Kikao kati ya CHADEMA na Serikali (Ikulu) chaisha, makubaliano haya hapa!

Kikwete: Kwanza napenda kuwashukuru kwa kuonesha njia njema kabisa ya Kuzungumzia Mustakabali wa
Katiba ya nchi yetu. Kwa kweli nimefarijika sana na ninawapongeza sana kwa moyo wa kizarendo
Mliouonyesha.

Kikwete: Pili naomba tusahau yote yaliyopita hasa ukizingatia ukweli kwamba hata Glass Kabatini ugongana
Sembuse sisi binaadamu bwana, au siyo Bwana Mbowe.

Mbowe: Ni Kweli Muheshimiwa, lakini kwa Maslahi ya Taifa Letu, Kuna mambo ya Msingi ambayo si busara
Kuyasahu badala yake ni nyema kuendelea kuyakumbuka na kuyakumbusha mpaka pale yatakapopatiwa
Majibu ya uhakika.

Kikwete: Ni kweli, lakini ninachomaanisha ni kwamba kwa sababu tuko hapa kujadili mchakato wa kuandaa katiba
Mpya ni vyema tukasahau yote yaliyotokea apo nyuma kama Maswala ya CHADEMA kutoka nje ya Bunge,
Maswala ya Muswada ama kusomwa mara ya Kwanza ama Mara ya Pili Bungeni na hata Upitishwaji wake Bungeni
Ukizingatia kwamba Bado sijausign kuwa sheria nikitambua kwamba Mazungumzo yetu leo yanaweza kuboresha
zaidi mchakato huu kwa Maslahi ya Taifa.

LISSU: Samahani Mheshimiwa Rais, Kwani wewe binafsi umeuonaje mchakato mzima ulivyokwenda mpaka kufikia
Mswada huo kufikishwa kwako ili usainiwe kuwa sheria.

Kikwete: Tehe tehe tehe, LISSU bwana, tehe tehe tehe, aaaahaaaa. Unajua, haya mambo bwana, ndio maana
mimi nimesema hapa kwamba ni vyema tukasahau yaliyopita ama sivyo mazungumzo yetu yatakuwa mareefu
sana na mwisho wa siku watanzania watatushangaa wote.
Mimi, mimi, mimi dhamira yangu ni kuhakikisha kwamba, Katika mchakato wetu huu, hatufikii kwenye hatua
mbaya kama majirani zetu, sababu haya mambo ukianza kuyawekea maandamano na mihadhara mwisho wake
kwa kweli kabisa hauwezi kuwa mzuri.

Anakunywa Maji kidogo, kisha anaendelea
Pale Kenya pale, wakati wa mchakato wao damu imemwagika pale, sasa mimi siko tayari kuona hili linatokea hapa,
na ndio maana hata kwenye swala la madiwani wa arusha, mimi niliwaelekeza Waziri Mkuu na Katibu wangu Mkama
kuhakikisha Mnakaa, mnazungumza na kulimaliza hili, lakini kinachoendelea pale mi hata sikielewi nikiuliza naambiwa
tatizo ni Lema, vyombo vya habari kwanza vilikuwa vinasema tatizo ni Chitanda, sasa Chitanda simsikii tena
naambiwa tatizo ni Kamanda wa Polisi Zuberi na Mkuu wa Mkoa, mimi sielewi kabisa nini kinaendelea Pale, na hali
hii inachafua kabisa picha ya nchi yetu uko nje.

Anakunywa Maji tena.alafu
Pale Arusha Pale, kile ni kitovu cha Utalii nchini Mwetu, sasa Arusha tukiichezea itatualibia kabisa kabisa, ndio maana
mi nasema swala la Arusha tunatakiwa tukae kama hapa tuzungumze na kulipatia Muafaka. Hii nyumba tunajenga
wote kwa nini tugombee fito Jamani.

Mimi, mimi nasema, wakati tuko Kwenye kikao cha Kamati kuu Dodoma Pale, kuna watu walitaka kukataa nisionane
na CHADEMA, mi nikasema hapana, Lazima nionane nao hawa, kwa sababu hata mimi hili swala la Katiba mpya bado sijalielewa
vizuri.

Kwa hiyo mi nawashukuru sana kwa Moyo wa Uzalendo mliouonyesha, na niko tayari kuonana na nyie na kuzungumza
hata kwenye mambo mengine, sina tatizo hata kidogo na nyie, si unaona bwana, tumezungumza na hakuna mtu
ametoka damu, hii ndio watanzania wanataka kuona.

Mimi kwa kweli niwashukuru sana, na hizi ndio siasa za kizalendo kwelikweli, asanteni sana na karibu tena.
 
Sasa jamani ni kipi kilichokubaliwa?

Mbona hicho kifunguu cha kwanza kiko "general" sana?, CDM walipeleka terms zipi?

By the way naona kila mmoja kasaini kwa rangi anayoiamini! Mnyika bluu, Nchimbi kijani!
 
waziri wa Habari anasign kama nani????????? haya ni makubaliano ya sheria sasa yeye kaja vipi hapo???:A S embarassed:
 
Yaleyale tu hakuna jipya. kwa maana nyingine mswada ata saini. Dah hili changa la macho kweli JK mtoto wa mjini
 
Mkuu Invisible, heshima mbele sana Mkuu!!

Yani kikao cha siku mbili kimehitimishwa na Paragraph Mbili tuu, hii kitu hatuwezi kuipata kwa kina Mkuu.

Gamba Jipya
Hata mimi nimepigwa na butwaa tena katika aya hizo mbili hakuna chochote cha maana zaidi ya sahihi ya Mnyika na Nchimbi!!!
 
Sorry kamanda wangu, yaani na huo mkoba wooooooteeee umebeba hoja mbili???
sasa kitu gani mmekubaliana?


images
 
tangu lini press release ikawa detailed? kimsingi vipo vitu wamekubaliana ambavyo vitaingizwa punde sheria hiyo ikifanyiwa marekebisho .
 
Sheria itaboreshwa kivipi wakati imepitishwa na bunge? Ina maana itarudishwa tena bungeni kufanyiwe marekebisho? Wananchi wanataka kufahamu wazi wazi nini kinaendelea baada ya haya mazungumzo.
 
Ni kweli tumemaliza kikao kwa amani kama tulivyoanza jana. Kimsingi, tumekubaliana kutokukubaliana na madai mengi yaliyowasilishwa. Kwa undani zaidi, subirini taarifa toka ikulu hapo saa mbili usiku.
 
Kwanini tunalumbana bila mwelekeo?hoja zenyewe hazionekani bado tunakuwa kama vikasuku,is this r'lly Jf?
 
Back
Top Bottom