Kikao cha pili bunge la kumi: Je vijana tuna la kujivunia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikao cha pili bunge la kumi: Je vijana tuna la kujivunia?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NewDawnTz, Feb 22, 2011.

 1. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot]
  Hatimaye juma lililopita tumeshuhudia kufungwa kwa kikao cha pili cha bunge la kumi.

  Kimsingi,basing on historia ndogo niliyonayo kichwani, hili linaweza kuwa ni bunge lenye wabunge wengi vijana zaidi ya bunge lolote ambalo nimelifahamu hapo kabla (stand to be corrected please). Ni kweli bado changamoto ya kujaa wazee wasiokuwa na tija ndani ya bunge inalitafuna bunge letu, lakini angalau kwa sasa tuna wabunge wengi vijana zaidi ya hapo awali.

  Wengi tumeona na kushuhudia walichofanya wabunge wetu (japo maeneo mengine mgao umekuwa changamoto).
  Hata hivyo swali langu kubwa ni je vijana tumeanza kuona la kujivunia kwa wabunge ambao ni vijana wenzetu?

  Wako ambao wamepata tumaini kuwa vijana hawa watatoa changamoto kwa bunge hili na hatimaye kusaidia mabadiliko katika mifumo kadha wa kadha.

  Nimetembea maeneo kadha wa kadha kwa majuma kadhaa kwa shughuli za kiofisi, na nimebahatika kukutana na kuzungumza na vijana wengi kutaka kupata picha na mtazamo wao juu ya bunge hili na vijana wenzetu walioko bungeni:
  [/FONT]​

  • [FONT=&quot] Wako wanaomzungumzia January Makamba kuwa kauli zake katika kikao hiki cha bunge kinaonesha mwamko wa vijana kutaka mabadiliko ya kimfumo na huenda akatutoa hasa kwa kuonesha wazi kuwa kuna "mafungu" yasiyo eleweka yanayotolewa kwa wajumbe wa kamati za ambayo huathiri maamuzi. Ameweka wazi kuwa kamati chini yake haitakubali upuuzi huu
   [/FONT]
  • [FONT=&quot] Wako wanaomzungumzi Lusinde kibajaji kilichoangusha tingatinga kama aibu kwa vijana ndani ya bunge letu kwa kauli zake za utata....[/FONT]
  • [FONT=&quot] Wako wanaozungumzia watu kama wakina Mnyika kama nguzo na mwamko mwingine ndani ya bunge letu kwa mtazamo na msimao usiotarajia kwa wazee ambao ubongo wao umechoka na unawaza kujikusanya mara watakapomaliza utumishi wao
   [/FONT]
  • [FONT=&quot] Wako wenye mashaka kuwa wengi wa vijana hawa (has jinsia ya kike) ni wa mgongo wa kuteuliwa na huenda wasiwe na lolote la maana zaidi ya kutetea maslahi ya waliowateua (au kuwapa uhakika wa kuwa wateule) na si vijana wenzao hasa kwa kuzingatia wengi wao wanatia utata juu ya vigezo na uadilifu wao kuwastahilisha nafasi ya uwakilishi.[/FONT]
  • [FONT=&quot] Wengi nimewasikia wakihofu vijana hawa hawataweza kuhimili ushawishi wa wazee na wengi wao wataburuzwa nao kwa ahadi itakayowapa cheap popularity au benefits nyinginezo. Wako wanaotumia mfano wa Kafulila na Hamad Rashid ku-justify hili lakini pia uwingi wa vijana wa viti maalum ambao hofu kubwa ni kama nilivyo taja hapo juu
   [/FONT]
  [FONT=&quot]Swali kubwa, ni je vijana walioko bungeni wameonesha kutambua kiu waliyonayo vijana wenzao angalau tu kwa kikao hiki cha bunge? Je wameonesha kuweza kuhimili mikiki ya wazee na kukataa kutumiwa for cheap popularity?

  [FONT=&quot]Je vijana tulioko nje ya bunge tumepata tumaini lolote kwao? Je tuna jambo la kuwashauri (ikiwezekana mmoja mmoja) kama vijana wenzetu kwa kile tulichoona kwenye bunge hili na kutaka labda wajisahihishe maeneo fulani kusudi kubeba yale matumaini ambayop vijana wenzao tunayo kwao?

  Uwanja ni wetu tuwashauri maana wengi wako humu na wanaweza kupata ushauri wa kutosha kutoka kwetu vijana wenzao

  Nawakilisha[/FONT]
  [/FONT]
   
Loading...