Kikao cha NEC Zanzibar: Karume hataki kuongezewa muda! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikao cha NEC Zanzibar: Karume hataki kuongezewa muda!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Field Marshall ES, Jan 22, 2010.

 1. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - According to the dataz, Jumapili hii kutakua na kikao cha dharura cha CCM. Habari hizi tumezithibitisha toka kwa vigogo mbali mbali wa CC walio katika safari za mbali, ambao wamefahamishwa kuanzia jana kuanza kurudi Mjini kwa ajili ya kikao hiki.

  - Bado hatujapata what is the agenda, lakini kuna tetesi nzito sana kwamba kutawaka moto huko ndani, hasa kuhusiana na kusajiliwa kwa chama kipya cha CCJ, ambacho kinaaminika kuwa na waasisi wengi vigogo kutoka CCM.

  - Kama kawaida tunafuatilia kwa karibu sana, kujua kinachoendelea sasa na mpaka siku hiyo ya kikao, zikipatikana tutahabarishana hapa hapa uwanja wa JF kumkoma nyani!

  Respect.


  Field Marshall Es = Ni Wazee Wa Sauti Ya Umeme!
   
 2. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Vipi Field Marshal, kikao cha baraza la mawaziri kulikoni?
   
 3. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Tumekusoma FMES, tunategemea JF tutakuwa wa kwanza kupata kilichojiri kama ambavyo umetujuza juu ya kikao hicho muhimu.

  Respect!
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Jan 22, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,385
  Trophy Points: 280
  Yanayoendelea Zanzibar yanawatisha zaidi kuliko hili la CCJ.. they can control CCJ.. Zanzibar is the whole new ball game. Don't hold your breath. Wanajua wakicheza vibaya tu wataipa CCJ nguvu isiyostahili so sitoshangaa kuwa nayo inawaumiza kichwa ni kama kupata "double punch" a hook and a jab!
   
 5. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2010
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Duh! kamati kuu inaitishwa J2!! naona maji yanazidi unga, walidhani uongozi ni kugawana madaraka tu!!
   
 6. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Even ccj is not that easy. Natamani mpasuko uwe rasmi baada ya hicho kikao j2
   
 7. Chechetuka

  Chechetuka JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 549
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naona kama maneno ya Marehemu Baba wa Taifa yanatimia vile... Alisema kuwa "chama cha upinzania wa kweli kitatoka ndani ya CCM". Inawezekana neema hii ipo karibu sana. Hebu tusubiri.
   
 8. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #8
  Jan 23, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Iwapo CCM wangekubali matokeao halali ya uchaguzi uliofanyika huko Zanzibar mwaka 1995 au yale ya 2000, huenda sasa hivi wasingekuwa na presha na siasa za zanzibar kabisa; kwanza huenda CUF ingeshindwa kudeliver katika kipindi cha kwanzana na kutupiliwa nje katika uchaguzi uliofuata. Sasa hivi walichokutana nacho ni mwiba mkali sana kwao. Karume anataka abakie madarakani, wakati Hamadi naye anataka angalau naye awepo madarakani kabla ya siku zake za kisiasa hazijaisha: yuko ukingoni sasa. Karume anajua kuwa Katiba haimruhusu, na Hamadi anajua kuwa hawezi kuyapata kwa njia ya uchaguzi. Jawabu wote wamelipata, Karume ameahidi kumpa Hamadi madaraka kikubwa katika serikali yake kama tu Hamadi huyo atamsaidia Karume kubaki madarakani.

  Kati ya Hamadi na Karume, nadhani kuwa Karume ni smart sana kwani sasa hivi anamtumia Hamad kuwa mpiga debe mkuu. Hakuna uhakika iwapo Karume atampa kweli hayo madaraka akishakubaliwa kuendelea kubaki madarakani.

  Zanzibar kuna ugonjwa mkali sana wa madaraka; kila inapofikia mwisho wa kipindi cha uraisi, lazima ziwepo mbwembe za kutaka kumuongezea muda. Nakumbuka hata wakati wa Mwinyi anamaliza mkataba wake wa kupanga kwenye lile jumba la magogoni, ngoma ndogo ndogo zilianza kupigiwa kumtaka aendelee na madaraka, lakini mchonga akingilia kati.
   
 9. Chechetuka

  Chechetuka JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 549
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wahenga walisema... "Lisemwalo lipo, na kama halipo linakuja".
   
 10. Chechetuka

  Chechetuka JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 549
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna siri ambayo imejificha nyuma ya sakata hli za Zenj. Baada ya matokeo ya daftari la wapiga kura kuhakikiwa ktk visiwa hivyo, takwimu zinaonyesha kuwa kiongozi wa chama kikuu cha upinzania atashindwa ktk kura za Urais na hivyo kufanya yale yote aliyokuwa anayalalamikia siku za nyuma ni uongo. Kwa kufanya hivyo, atakuwa anakiua chama chake kisiasa ktk visiwa hivyo.
  Njia pekee aliyoiona ya kumnusuru yeye na chama chake ni kumuongezea kiongozi wa sasa muda wa miaka miwili a mitatu ili wao waweze kuzirudisha kura ktk kipindi hicho. Na hapa mgombea atakayesimamishwa sio Hamad Rashid, bali nia Juma Duni.
   
