability.
 
Naziacha ibara za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (kama ilivyofanyiwa marekebisho mara kwa mara) ziseme zenyewe.

Ibara ya 42 (1):

42.-(1) The President elect shall assume office of President as soon as

possible after it is declared that he has been elected President, but in any event he

shall assume office before the expiration of not more than seven days.

Ibara ya 42 (2):

(2) Unless he sooner resigns or dies, the President shall, subject to sub

article (3), hold office of President for a period of five years from the date on

which he was elected.

Ibara 42 (3):

(3) A person elected President shall hold the office of President until -

(a) the day his successor in office takes the oath of office;

(b) the day he dies while in office;

(c) the day he resigns from office; or

(d) he ceases to hold the office of President in accordance with the

provisions of this Constitution.

Ibara ya 40 (1) na (2):

40.-(1) Subject to the other provisions of this Article, any person who

holds office as President shall be eligible for re-election to that office.

(2) No person shall be elected more than twice to hold the office of

President.

Kikatiba na kimantiki, Urais ni miaka mitano. Lakini, kama haki iliyotolewa na Katiba, aliyekuwa Rais kwa muhula mmoja uliokwisha aweza kugombea na kuchaguliwa tena. Kuchaguliwa kwake mara ya pili kutakuwa ni mara moja tu. Ndiyo kusema, kama Rais amechaguliwa tena, ataishia miaka kumi (10) madarakani.

Rais, akiwa na nia, sababu na wito wa kututumikia tena, atagombea tena mwaka 2020 na, kwa mazuri yake, tutamchagua tena. Kama wananchi tukiona hatoshi, tutamkataa kwa njia ya kura. Nasisitiza kuwa Urais ni miaka 5 na si miaka 10. Miaka 10 hutokana na utendaji mzuri wa Rais na nia yake ya kutaka kutuongoza tena.
Nkuunga mkono kwa kusisitiza hili jambo maana naona bado ile nia ya dhati ya kuondoka bado haipo. Waliong'ang'ania madarakani walianza hivi hivi tu wala si tofauti. Huwa wanaanza kwa kusema wataheshimu katiba. Lakini mimi natofautiana na kauli ya rais kwamba "muda wangu wa miaka kumi..." Ni nani amemwambia ana miaka kumi? Angesema mimi nawatumikia kwa miaka mitano tu, mkiona nafaa katiba inaniruhusu miaka mingine mitano. Kwa namna alivyoitoa hiyo kauli ni kama vile hatakiwi kupingwa kwa namna yoyote ile na ndo maana inatumika nguvu kubwa sana kusupress possible dissidents. Kw mtu muadilifu kabisa kabisa, hatakiwi kuchukia wanaotaka kupambana naye baada ya miaka mitano.
 
Kwani tatizo lako nini?
Mbona hujakionesha kifungu kinachosema Rais atatumikia si zaidi ya vipindi viwili vya miaka kumi?vifungu hivyo vinasomeka sambamba lakini umeamua kukificha ili ufikie malengo yako ya kuwatoa watu kwenye reli
Mkuu,lugha ya Malkia haipandi? Soma Ibara ya 40
 
Kwani tatizo lako nini?
Mbona hujakionesha kifungu kinachosema Rais atatumikia si zaidi ya vipindi viwili vya miaka kumi?vifungu hivyo vinasomeka sambamba lakini umeamua kukificha ili ufikie malengo yako ya kuwatoa watu kwenye reli
Nahisi una matatizo ya kusoma taharifa mpaka mwisho ukiangalia chini kabisa amezungumzia ibara ya 40(2)
 
Ni kweli. Hata kama ukitoka Dar kwenda Mbeya, kutoka Dar utakutana na vibao vinavyokuonesha KM zilizobaki ufike Moro, Ukitoka pale utakuta na kibao kinachokuonesha km zilizobaki ufike Iringa, na ukitoka pale utakutana na kibao kinachokuonesha KM zilizobaki kufika Mbeya... Mgawanyo huo haondoi maana kuwa in total safari ya Dar mpaka Mbeya ni KM fulani...
 
Hoja za miaka hii ni nzito kweli kweli, huku Lissu anatoka povu waziri kasema anaipenda kazi yake, wanasheria wasomi nao wanatufafanulia katiba kuhusu ukomo wa urais. Aliyemficha Slaa tafadhali mrudishe.
 
Back
Top Bottom