Kikao cha Rais na wabunge wa CCM huko Dodoma kimekwendaje?

SubiriJibu

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
1,805
1,874
Wakuu,

Magazeti ya wiki hii na hata kuanzia wiki jana yalijazwa na habari kwamba Rais atakaa kikao na wabunge wa CCM ikizingatiwa kwamba wako huko kupitisha bajeti ya serikali.

Sasa sijui imekuwaje hata magazeti yote hayasemi lolote wakati tumezoea hata kikifanyika kwa siri namna gani lazima kilochoongelewa kitamwaga gazetini.

Cha ajabu hata hapa JF naona kimya kama vile pamepigwa ganzi fulani.

Hebu waheshimiwa sana mnaojua kilichojiri tufunulieni tujue yaliyotokea.

Wenu mwana JF.
 
Labda walimtoa nje nanii na yule aliekuwa waziri wa nanii.....
 
Yule Mzee Tupatupa wa Lumumba yuko wapi siku hizi? Angetupatia taarifa hii mara moja kama kuna lolote limetokea.
 
Safari hii wamepigwa mkwara mzito baada ya kikao kilichopita kuvujishwa kila yaliyosemwa kwenye caucus yao .........

Maana baada ya kikao kile ndiyo tukajua kumbe 'Ba'Bashite' ndiye aliyezuia Bunge lisionyeshwe Live!

Tukajua pia kumbe wabunge wa Sisiem walipewa 'mlungula' wa milioni 10 ili kuwaziba mdomo!

Tukajua pia kumbe kuna baadhi ya wabunge wa Sisiem walikuwa na mkakati wa kumpigia kura ya kukosa imani na PM ili serikali iundwe upya......
 
Back
Top Bottom