 11. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kitendo cha watu wengi kuongelea zanzibar na mambo ya ina dalili mbili:-

  1. Madai ya wanzazibar kwamba CCM (bara) imefanya zanzibar koloni lake yanaonyesha ni kweli kwani kama bunge lao (halali) linakubali kubadilisha katiba yao ili rais aendelee what is the problem?? mbona uganda Mu7 amebadilisha hakuna aliyepiga kelele?? wao nao nchi huru ati!

  2. Kwamba CCM (bara) ilikuwa inafaidi sana wazanzibar wakigombana na kufurakana na sasa wamedhihirisha kina makamba na msekwa kwa ndimi zao.. ndio source ya fitna ...(divide and rule)

  Bottom line: I care less zanzibar rais wao akitaka aendelee milele maana watamtoa wenyewe wanao uwezo waachwe wenyewe bara washugulikie mambo yanahusu Tanganyika yao. Wameonyesha wanaweza kuwa na upinzani wengi kuliko hata wabara ambao bunge nzima wako 5 shame.
   
 12. Chechetuka

  Chechetuka JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 549
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CUF hawako tayari kuingia kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu kwa kigezo hicho cha kushindwa ktk kura za Urais, hivyo wapo tayari kwa gharama zozote kuhakikisha uchaguzi Zenj haufanyiki angalau kwa miaka miwili ili wao wapate muda wa kuzirudisha kura hizo walizozipoteza.

  Njia pekee ya kistaarabu ya kutokuingia ktk uchaguzi ni kuibadilisha Katiba na kumuongezea Karume muda kwa kisingizio cha kumpa nafasi zaidi ya kumalizia mageuzi ya kisiasa ktk visiwa hivyo. Mabadiliko haya wanayotaka kuyafanya ni maalumu kwa muda huu tu wa miaka miwili au mitatu, baada ya hapo hawayahitaji TENA.

  Karume na wapambe wake wanaona hiyo ni neema ya kufanya mambo yao na kurekebisha baadhi ya sheria ambazo zitamuongezea kinga ya kutokusumbuliwa pale atakapomaliza kipindi chake cha utawala. Kuna taarifa kuwa tayari kuna watu wameanza kumtisha Karume kuwa akimaliza muda wake atapelekwa mahakamani. Hii inathibitishwa na kauli ya hivi karibuni ambapo Karume hakukataa kuendelea kutawala, bali alisema kuwa Katiba ya nchi hairusu vipindi vitatu vya utawala, na ndio maana ktk marekebisho wanayotaka kuyafanya ni ya muda maalumu wa miaka mitatu tu, hayatakuwa ya kudumu. Kama Karume angesema kuwa yeye kama Karume hana nia ya kugombea tena, nadhani angekuwa amekata mzizi wa fitna yote hii. Lakini yeye aliitupia lawama Katiba ya nchi.

  Kuna kundi jingine la wale wote waliojiandaa kuingia ktk kiny'ang'anyiro cha Urais mwaka huu. Hawa hawatakubali kuona Karume anaongezewa muda, hivyo watapigania kuhakikisha mabadiliko hayo hayatokei. Lakini hatari kubwa ni kuwa, CUF wanahitaji nusu ya WAWAKILISHI wa CCM kuwaunga mkono ktk mpango wao huo. Jambo hili linawezekana kabisa kama pesa itatembea kwa wajumbe.

  Kuna tetesi kuwa kundi la "Mafisadi" ndio linalo ratibu mchakao huo mzima, hivyo pesa sio hoja kwao. Mafisadi wamepanga mashambulizi yao ndani ya CCM, na kwa Zenj huo ndio mchongo wao.
   
 13. Chechetuka

  Chechetuka JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 549
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati tunasema tuwaachie Wazanzibar wajiamulie mambo yao, na Bara watizame ya kwao, hapa tunapeleka ujumbe kuwa Muungano uliopo hivi sasa ufe. Lakini ni vizuri wakati tuaua Muungano huu tukumbuke historia ya visiwa hivi (Pemba na Unguja).

  Sidhani kama Tanganyika itapata hasara ya kiuchumi na kiulinzi kama Muungano huu utavunjwa. Lakini tujiulize, kuna Wanzanzibar wangapi Bara amabo wamewekeza biashara zao?

  Kumbuka kuwa, mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar yataingizwa ktk Katiba ya Muungano, je Wabara wapo tayari kuahirisha uchaguzi mkuu kwa kusubiri mabadiliko ya Zanzibar kwanza?
   
 14. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Wanaoingia kwenye hiyo kamati kuu siku zote hwua wanasema kwamba katika ishu inayowaudhi sana wajumbe wa hii kamati ni hii ya kuongeza muda, katika kamati hii hii Salmin alimtaka Mwalimu kufafanua nini maana ya yeye kuendelea na kofia moja na sio kuachia zote mbili mara moja, ni kamati hii hii juhudi za Kolimba RIP, kutaka Mwinyi apewe term ya tatu zilipiga mwamba na kuishia kung'olewa ukatibu, na ni kamati hii hii juhudi za Mkapa kutaka term ya tatu ziliuliwa na Sumaye tena kwa ukali sana, again ni hii hii kamati kuu ilimuadhibu vikali Salmin na juhudi zake za kutaka term ya tatu,

  - Kwanza walimshangaa sana na infact, waliamua kumtoa hata mgombea wake Dr. Bilali na kumpa mgombea aliyeshindwa Amani Karume according to mjumbe mmoja hii ilikuwa ni hasira ya wajumbe dhidi ya Salmin na hii idea ya term tatu, sasa kwa nini Karume anaamini kwamba he is defferent? Salmin alikua na a very strong case on his side kwamba ni yeye peke yake ndiye mwenye kuweza kuwathibiti CUF, lakini CC wakamtupilia mbali sana, na huyu naye naamini wataishia kumtupilia mbali sana, infact Salmin alitishiwa na wajumbe wengi kwamba wako radhi kumpa Seif urais, kuliko kumpa term tatu Salmin!

  - Zanzibar wana tabia ya kutishia nyau, na wanafahamu sana kwamba maamuzi ugly ya kuwahusu huko Visiwani huamuliwa na wajumbe wa CC bila kumhusisha rais, makamu wala waziri mkuu, au Rais wao maana mara ya mwisho kwenye kumtwanga Salmin na term zake tatu, Mwenyekiti wa CCM Mkapa aliombwa kutoka nje ya kikao ili wamshugulikie kikamilifu, Karume naye ataishia kilio cha mbwa tu, tena very soon kule Chimwanga!

  - Sio siri kwamba recently Karume amekuwa akijaribu sana kuwa a political genius, lakini kule CC wazee kina Almeir, Khatibu na Balozi Idd, wako kimya wanamuangalia tu watch siku yake itakapofika!

  Respect.

  FMEs!
   
 15. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Damn, siamini kama kuna ujinga wa third term Zanzibar. For sure utagomba mwamba, zanzibara kuna wengi tu wanaweza kuongoza sio Karume peke yake na si kweli kuwa mwafaka bila Karume utayeyuka, huu ni utoto. Hali ya ushwari katika siku karibu na uchaguzi Zanzibar ni ya kawaida ni fooling trick wanayofanyiwa CUF wakati wote.

  As to CC jumapili, tuombe mungu chama kipya kianzishwe. Tunatakiwa tuwe na chama chenye nguvu inayoendana na CCM. Chama chetu ni kikubwa sana na kimemonopolize siasa. Tuombe tu.
   
 16. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #16
  Jan 23, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hivi ccm muda wote hawakuwa na taarifa za kuanzishwa kwa ccj hadi kimetangazwa kwenye magazeti?
   
 17. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #17
  Jan 23, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,322
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Ndio matatizo ya kudharau umuhimu wa kufanya changes mara inapostahili. Huwa zinakuja kama thunami na kishindo chake kikasikika dunia nzima. Hiyo CCJ na hata yanayoendelea visiwani ni moja ya tabia ya kina baba haambiliki ambao ni wengi kwenye chama kuendeleza arrogance zao na kusahau kuwa kama wakiendelea kuchezea muda basi mambo muhimu yatanyang'anywa mikononi mwao na kuchukuliwa na wale wanaostahili.
  Huu sio muda wa kuendeleza dharau kwenye mambo ya msingi
   
 18. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #18
  Jan 23, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wacha livunjike hilo CCM mbona itakuwa faida kwa nchi..kutakuwa na watu waliofanya kazi serikalini wako upinzani that is health for our country political framework.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Jan 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,385
  Trophy Points: 280
  Ninalozungumzia la Zanzibar siyo suala la term tatu tu (hiyo ni hoja ya kupandia mgongonai). Kimsingi hoja ni kuwa Zanzibar watataka makubaliano ya Muungano yazungumzwe tena na vipengele vya muungano viangaliwe ama sivyo wao wataamua kutoka nje ya Muungano. Wakichukua msimamo huo Zanzibar nzima italipuka kwa shangwe.

  Kitakachotokea watu wenye asili ya bara wataanza kunyanyaswa na kutakiwa kuridishwa "kwao" bara na watakapochelewa chelewa damu itaanza kumwagika. Na ndipo tutaona maelfu ya wale wanaoitwa "Watanganyika" wakitafuta mahali pa kukimbilia...

  Na tuombee hoja iwe hiyo ya kisiasa tu; itakapoingizwa hoja ya dini tu kama ambavyo imejaribiwa mara kadhaa, tutashuhudia makanisa yakitakiwa kufungwa siku za Jumapili na hata watu kulazimishwa kuondoka.

  Kikwete hatojua la kufanya.
   
 20. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #20
  Jan 23, 2010
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  UNABI UMETIMIA? conecting the dots to ur article, why imerudiwa kuchapishwa
   
Loading...