Kikao cha Taasisi za Fedha na Waziri wa Madini, Mavunde

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,756
1,261

ANTHONY MAVUNDE, WAZIRI WA MADINI, TANZANIA

Mwaka jana mwezi Septemba, nilifanya kikao na Taasisi za Fedha na Benki zote nchini chini ya mwamvuli wa Taasisi ya Umoja wa Benki nchini (TBA).

Madhumuni ya kikao kile ilikuwa ni kujadiliana kwa pamoja namna nzuri ya kuifikia sekta ya madini kwa kutoa mikopo ili kuchochea shughuli za Madini nchini.

Kikao hicho kilifungua ukurasa mpya kati ya Taasisi za Fedha na Wizara ya Madini juu ya upatikanaji wa mikopo kwa wadau wa Sekta ya Madini.

Benki zimeendelea kutekeleza tuliyokubaliana,katika kipindi cha muda mfupi ukiacha mikopo iliyotoka kwa kampuni kubwa hapa nchini za Madini,Benki ya CRDB imetoa mkopo kwa wachimbaji wadogo wa Tsh Bilioni Kumi (10,000,000,000 Tzs*) kwa ajili ya ununuzi wa mitambo ya uchenjuaji,mashine za uchimbaji na utoaji huduma migodini.

Hii ni hatua kubwa katika kuijengea sekta ya madini na wadau wa madini imani ya kukopesheka ili kuchochea zaidi ukuaji wa sekta.

Anthony P. Mavunde
Waziri wa Madini.
 
Back
Top Bottom