Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,679
- 149,864
Kwa upande wa Tanzania bara,kama sikosei,kuna muda maalumu wa Kikatiba kutangaza matokeo ya uraisi tangu tarehe ya kufanyika uchaguzi na pia kuna muda maalumu wa Kikatiba (siku 7 kama sikosei)ambapo Raisi Mteule anapaswa kuwa ameapishwa ndani ya muda huo tangu kutangazwa mshindi.
Sasa wadau,leo hii Zanzibar imeshapita miezi miwili na siku kadhaa tangu uchaguzi ufanyike na Raisi Mteule hajatangazwa,je hapa hapatakuwa na mgogoro wa Kikatiba?Kama upo,utamalizwaje?
Sitashangaa katikati ya maandalizi ya kumtangaza mshindi wakaibuka watu na kwenda mahakamani kupinga mshindi kutangazwa mpaka pale mahakama itakapotoa tafsri ya kikatiba juu ya jambo hili.
Huu naona unaenda kuwa mgogoro juu ya mgogo na ambao utabidi umalizwe bila kuangalia katiba inasemaje vinginevyo suluhu inaweza kuwa ngumu kupatikana unless katiba ya Zanzibar haijaweka mashariti ya aina yoyote katika swala hili.
Sidhani kama katiba ya Zanzibar na ya Bara zinatofautiana sana katika swala hil.Mnaoijua katiba ya Zanzibar mtusaidie hapa.

Last edited: