Kikao kati ya CHADEMA na Serikali (Ikulu) chaisha, makubaliano haya hapa!

kwa jinsi alivyo makini, John Mnyika hawezi kusaini document kwa peni ya blue. Kama ni kweli atakuwa ameteleza.

na swali langu linabaki palepale. Mnyika ni Naibu Katibu Mkuu wa CDM?
 
Ukweli ni kubwa sheria yaweza kusainiwa na Rais kama haina vitu ambavyo say vinapingana na katiba ya sasa... lakini wabunge e.g. wa CHADEMA wanaweza kupeleka hoja ya amendment kwenye bunge la January.... So ku-signiwa kwa sheria sio mwisho ya sheria kubadilishwa au kuhuishwa.


Mungu Ibariki Tanzania
Kwanini huyu mtu anaitwa Pasco huwa anakuwa sahihi mara nyingi sana?!

Ikishasainiwa kuwa sheria na sheria hiyo kuanza kufanya kazi,kuifanyia marekebisho ni another fight that will take more time...The fight that once again the obstacle is the "Anna Makinda" factor,and the majority from CCM,walishasema kuwa parliamentary fight is unwinnable!

Ndiyo maana hawaku exhaust kifungu cha 86 na wakaamuwa kwenda kumwona JK...

Halafu pia walishakubaliana kuwa hata hii iliyopo ni nzuri tu,nachelea kusema wasije wakakosa la kuwaambia wananchi...

Duh!

Yangu macho...
 
mimi sielewi, kuboresha kivipi wakati akisaini itakuwa sheria?siku mbili wanajadili mambo hayo mawili ya dk 5tu? walienda kunywa chai tu.....
 
kwa jinsi alivyo makini, John Mnyika hawezi kusaini document kwa peni ya blue. Kama ni kweli atakuwa ameteleza.

na swali langu linabaki palepale. Mnyika ni Naibu Katibu Mkuu wa CDM?
Nadhani ni third on line after Zitto?
 
Huu unaweza kuwa mwanzo mzuri wa mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya. Serikali kukiri kwamba sheria ile inaweza kurekebishwa kabla haijasainiwa inaweza kuwa habari njema mbeleni

Kaka ww ni kiongozi wa Chadema sasa inakuwaje mnatuletea habari nusu nusu. Halafu mlitangaza kutokumtambua JK kama Rais wa JMT imekuwaje leo mmemfuata Ikulu tena nyie wenyewe halafu mnakuja na habari nusu nusu hapa sisi tuwaelewe vipi bana au na nyie mnataka kuwa CCM - C?
 
Kweli JK kiboko , mbwembwe zote za cdm mwishowe wameishia kuandika paragraph 2 tu , na wametoka wanafurahi kwa kunywa chai ya ikulu, juice nakupiga picha na Rais.

Kweli timu hii ifuatayo ya Chadema ni ya kuandika paragraph 2 tu??? semeni nanyi hamko seriouss na suala hili la katiba na uamuzi wenu wa kuonana na Rais mlikurupuka.

Timu ya Chadema : Philman Mbowe ( Mwenyekiti ), Said Arfi ( makamu mwenyekiti bara), Said Issa Mohammed (makamu mwenyekiti zanzibar), Prof. Mwesiga Baregu, Prof. Abdallah Saffari (washauri wa masuala ya siasa), Tundu Lisssu (mnadhimu wa kambi ya upinzani), John Mrema. Timu yote hii na vigogo then paragraph 2, kwa siku 2, ur joking !

Kwani taarifa ya Ikulu wanaandika CHADEMA. Hizo para2 zimebeba maelezo mengi mno.
Kwanza: Kwa jinsi JK alivyozungumza na wazee wa DSM, hataki kuonekana alichemsha
Pili: Maana ya sheria kuborehswa inaeleweka - ni kupeleka marekebisho bungeni. How serious the government is in this shall be known in Jan/Feb 2012 katika kikao chake kama kuna mswada wa marekebisho.

Hata hivyo ni ukweli usiopingika kuwa CDM wamenyang'anywa hoja. Maana ni juu ya serikali kucheza na maneno yaliyoko kwenye barua hiyo watakavyo. Kama CDM wataamua kuendelea na maandamano, Ikuli itasema waoneni wabaya hao --- Tulikubaliana hivi sasa wanafanya hivi.

Mimi nawashauri makamanda wakae watafakari vyema yote waliyoongea yakiwemo na yale ambayo hayajawekwa kwenye taarifa hii. Kisha wafanye maamuzi ya busara.
"Failling in one area is just a knowledge that - that option does not work."
 
I feel very sorry for this thead b/se my mobile fail to download the attachment! Very sorry!!?
 
Tafakari hapo, kuwa kwa upande wa serikari anasain Nchimbi na upande wa chdm anasain Mnyika, hapo maana yake nn? Na uzito wa jambo lenyewe ni upi?,, tusubiri taarifa lakini kuna picha inaashiria ki2 fulani pale ambacho ni cha kawaida saana, tusitegemee mabadiliko sana.
username hii kiboko,nimekumbuka mbali sana
 
Maswali ambayo bado nasubiri majibu kutoka CDM ni haya;
  1. Mbona Maneno kudumisha muafaka wa Kitaifa yamerudiwa katika paragrph zote mbili???
  2. Kwa nini hiyo taarifa imekuwa signed na Nchimbi na Mnyika wakati mazungumzo yaliongozwa na JK (upande wa serikali) na Mbowe (CDM).
  3. Kwa nini wananchi tusitilie mashaka haya makubaliano wakati tushashuhudia makubaliano ya design hii kati ya CCM na CUF ZNZ??
Dhu, after two days........................... one page with only two paragraph????
 
KAMA HAYO NDIYO MANENO YA JK THEN, SASA NDIPO NIMEELEWA RASMI KWA NINI KIPANGA[Dr. W.P.S] HAKUHUDHULIA HUO MKUTANO!!

Kikwete: Kwanza napenda kuwashukuru kwa kuonesha njia njema kabisa ya Kuzungumzia Mustakabali wa
Katiba ya nchi yetu. Kwa kweli nimefarijika sana na ninawapongeza sana kwa moyo wa kizarendo
Mliouonyesha.

Kikwete: Pili naomba tusahau yote yaliyopita hasa ukizingatia ukweli kwamba hata Glass Kabatini ugongana
Sembuse sisi binaadamu bwana, au siyo Bwana Mbowe.

Mbowe: Ni Kweli Muheshimiwa, lakini kwa Maslahi ya Taifa Letu, Kuna mambo ya Msingi ambayo si busara
Kuyasahu badala yake ni nyema kuendelea kuyakumbuka na kuyakumbusha mpaka pale yatakapopatiwa
Majibu ya uhakika.

Kikwete: Ni kweli, lakini ninachomaanisha ni kwamba kwa sababu tuko hapa kujadili mchakato wa kuandaa katiba
Mpya ni vyema tukasahau yote yaliyotokea apo nyuma kama Maswala ya CHADEMA kutoka nje ya Bunge,
Maswala ya Muswada ama kusomwa mara ya Kwanza ama Mara ya Pili Bungeni na hata Upitishwaji wake Bungeni
Ukizingatia kwamba Bado sijausign kuwa sheria nikitambua kwamba Mazungumzo yetu leo yanaweza kuboresha
zaidi mchakato huu kwa Maslahi ya Taifa.

LISSU: Samahani Mheshimiwa Rais, Kwani wewe binafsi umeuonaje mchakato mzima ulivyokwenda mpaka kufikia
Mswada huo kufikishwa kwako ili usainiwe kuwa sheria.

Kikwete: Tehe tehe tehe, LISSU bwana, tehe tehe tehe, aaaahaaaa. Unajua, haya mambo bwana, ndio maana
mimi nimesema hapa kwamba ni vyema tukasahau yaliyopita ama sivyo mazungumzo yetu yatakuwa mareefu
sana na mwisho wa siku watanzania watatushangaa wote.
Mimi, mimi, mimi dhamira yangu ni kuhakikisha kwamba, Katika mchakato wetu huu, hatufikii kwenye hatua
mbaya kama majirani zetu, sababu haya mambo ukianza kuyawekea maandamano na mihadhara mwisho wake
kwa kweli kabisa hauwezi kuwa mzuri.

Anakunywa Maji kidogo, kisha anaendelea
Pale Kenya pale, wakati wa mchakato wao damu imemwagika pale, sasa mimi siko tayari kuona hili linatokea hapa,
na ndio maana hata kwenye swala la madiwani wa arusha, mimi niliwaelekeza Waziri Mkuu na Katibu wangu Mkama
kuhakikisha Mnakaa, mnazungumza na kulimaliza hili, lakini kinachoendelea pale mi hata sikielewi nikiuliza naambiwa
tatizo ni Lema, vyombo vya habari kwanza vilikuwa vinasema tatizo ni Chitanda, sasa Chitanda simsikii tena
naambiwa tatizo ni Kamanda wa Polisi Zuberi na Mkuu wa Mkoa, mimi sielewi kabisa nini kinaendelea Pale, na hali
hii inachafua kabisa picha ya nchi yetu uko nje.

Anakunywa Maji tena.alafu
Pale Arusha Pale, kile ni kitovu cha Utalii nchini Mwetu, sasa Arusha tukiichezea itatualibia kabisa kabisa, ndio maana
mi nasema swala la Arusha tunatakiwa tukae kama hapa tuzungumze na kulipatia Muafaka. Hii nyumba tunajenga
wote kwa nini tugombee fito Jamani.

Mimi, mimi nasema, wakati tuko Kwenye kikao cha Kamati kuu Dodoma Pale, kuna watu walitaka kukataa nisionane
na CHADEMA, mi nikasema hapana, Lazima nionane nao hawa, kwa sababu hata mimi hili swala la Katiba mpya bado sijalielewa
vizuri.

Kwa hiyo mi nawashukuru sana kwa Moyo wa Uzalendo mliouonyesha, na niko tayari kuonana na nyie na kuzungumza
hata kwenye mambo mengine, sina tatizo hata kidogo na nyie, si unaona bwana, tumezungumza na hakuna mtu
ametoka damu, hii ndio watanzania wanataka kuona.

Mimi kwa kweli niwashukuru sana, na hizi ndio siasa za kizalendo kwelikweli, asanteni sana na karibu tena.
 
Huyu GB anawachezea akili nanyi mnatoka mapovu pasipo sababu ya Msingi. Mnaletewa taarifa haina hata uthibitisho ime originate toka wapi mnaanza kulumbana na anayeongoza kebehi ni huyo huyo mtoa mada.

Kwani mkiwa na subira ili CDM watoe tamko rasmi mtapungukiwa nini? CDM sio CCM, lazima watakuja na kauli ya kueleweka vizuri nasi tutajua kama wamekosea au wamejipanga sawasawa.
 
Kwani taarifa ya Ikulu wanaandika CHADEMA. Hizo para2 zimebeba maelezo mengi mno.
Kwanza: Kwa jinsi JK alivyozungumza na wazee wa DSM, hataki kuonekana alichemsha
Pili: Maana ya sheria kuborehswa inaeleweka - ni kupeleka marekebisho bungeni. How serious the government is in this shall be known in Jan/Feb 2012 katika kikao chake kama kuna mswada wa marekebisho.

Hata hivyo ni ukweli usiopingika kuwa CDM wamenyang'anywa hoja. Maana ni juu ya serikali kucheza na maneno yaliyoko kwenye barua hiyo watakavyo. Kama CDM wataamua kuendelea na maandamano, Ikuli itasema waoneni wabaya hao --- Tulikubaliana hivi sasa wanafanya hivi. Mimi nawashauri makamanda wakae watafakari vyema yote waliyoongea yakiwemo na yale ambayo hayajawekwa kwenye taarifa hii. Kisha wafanye maamuzi ya busara.
"Failling in one area is just a knowledge that - that option does not work."


HApo kwenye RED umehit kwenye POINT

:poa:poa:poa:poa:spy:
 
Huyu GB anawachezea akili nanyi mnatoka mapovu pasipo sababu ya Msingi. Mnaletewa taarifa haina hata uthibitisho ime originate toka wapi mnaanza kulumbana na anayeongoza kebehi ni huyohuyo mtoa mada.
Kwani mkiwa na subira ili CDM watoe tamko rasmi mtapungukiwa nini? CDM sio CCM, lazima watakuja na kauli ya kueleweka vizuri nasi tutajua kama wamekosea au wamejipanga sawasawa.


KUNA WATU HAWAMJUI GB

nAONA NA INVISIBLE KADAKIA au GB ndo INVISIBLE ??????????????????????????

hII documaa ni magumashi

Hawezekani press release wanawaweka na CDM
 
Ukisoma katikati ya mistari utagundua kuwa kuna mambo hawakutaka kuyaweka wazi; lakini mimi naona rais amekubali kurudi hatua fulani nyuma.

Ukisoma kifungu cha kwanza; ina maana kwamba bunge kupitisha siyo mwisho, bado kuna nafasi ya kuboresha, baada ya rais kusaini ali mradi utumikaji wa sheria uwe haujaanza. Maboresho hayo yatakuwaje ndipo tunakuja kifungu cha pili kwamba mawasiliano na mashauriano kati ya serikali na wadau mbalimbali juu ya kuboresha sheria hiyo yafanyike. Hapa wadau si ndio sisi - wananchi, jukwaa la katiba, dini mablimbali, NGOs wasomi nk.

Hii ni diplomatic language kwamba rais amekubali maoni ya wadau mbalimbali yaendelee kupokelewa! Mnajua kwa vyovyote vile isingewezekana kuandika wazi kuwa muswada unarudishwa kwa wananchi, hii ingemcontradict rais straight ukifikiria yale aliyozungumza na wazee wa dsm.
Lakufanya sasa sisi wadau kwa makundi yetu mbalimbali tuwasilishe hoja za kuboresha sheria hiyo.

Kumbuka hapa inaongelewa sheria, maana yake rais atakuwa ameshaisaini na kitakachofanyika ni serikali kuwasilisha bungeni muhtasari wa marekebisho kutegemea na hoja tutakazotoa sisi wadau - na hili ndilo Lisu aliliongelea isipokuwa sasa badala ya wadau kurudishiwa muswada uliosomwa kwa mara ya kwanza, tunarudishiwa sheria ili mawazo yetu yatumike kuiboresha kabla haijaanza kutumika.

Kama kweli rais atakuwa tayari (kama siyo usanii) kuiambia seriakali yake kuwa mawazo yetu yaingizwe kwenye marakebisho then tutakuwa tumefaulu.
 
Heshima kwenu wakuu!!
leo nipo a bit disappointed because from what I read, many of you have fallen in a "paragraph trap" - hii si kawaida kwa great thinkers!

Hiyo ripoti iliyosainiwa na Mheshimiwa J.J Mnyika pamoja na Nchimbi is nothing but a press release - sasa swali ninalotaka kuwauliza pseudo-critics, je hiyo taarifa kwa vyombo vya habari hisingetolewa ninyi mngeamini kwamba hawakujadili kitu??? Timu iliyotumwa na CHADEMA ilikuwa ni timu nzito ya watu ambao personally I could handle a blank checque - so I trust them blindly because their respective records speak!!!

Ushauri wangu kama mtaniruhusu ni kuwa wavumilivu na kusubiri habari zitakazoanza kutoka especially kwa upande wa CHADEMA, u and i know kwamba hakuna siri ya watu wawili - so just wait patiently and we'll know every detail of eventual agreement/disagreement they have reached - TRY TO THINK BIG!!!!

Curiosity, hivi humu ndani kuna watu wanaamini kuwa Dr, Hon. Lissu bila kusahau wengine wanaweza kuhongwa kwa chai za Ikulu??? You must be kidding - hao watu siwafahamu personally lakini records zao "zinatisha" - they are really fighters so let's have TRUST and above all RESPECT to those guys.

Thanks dudes!!!
 
Kama hizo ndo hoja walizokubaliana, hapo hamna kitu, changa la jicho hilo. Tuliahidiwa maisha bora kwa kila mtanzania, yako wapi? Hata katiba iliyopo inataja haja ya mabadiliko. Lakini anayedictate mabadiliko hayo ni mkuu wa nchi. Kwa hiyo hayo makubaliano ni kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa.
 
Back
Top Bottom